Katiba mpya iweke ukomo wa mtu kuwa mbunge na diwani iwe miaka kumi

Katiba mpya iweke ukomo wa mtu kuwa mbunge na diwani iwe miaka kumi

Wakili wa shetani

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2022
Posts
1,726
Reaction score
3,391
Suala la kuwakilisha wananchi halipaswi kuhodhiwa na mtu mmoja kwa muda usio na ukomo. Ni vyema katiba mpya ikaweka ukomo wa mtu kuwa mbunge. Haiwezekani mtu alikuwa mbunge au diwani toka enzi za Mkapa. Hadi leo kwa Rais wa nne bado anataka kuendelea kuwakilisha wananchi. Na bado anataka kuendelea kuwa muwakilishi wa wananchi.

Hakuna mawazo mapya, wamebaki kusema tunafanyaga hivi nk. Ni vyema nafasi ya kuwakilisha wananchi ikawa na ukomo kama ambavyo kuna ukomo wa Urais.
 
Hata kwa ajira zingine zote ilikuwa vyema zikawa na ukomo si zaidi ya vipindi 2 cha angalau miaka 4 kila kimoja.

Hii ingepungaza tatizo la ajira na kuwafanya watu wote kupanga kujiajiri na hivyo kuzalisha ajira zaidi.

Wasomi ni wengi mtaani dhana ya rare professions ni dhana uchwara.
 
Pamoja na ufisadi wote aliokuwa nao, Ngereja anataka kurudi tena bungeni 2026. Wengi wanaona atatoboa maana ni timu Msoga.

Pamoja na mbunge aliyepo sasa kukubalika na wananchi wa jimbo la Sengerema, lakini inavyoonekana hatatoboa maana alikuwa timu Magufuli.
 
Back
Top Bottom