Kaka mwisho
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 407
- 178
Tukielekea kwenye kuunda katiba mpya ya jamhuri wa muungano pamekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu aina ya muungano, kuna watu wanaotaka serikali 1, 2 au 3 na kuna vyama tayari vimetoa misimamo yao mfano mzuri ni CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi vimeungana pamoja na kutaka serikali 3.
CCM ilipotangaza kuwa msimamo wake ni serikali 2 imekuwa nongwa. Kosa la CCM ni lipi ikiwa kila vyama vimetoa misimamo yake kuhusu muundo wa muungano.
Presha ya wapinzani na watu wanaotaka serikali 3 inatoka wapi ikiwa siku ya mwisho wananchi ndio tutakaoamua kwa kura ya maoni.
Demokrasia ni mashindano ya hoja na kura, tushindane kwa hoja na siku ya mwisho wajumbe wataamua kwa kura zao pale bungeni.
Ama kweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha.