Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Nchi yetu sio ya demokrasia, hili tuliseme wazi bila kudanganya
Rais wa nchi hii anaamuliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM na wazee, amboa ndio huamua nani akatwe jina na nani apitishwe kwenda kupigiwa kura na wajumbe wa chama
Akishapitishwa na wajumbe ndio tayari ameshakuwa rais, sababu mengine yanayofuata tunajua mwisho wake
Na katiba mpya inataka nchi hii iwe ya kidemokrasia, yaani Rais awe anaamuliwa na wananchi na sio kamati ya CCM
Hili nalipinga, Rais kuamuliwa na wananchi ni hatari, kwa sababu hizi
1. Wananchi wengi wa Tanzania ni wajinga, wananchi wajinga hawajui kutofautisha kati ya kiongozi mzuri na kiongozi asiyefaa, kiongozi mbaya ambaye atakuwa na uwezo wa kuhadaa wananchi wengi basi huyo ndio atakuwa Rais, hii ni hatari sana
2. Kuleta ukabila, tumeona katika miaka 5 iliyopita ukabila umeanza kumea Tanzania, lipo kundi la watu utasikia wakijidai sisi ndio tupo wengi Tanzania, sisi tunaweza kuamua Rais awe nani n.k, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi itachochea zaidi ukabila kwa watu kupiga kura kikabila ili watoe Rais kwenye kabila lao
3. Rushwa na ufisadi kutamalaki, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi inachangia viongozi kukwapua fedha za umma kwa ajili ya kuzitumia kwenye kampeni ya urais kuhakikisha wanashinda
Mfano Katika uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana, Serikali ilikuwa ikitumia shilingi bilioni moja na nusu kila siku kwenye kampeni kuhakikisha mgombea wake Raila Odinga anashinda
Nini Cha kufanya?
Kuwaachia wazee wetu wastaafu pamoja na Chama kituamulie nani atakuwa Rais ni vizuri zaidi kuliko wananchi wasiojua lolote na wanaodanganyika kirahisi.
Nchi hii kwa sasa ipo chini ya Rais na wazee wenye busara ambao wataendelea kuhakikisha viongozi na wazee wajao wanakuwa na busara