Mkuu nimeanza kuelewa mantiki ya Uzi huu. Huku tuendako kweli ni vizuri tukasoma alama za nyakati na kuja na way forward badala ya kukaa kimya then mwisho wa siku tuweke mikono kichwani.
Kila nikiangalia jamii yangu hii ya kitanzania na namna ya mfumo wetu unavyofanya kazi, naamini kuwa ni janga zaidi kukimbilia "katiba mpya"....
Ingekuwa poa tu kama kuna vitu vidogo vidogo tungevirekebisha kwa sheria na mabadiliko ya katiba ya sasa!!
Tujikumbushe ukweli mchungu.
"Narudia kusema kwamba tusifanye mambo kwa haraka kwani hatuna tunakoenda. Tupo hapa, na tunataraji kuwa hapa kwa miaka milioni ijayo, kama si zaidi. Kwa nini tunafanya mambo kama vile tuko mapitoni (transit) tukienda mahali pengine?"
Tunayo KATIBA ya JMT nzuri tu. Hata tusipopata hii mpya tutaendelea na iliyopo.
Tatizo tulilonalo ni UONGOZI BORA na IMARA wa kuilinda na kuitetea Katiba. Hata tuandike katiba nzuri vipi kama ulinzi na utetezi wake ndio huu hakuna jipya.