Hiyo katiba mpya itajisimamia yenyewe au itasimamiwa na watu hawa hawa mnaowalalamikia kila siku kuvunja katiba, Kama kweli katiba iliyopo inakanywagwa, kutakuwa na guarantee gani kuwa hiyo katiba mpya haitakanyagwa?
Katiba inaweza kuwa nzuri Sana na isifuatwe Kama mfumo wa uongozi utaendelea kuwa ule ule wa siku zote.
Vyama vya upinzani jiimarisheni kisera ili mpate ushawishi na kuaminika kwa wananchi, itakuwa rahisi hata mkiitisha maandamano ya kitaifa watu watawaelewa na kuwaunga mkono.
Katiba si kwa ajili ya vyama vya upinzani tu. Katiba ni kwa wananchi wote.
Mapungufu katiba iliyopo ndiyo yanayoyaleta mikanganyiko unayoiongelea. Hivi unayatambua haya:
1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Nk nk.
Kwenye mazingira haya asiyewajibishwa kwa mujibu wa katiba atawajibika vipi kwa katiba hiyo?
Hapa chini ni mawazo tokea baina ya wana CCM wafia chama:
Katiba mpya ni hitajio sahihi la wananchi sasa. Hili si hitajio la vyama vya siasa.
Uzi huu hapa chini una ufafanuzi zaidi:
Mabibi na mabwana kumekuwa na vita vikali vya mitandaoni. CCM, Chadema, Corona, Legacy, tuzo za BET nk. Kwa hakika imekuwa ni patashika nguo kuchanika. Hata hivyo pana haja ya kufanyika tathmini za msingi. Kuna uwezekano mkubwa kuwa waungwana, letu sote ni moja. Yawezekana ni kwa sababu ya...