Katiba Mpya itaondoa wanaume wapiga magoti na watandika kanga wa mfalme

Katiba Mpya itaondoa wanaume wapiga magoti na watandika kanga wa mfalme

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Hakuna fedhea na utumwa wa fikra kama mwaume mwenye familia kwenda kupiga magoti Kwa kiongozi WA kisiasa wakiamini NI Mungu.

Namna Watanzania wanavyomsujudia mwanadamu just Kwa Sababu ana madaraka ina kera zaidi hata ya utumwa.

Endapo katiba mpya itaondoa mamlaka makubwa ya kuteua zikabaki nafasi za kuomba Kwa kufanyiwa USAHILI kama Kenya naamini watu watajikita kufanya KAZI siyo kupiga magoti.

Sijui watoto wa wapiga magoti wanajisikiaje wakiwaona wazazi wao wamepishwa magoti.

Nimeandika Uzi huu baada ya kusikia kuna kampeni ya kumpigia mama magoti nchi nzima imezinduliwa rasmi. Tujitafakari umuhimu wa magoti kwenye kuondoa njaa na umaskini NI UPI?
 
Nchi ya Wajinga!
Ujinga umefikia kiwango Cha juu na hivyo watu wengi hasa wanasiasa wanaishi kwa kujikomba Komba, kujipendekeza na ujinga ujinga mwingi ili kupata teuzi.
Bila hivyo maisha yao hayaendi kabisa!
Tujiandaeni kwa vituko vingi huko mbeleni!
 
Back
Top Bottom