Hata sisi huku kwetu tunapambana na genge la mwenyekiti ili kurudisha demokrasia ya kweli ndani ya chama chetu. Tunaomba chawa wa mwenyekiti na mwenyekiti mwenyewe watambue kuwa hiki chama ni cha wananchi na sio cha mtu binafsi.
Haiwezekani mwenyekiti atumie vipesa vyake alivyokusanya kupitia ruzuku mbali mbali kujimilikisha chama. Lengo la kukiita chama chetu "chama cha demokrasia na maendeleo" lilikuwa ni kutaka kuwaonesha wananchi na wanachama wetu kuwa chama chetu kinasimamia demokrasia ya kweli tofauti na sasa chama kimegeuzwa cha kisultani kinasimamia genge la mwenyekiti na familia yake.
Wenye maono ya kweli na chama wanazuiwa kupewa uongozi wa juu nk, huku ubadhilifu mkubwa wa mali za chama ukiendelea chini ya uongozi wa sultani na genge lake.
Mwaka huu tutahakikisha mwenyekiti na chawa wake wanaheshimu katiba ya chama iliyowekwa chini ya waasisi wetu kina mzee Mtei na hayati bob Makani, na tutarejesha demokrasia ya kweli ili kila mtanzania mwenye sifa zinazostahili kuongoza chama aweze kuongoza chama chetu kwa kipindi cha miaka mitano au kumi kama katiba yetu inavyosema.
Tushachoka kuwa chini ya uongozi wa kisultani. Chawa mnaruhusiwa kuja kwa wingi kunipinga kwa hoja.
View attachment 2173705
View attachment 2173706