Katiba Mpya: Heri Rais Samia akaruhusu mchakato, asisubiri mashinikizo

Katiba Mpya: Heri Rais Samia akaruhusu mchakato, asisubiri mashinikizo

Baada ya kuwasiliana moja kwa moja na Nigrastratatract ninaamini kuwa hitajio la Katiba mpya ni kubwa ikiwamo pia ndani ya CCM:

IMG_20210628_001547_135.jpg

Hii ikiwa ni comment #25 kwenye uzi huu:

Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Katiba mpya ni hitajio letu sote.
 
Tofauti yetu sisi na watu weupe ni ustaarabu, binaadamu wenzetu hao wametuzidi ustaarabu na ndio kitu cha kwanza kinachowaongoza kabla ya vitu vyengine na ndio inakuwa rahisi hata kufuata hayo mengine. Sisi utakuta kitu kitu kizuri kimejengwa masiku kadhaa tu ila unakuta watu washaharibu bila kujali kwamba kitu hicho ni kwa manufaa yao wenyewe, ukiangalia matatizo ya afrika ni yaleyale tu sasa sidhani kama ni kwa sababu afrika tumekosa katiba bora.
Ustaarabu ni kitu muhimu sana tungekuwa na ustaarabu hata katiba ya sasa tungeiheshimu ila sasa ustaarabu hatuna.
 
Mkuu siyo Rahisi ni Hivyo, Ngoja tuone, maana CCM wanajua ya kwamba Katiba Mpya yenye tume huru ya Uchaguzi ndio Mwisho wao. Je wako tayari Kukabidhi nchi, kwa Maana Katiba Mpya Means CCM Kwa Kheri kama ilivyokuwa KANU ya Kenya.
Watakubali tu hakuna namna nchi siyo mali yao binafsi
 
Tofauti yetu sisi na watu weupe ni ustaarabu, binaadamu wenzetu hao wametuzidi ustaarabu na ndio kitu cha kwanza kinachowaongoza kabla ya vitu vyengine na ndio inakuwa rahisi hata kufuata hayo mengine. Sisi utakuja kitu kitu kizuri kimejengwa masiku kadhaa tu ila unakuta watu washaharibu bila kujali kwamba kitu hicho ni kwa manufaa yao wenyewe, ukiangalia matatizo ya afrika ni yaleyale tu sasa sidhani kama ni kwa sababu afrika tumekosa katiba bora.
Ustaarabu ni kitu muhimu sana tungekuwa na ustaarabu hata katiba ya sasa tungeiheshimu ila sasa ustaarabu hatuna.
Umesema point sn mkuu
 
Kwa upepo unavyovuma, hali ya uwanja ilivyo na watu nao walivyo dhamiria, Mama mbona kawafungua macho wengi?

Wasiotaka kurejea tulikokuwa si wachache. Wanahitaji kesho ya uhakika. Inaeleweka kuwa inawezekana lakini si bila katiba sahihi.

Mola amjalie Mama kuiona busara iliko. Urais si lelemama hakuna kulala.

La Katiba mpya liko njiani linakuja. Uchaguzi ni kwake. Kusubiri mashinikizo au kuwahi na kujizatiti kileleni.
CCM wanadhani nchi ni mali yao binafsi
 
Mkuu siyo Rahisi ni Hivyo, Ngoja tuone, maana CCM wanajua ya kwamba Katiba Mpya yenye tume huru ya Uchaguzi ndio Mwisho wao. Je wako tayari Kukabidhi nchi, kwa Maana Katiba Mpya Means CCM Kwa Kheri kama ilivyokuwa KANU ya Kenya.
Naunga mkono hoja. CCM hawawezi kunoa panga litakalo wakata wao kwanza.
 
Naunga mkono hoja. CCM hawawezi kunoa panga litakalo wakata wao kwanza.

Hapa ni mafukuto ya wazi tokea ndani kwa wafia chama:

Mama ana hiari kuamua, iwe kabla au baada ya mashinikizo.
 
Katiba tuliyo nayo haiheshimiwi na baadhi ya watu kwa sababu ya mapungufu na mianya ya wazi iliyomo.

Inahitajika mpya itakayo hakikishwa kuwa haiachi mianya kama ilivyopo.

Mfano: kwanini wawepo watu wasioweza kushitakiwa kwa mapungufu yao yoyote kwa mujibu wa katiba?

Itaheshimiwa katiba vipi kwenye mazingira kama haya?
Hiyo katiba mpya itajisimamia yenyewe au itasimamiwa na watu hawa hawa mnaowalalamikia kila siku kuvunja katiba, Kama kweli katiba iliyopo inakanywagwa, kutakuwa na guarantee gani kuwa hiyo katiba mpya haitakanyagwa?

Katiba inaweza kuwa nzuri Sana na isifuatwe Kama mfumo wa uongozi utaendelea kuwa ule ule wa siku zote.

Vyama vya upinzani jiimarisheni kisera ili mpate ushawishi na kuaminika kwa wananchi, itakuwa rahisi hata mkiitisha maandamano ya kitaifa watu watawaelewa na kuwaunga mkono.
 
Katiba si kwa ajili ya vyama vya upinzani tu. Katiba ni kwa wananchi wote.

Mapungufu katiba iliyopo ndiyo yanayoyaleta mikanganyiko unayoiongelea. Hivi unayatambua haya:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Nk nk.

Kwenye mazingira haya asiyewajibishwa kwa mujibu wa katiba atawajibika vipi kwa katiba hiyo?

Hapa chini ni mawazo tokea baina ya wana CCM wafia chama:

IMG_20210628_001547_135.jpg

Katiba mpya ni hitajio sahihi la wananchi sasa. Hili si hitajio la vyama vya siasa.

Uzi huu hapa chini una ufafanuzi zaidi:

Asisubiri mashinikizo kutoka wapi? Sisi kama Watanzania kipaumbele chetu sio Katiba kwasasa tumuache mama afanye kazi.
 
Asisubiri mashinikizo kutoka wapi? Sisi kama Watanzania kipaumbele chetu sio Katiba kwasasa tumuache mama afanye kazi.

Hahaahaaa haa 😂😂😂😂.

Uhamiaji kwa mwaka mmoja tu uliopita, wamekamata wahamiaji haramu zaidi ya 44,000. Wewe hawajakufia ulipo?

Watanzania ninaongelea miye wako hapo kwenye red:

IMG_20210628_114437_573.jpg

Habari ndiyo hiyo.
 
Hapa ni mafukuto ya wazi tokea ndani kwa wafia chama:

Mama ana hiari kuamua, iwe kabla au baada ya mashinikizo.
Sasa nimekuelewa mleta mada. Kumbe hii kitu ni serious Sana.

Jiwe alisurubu makundi yote wakiwemo ccm. Hakuna anayetaka ile shuruba irudi tena.
 
Sasa nimekuelewa mleta mada. Kumbe hii kitu ni serious Sana.

Jiwe alisurubu makundi yote wakiwemo ccm. Hakuna anayetaka ile shuruba irudi tena.

Ni wazi kuwa makundi yote yanachopishana ni kufahamiana tu. Hii ilimhusu hata yule wa tuzo za BET pia.

Tulipo ni kwamba tunashangaana tu. Ndiyo maana kando ya Nigrastratatract, si Wakudadavuwa, johnthebaptist, Idugunde wala wenzao ameweza kutokea kutupa ufafanuzi pamoja na kuwaomba hivyo kwa majina:

Kuna uwezekano mkubwa kuwa waungwana, letu sote ni moja ambalo ni jambo jema tu.
 
Back
Top Bottom