Katiba mpya itatuletea matatizo haya 3 makubwa kwa nchi yetu

Nchi yetu sio ya demokrasia, hili tuliseme wazi bila kudanganya

Rais wa nchi hii anaamuliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM na wazee, amboa ndio huamua nani akatwe jina na nani apitishwe kwenda kupigiwa kura na wajumbe wa chama

Akishapitishwa na wajumbe ndio tayari ameshakuwa rais, sababu mengine yanayofuata tunajua mwisho wake

Na katiba mpya inataka nchi hii iwe ya kidemokrasia, yaani Rais awe anaamuliwa na wananchi na sio kamati ya CCM

Hili nalipinga, Rais kuamuliwa na wananchi ni hatari, kwa sababu hizi

1. Wananchi wengi wa Tanzania ni wajinga, wananchi wajinga hawajui kutofautisha kati ya kiongozi mzuri na kiongozi asiyefaa, kiongozi mbaya ambaye atakuwa na uwezo wa kuhadaa wananchi wengi basi huyo ndio atakuwa Rais, hii ni hatari sana

2. Kuleta ukabila, tumeona katika miaka 5 iliyopita ukabila umeanza kumea Tanzania, lipo kundi la watu utasikia wakijidai sisi ndio tupo wengi Tanzania, sisi tunaweza kuamua Rais awe nani n.k, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi itachochea zaidi ukabila kwa watu kupiga kura kikabila ili watoe Rais kwenye kabila lao

3. Rushwa na ufisadi kutamalaki, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi inachangia viongozi kukwapua fedha za umma kwa ajili ya kuzitumia kwenye kampeni ya urais kuhakikisha wanashinda

Mfano Katika uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana, Serikali ilikuwa ikitumia shilingi bilioni moja na nusu kila siku kwenye kampeni kuhakikisha mgombea wake Raila Odinga anashinda

Nini Cha kufanya?
Kuwaachia wazee wetu wastaafu pamoja na Chama kituamulie nani atakuwa Rais ni vizuri zaidi kuliko wananchi wasiojua lolote na wanaodanganyika kirahisi.

Nchi hii kwa sasa ipo chini ya Rais na wazee wenye busara ambao wataendelea kuhakikisha viongozi na wazee wajao wanakuwa na busara
Mkuu
Nimeishia kusoma hapo uliposema WATANZANIA WENGI NI WAJINGA.... Hapana mkuu wangu.

Watanzania wengi wana hofu kubwa ya kushughulikiwa kikatili na dola endapo wataonesha kutoikubali CCM wazi wazi.

Usiwaite Wajinga watu ambao wanavumilia ili kutoliingiza taifa machafukoni
 
1.Kama wananchi wengi wa Tanzania ni wajinga kwa nini usiseme Rais achaguliwe na watu wenye elimu kuanzia Diploma kwenda juu tu kwa sababu hata katika hao wajumbe wa CCM wanaompitisha wajinga na vilaza wapo wengi tu

2.Kuhusu ukabila, hilo ni jambo rahisi sana kwa sababu katiba mpya inaweza kuweka mgombea ili ashinde urais lazima ashinde kwa zaidi 51% ya kura katika nusu ya mikoa yote ya nchi.

3.Unasemaje kuhusu Rushwa na ufisadi uliotamalaki nchini kwa miaka mingi wakati hatuna Katiba mpya? Escrow, EPA, rada ya BAE, ndege ya Rais, Meremeta, 1.5T, Plea bargain n.k mbona vimekuwepo tu pasipo uwepo wa katiba mpya?
Kukazia mkuu.Haya yote yakiwa chini ya Chama na Viongozi wa ChichieM....!
 
Wapiga Kura wenyewe ndo hao wanapigwa kila siku mara kalyanda..mara Jatu...mara Mr Kuku...
 
UPUUZI MTUPU
1.
Nchi yetu sio ya demokrasia, hili tuliseme wazi bila kudanganya

Rais wa nchi hii anaamuliwa na kikao cha kamati kuu ya CCM na wazee, amboa ndio huamua nani akatwe jina na nani apitishwe kwenda kupigiwa kura na wajumbe wa chama

Akishapitishwa na wajumbe ndio tayari ameshakuwa rais, sababu mengine yanayofuata tunajua mwisho wake

Na katiba mpya inataka nchi hii iwe ya kidemokrasia, yaani Rais awe anaamuliwa na wananchi na sio kamati ya CCM

Hili nalipinga, Rais kuamuliwa na wananchi ni hatari, kwa sababu hizi

1. Wananchi wengi wa Tanzania ni wajinga, wananchi wajinga hawajui kutofautisha kati ya kiongozi mzuri na kiongozi asiyefaa, kiongozi mbaya ambaye atakuwa na uwezo wa kuhadaa wananchi wengi basi huyo ndio atakuwa Rais, hii ni hatari sana

2. Kuleta ukabila, tumeona katika miaka 5 iliyopita ukabila umeanza kumea Tanzania, lipo kundi la watu utasikia wakijidai sisi ndio tupo wengi Tanzania, sisi tunaweza kuamua Rais awe nani n.k, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi itachochea zaidi ukabila kwa watu kupiga kura kikabila ili watoe Rais kwenye kabila lao

3. Rushwa na ufisadi kutamalaki, Rais akiwa anaamuliwa na wananchi inachangia viongozi kukwapua fedha za umma kwa ajili ya kuzitumia kwenye kampeni ya urais kuhakikisha wanashinda

Mfano Katika uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana, Serikali ilikuwa ikitumia shilingi bilioni moja na nusu kila siku kwenye kampeni kuhakikisha mgombea wake Raila Odinga anashinda

Nini Cha kufanya?
Kuwaachia wazee wetu wastaafu pamoja na Chama kituamulie nani atakuwa Rais ni vizuri zaidi kuliko wananchi wasiojua lolote na wanaodanganyika kirahisi.

Nchi hii kwa sasa ipo chini ya Rais na wazee wenye busara ambao wataendelea kuhakikisha viongozi na wazee wajao wanakuwa na busara
Chama kinateua mtu wanyemuamini, kisha ndio huletwa mbele ya Wananchi kupigiwa kura,Kiongzi mbaya ataokea wapi hapa? Kuna Kamati za Maadili ya Viongozi, zinatakiwa ziwahakiki wagombea na 'Merits' zao kabla kupitishwa kugombea dhamana ya nchi, yote ni kuhakikisha hatuletewi kichaa kama yule anayefukuza watu kazi jukwaani.

2. Tanzania hilo halipo, wali haliwezi kuruhusika.

3. Rushwa itokee wapi ikiwa jukwaa la kampeni liko sawa kwa wote?
serikali ndio itowe gharama za mikutano ya wagombea bila kujali ukubwa wa chama kisha uone kama kuna atakayetowa rushwa.

Tunataka Katiba Mpya NOW not tomorow
 
Rushwa imefanywa sana na hakuna Mtz asiyefahamu Kama ripoti ya CAG ilibamiza vichwa vyetu ssa iwe je unawaita wajinga ilhali Wenye Akili Wametulia wakiangalia Rushwa zikiendelea
 
Back
Top Bottom