Suala la kuwapo au kutokuwapo kwa katiba mpya kwa sasa halina mbadala tena. Ni wazi kuwa watanzania walio wengi tunahitaji katiba mpya na iliyopo haitufai tena. Tofauti iliyopo ni kwenye viwango (extent) tu.
Ni dhahiri kuwa mchakato huu usiporuhusiwa kwa hiari, mashinikizo yatafuata. Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.
Katiba mpya haizuiluki. Kwa hiari au kwa shuruti katiba mpya yaja. Kwa hiari, Mama ataibuka mshindi kwenye hili. Kwa shuruti, mama anajiweka matatani.
Chuki inazidi kumea baina ya watu na hata baina ya watu na serikali. Hali hii inahitaji ufumbuzi sasa na haiwezi tena kupuuzwa. Mzizi wa fitina ukiwa mapungufu ya wazi kwenye katiba iliyopo isiyokidhi mahitajio.
Mama Samia tunakuombea ukaione busara iliyoko katika jambo hili mapema na hatimaye ukaibuke kidedea.
Beberu hakukosea sana kusema: "Time time, before time times you."
Ninawasilisha.