Mitano tena kwa Zakaria.Matukio mengi ya utekaji yangeweza kudhibitiwa kama raia wengi wengekuwa wanamiliki bunduki au bastola za kujilinda, wangeweza kupambana na watekaji ambao mara zote huwa wengi na wenye silaha, tunaweza kukumbuka mfano mfanyabiashara Zakaria wa Mara alivyopambana na watekaji kwa bastola akaponea chupuchupu kutekwa.
Ni vyema kikawepo kipengele katika katiba mpya kinachoruhusu raia kumiliki bunduki kujilinda wenyewe pale itakopibidi kufanya hivyo. Tuondoe huu urasimu wa sasa ambapo ni watu wachache tu matajiri na wanasiasa ndio wanaruhusia kujilinda wenyewe kwa kujihami tena kwa vibastola vidogo ambavyo kupata ni mchakato mrefu. Tumeshajionea jinsi hata wasio matajiri au wanasiasa watawala wanavyokabiliwa na vitisho vibaya vya usalama wao.
Sheria inaruhusu mwananchi kumiliki bastora ila sasa kuipata ndio shughuli maana mchakato ni mrefu pia gharama yake kubwa. Kitu kingine kwa mental health ya wabongo waliowengi sidhani kama ni sahihi bastora kusambazwa mtaani kwa wingi. Tukomae tu kuwaondoa wahuni then tutengeneze vyombo vya usalama vyenye welediMatukio mengi ya utekaji yangeweza kudhibitiwa kama raia wengi wengekuwa wanamiliki bunduki au bastola za kujilinda, wangeweza kupambana na watekaji ambao mara zote huwa wengi na wenye silaha, tunaweza kukumbuka mfano mfanyabiashara Zakaria wa Mara alivyopambana na watekaji kwa bastola akaponea chupuchupu kutekwa.