Katiba mpya isipopatikana 2014; Nini cha kufanya?

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2011
Posts
705
Reaction score
441
Wana JF,

Kama mjuavyo serikali ipo mbioni kukusanya maoni ya kuandikwa kwa katiba Mpya ambapo hitaji hilo hasa litakuwa na mantiki ya kisiasa ikiwa itapatikana kabla ya mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu. Mantiki hiyo ya kisiasa inatokana na ukweli ulio wazi kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imelalamikiwa vya kutosha na wananchi wengi kwa kutokutenda haki kwenye chaguzi mbali mbali (Hasa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010).

Baadhi yetu tuliobahatika kuisoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tunakubaliana bado kimsingi kuwa ilipitishwa ikiwa na mapungufu ambayo tayari yameendelea kuonekana wazi wazi kwenye mchakato wa ukusanywaji wa Maoni kwa wananchi. Mapungufu hayo (Japokuwa mengine yanapuuzwa na Tume) yanaweza kuukwamisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya kabla ya 2015 kama ambavyo hata Serikali yenyewe ilivyopendekeza.
Baadhi ya mapungufu hayo ni Suala la Muundo wa Serikali; (Uhai wa Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano).

KURA YA MAONI.
Kama sheria inavyoelekeza ni lazima 51% ya Wazanzibari waupitishe Muswada huo wa Katiba na 51% ya Watanganyika. Kwa hali ilivyo nchini kwa sasa ni vigumu SANA pande zote mbili kukubali kwa kiwango hicho hasa ikizingatiwa Kuwa tayari kuna maneno ya chini chini kuwa CCM na viongozi wake hawana mpango wa kukubali muundo wa Serikali tatu (Ikiwa utapendekezwa na Tume. Wakati huo huo msimamo wa Wazanzibari unajulikana.

Kama vijana na Watanzania wengine, kwa haki tuliyopewa kikatiba sasa nadhani ni wakati muafaka wa kujadili nini cha kufanya ikiwa mpango huo wa Serikali utakwama?.
 
Nakuambia kwa jinsi hii tume ya kukusanya maoni inavosuasua 2014 hamna kitu, chezea CCM wewe
 
Kila nikiangalia jamii yangu hii ya kitanzania na namna ya mfumo wetu unavyofanya kazi, naamini kuwa ni janga zaidi kukimbilia "katiba mpya"....

Ingekuwa poa tu kama kuna vitu vidogo vidogo tungevirekebisha kwa sheria na mabadiliko ya katiba ya sasa!!


Tujikumbushe ukweli mchungu.


"Narudia kusema kwamba tusifanye mambo kwa haraka kwani hatuna tunakoenda. Tupo hapa, na tunataraji kuwa hapa kwa miaka milioni ijayo, kama si zaidi. Kwa nini tunafanya mambo kama vile tuko mapitoni (transit) tukienda mahali pengine?"

Rai Ya Jenerali

 
Wana JF,

Mleta mada ameona mbali. Katiba iliyopo sasa ni mtaji mkubwa kwa chama tawala hasa ktk muhundo uliopo wa tume ya uchaguzi. Kama tukingia uchaguzi 2015 bila mabadiriko ya katiba na bila ya mabadiriko ya tume ya uchaguzi hupo uwezekano mdogo wa kupata viongozi wazuri wa ktk nchi hii kwa sababu ya uchakachuaji.

Chakufanya: 1) Vyama vya upinzani (Chadema) washinikize mabadiriko ya tume ya uchaguzi
; 2) Chadema wasisitishe speed yao ya M4C. Zaidi wajikite vijijini na kuwaelimisha watu juu ya mabadiriko; 3) Mikakati ya kulinda kura za wapiga kura zizidishwe la sivyo...4)
 
CDM wameukubali mchakato wakubali na matokeo. Wameingiza mahindi kwenye mashine zikitoka pumba au unga wawe tayari kwalo
 
CDM wameukubali mchakato wakubali na matokeo. Wameingiza mahindi kwenye mashine zikitoka pumba au unga wawe tayari kwalo
CDM walishinikiza mchakato wa katiba Mpya...(siyo kukubali mchakato tu.) ndio utajua kwanini tunasema CDM ni Chama MAKINI..
Its simple, Zikitoka pumba au unga tutazirudia tena kenye mashine, mpaka kitaeleweka tu...
 
CDM wameukubali mchakato wakubali na matokeo. Wameingiza mahindi kwenye mashine zikitoka pumba au unga wawe tayari kwalo

Mkuu nilitaka tujadili nje ya Chadema, Tujadili sisi kama Watanzania wa kawaida wenye uhitaji mkubwa wa Katiba mpya na Uongozi bora (Si Utawala Bora).
 

He! Mkuu una moyo
 

Rais Jakaya Kikwete ni mtaalam wa kusoma kwa haraka sana 'Mwenendo wa hali ya kisiasa nchini'. Alichokifanya (Kukubali kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya katiba ni kuzima 'Hali mbaya ya upepo wa kisiasa' iliyokuwa imkumbe mapema tu baada ya kutangazwa kuwa Mshindi wa kiti cha Urais 2010. Amefanikiwa kwa muda kutuliza hali hiyo japokuwa 2014 inaweza kuwa mbaya mara mia kuliko ambavyo ingekuwa mwaka 2010 kama angefanya ulichokiona hapa (Kukubali kuliagiza bunge kufanya marekebisho ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Hiyo ingemsaidia sana kuliko wimbo huu ambao kimsingi unamaliza rasilimali kwa matarajio hafifu.
 

Mkuu,
Aya ya kwanza ya mchango wako ni nzuri (Kuacha upungufu mdogo wa fasihi andishi). Kwanza kuna nafasi za kuteuliwa ambazo Watanzania wengi hatutaki ziendelee kuwepo baada ya uchaguzi wa 2015. Pili kuna nafasi nyingine ambazo tungependa ziwepo na mamlaka yake yaainishwe kikatiba. Huku tunakoenda ni kubaya kuliko tulikotoka!
"Mungu saidia"
 
Nakuambia kwa jinsi hii tume ya kukusanya maoni inavosuasua 2014 hamna kitu, chezea CCM wewe

Imebaki miezi michache kuelekea 2014... Kila siku yanayotekelezwa na Tume yanaendelea kuwa ya hovyo! Huu muundo wa uundwaji wa mabaraza ya katiba unalalamikiwa sana!.. Naiona 2014 mbaya kuliko!.

Mungu saidia.
 
Tuwatoe CCM madarakani, ndipo tutapata katiba mpya.

Utawaondoaje CCM wakati Tume ikiwatangaza ushindi inatumia katiba ya sasa ibara ya 41(7) inayosema hivi:

{Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake}
 
umesema point na sasa hapo nimekuelewa kweli best yabidi tumwombe Mungu sana kwani tunakoelekea si kuzuiri kabisa
Naona Tanzania mbaya sana hapo baadae ikiwa tahadhari haitachukuliwa. Bila msaada wa Mungu inaweza kuwa ndiyo mwisho wa neno Tanzania.
 
Dawa ni kutofanya uchaguz mpaka 2pate katiba mpya make CCM wana2mia hyo ya kinyonyaji ku2ibia!
 
Dawa ni kutofanya uchaguz mpaka 2pate katiba mpya make CCM wana2mia hyo ya kinyonyaji ku2ibia!

Ndugu yangu Bless.
Naamini wewe na watanzania wenzangu mnaona mchakato unavyozidi kwenda mrama. Wakati nikiandika Uzi huu niliyaona haya yanayotokea Leo kwa upande mwepesi kidogo. Lakini Leo naona kila kukicha; afadhali ya Jana. Kusema kuwa tusifanye uchaguzi .mpaka katiba mpya ipatikane tunatakiwa tufanye Marekebisho ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanania. Marekebisho yatakayomuongezea Rais Kikwete muda wa kutawala.

Lakini kama tunaweza kufanya marekebisho hayo, kwanini tusifanye marekebisho kwenye vipengele muhimu vinne kama (i)Madaraka ya Rais, (ii)Ukubwa wa Baraza la mawaziri, (iii)Nafasi za majimbo na Tume huru ya uchaguzi kisha tukafanya uchaguzi? Rais atakayepatikana amalizie mchakato huu wa Katiba mpya? ... Vinginevyo Mimi bado kwa mwendo huu sijaiona katiba mpya ikipatikana hivi karibuni Mwaka huu.
 

Aisee! Kwaiyo, kwa vile tupo hapa hapa ndio tusubirie katiba ijibadili wenyewe au?
CCM at work!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…