Deus F Mallya
JF-Expert Member
- Jul 28, 2011
- 705
- 441
Wana JF,
Kama mjuavyo serikali ipo mbioni kukusanya maoni ya kuandikwa kwa katiba Mpya ambapo hitaji hilo hasa litakuwa na mantiki ya kisiasa ikiwa itapatikana kabla ya mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu. Mantiki hiyo ya kisiasa inatokana na ukweli ulio wazi kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imelalamikiwa vya kutosha na wananchi wengi kwa kutokutenda haki kwenye chaguzi mbali mbali (Hasa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010).
Baadhi yetu tuliobahatika kuisoma Sheria ya Mabadiliko ya Katiba tunakubaliana bado kimsingi kuwa ilipitishwa ikiwa na mapungufu ambayo tayari yameendelea kuonekana wazi wazi kwenye mchakato wa ukusanywaji wa Maoni kwa wananchi. Mapungufu hayo (Japokuwa mengine yanapuuzwa na Tume) yanaweza kuukwamisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya kabla ya 2015 kama ambavyo hata Serikali yenyewe ilivyopendekeza.
Baadhi ya mapungufu hayo ni Suala la Muundo wa Serikali; (Uhai wa Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano).
KURA YA MAONI.
Kama sheria inavyoelekeza ni lazima 51% ya Wazanzibari waupitishe Muswada huo wa Katiba na 51% ya Watanganyika. Kwa hali ilivyo nchini kwa sasa ni vigumu SANA pande zote mbili kukubali kwa kiwango hicho hasa ikizingatiwa Kuwa tayari kuna maneno ya chini chini kuwa CCM na viongozi wake hawana mpango wa kukubali muundo wa Serikali tatu (Ikiwa utapendekezwa na Tume. Wakati huo huo msimamo wa Wazanzibari unajulikana.
Kama vijana na Watanzania wengine, kwa haki tuliyopewa kikatiba sasa nadhani ni wakati muafaka wa kujadili nini cha kufanya ikiwa mpango huo wa Serikali utakwama?.