Katiba Mpya: Kuelekea Jan 25 tunayo ya kujifunza kutokea Gambia

Katiba Mpya: Kuelekea Jan 25 tunayo ya kujifunza kutokea Gambia

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Harakati za mapambano ya kujikomboa hazijawahi kuwa rahisi. Harakati hizi zinahitaji uongozi mahiri wenye kuweka maslahi ya taifa mbele dhidi ya maslahi yote binafsi.

Ujio wa Mh. Tundu Lissu Jan 25 unapaswa kuonekana nI mbaraka kamili kutokea kwa Mola na kwa hakika na aje na wenzake.

Mama Samia anapaswa kushukuru kuweza kupata msaada huu wa dhati kwenye ujio wa Lissu kuuondoa uozo uliopo. Nani anaweza kutokufurahia nchi hii ikiwa na namna iliyo bora kabisa ya uendashwaji na maisha bora kwa kila mmoja wetu?

"Anasema Samia kwenda mbali tushirikiane sote. Ya nini siasa za chuki, utengano au ubaguzi? Kwa nini kuwatenga wengine wanaofaa kwa sababu ya itikadi zao tu?"

Kumwondoa Yahya Jammeh mwiba kwa wengi Gambia hakukuwa rahisi na pasipokuwa na kuepuka yaliyokuwa malipo kamili:

IMG_20230114_113709_412.jpg

IMG_20230114_113729_171.jpg


Ebrima Solo Sandeng mpigania haki mahiri katika kifo aliwaamsha wagambia kumwambia Jammeh inatosha.

Mama Samia zingatia tunataka katiba mpya sasa ambayo ni kheri kushirikiana sote kuipata kuliko kuipata Kwa kuipambania.

Waungwana wanasema mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio na asikie.

BBC
 
Huyu jamaa aliwakamata wasiojulikana wote wa yahaya jameh akawasweka ndani sijui mama anangoja nini. Mbona wote wanajulikana kwa msaada wa wananchi dakika sifuri tu wote wanalipa matendo yao.
 
Mbona kama unaombea tundu lissu amwagwe damu kwa kisingizio cha ukombozi wa taifa. Au nimekuelewa sivyo?
 
Mbona kama unaombea tundu lissu amwagwe damu kwa kisingizio cha ukombozi wa taifa. Au nimekuelewa sivyo?
Unayasoma wapi hayo ya swala mbaya hizo mjomba?

Zingatia:

"Harakati za mapambano ya kujikomboa hazijawahi kuwa rahisi. Harakati hizi zinahitaji uongozi mahiri wenye kuweka maslahi ya taifa mbele dhidi ya maslahi yote binafsi."

Mh. Tundu Lissu ni mmoja wa viongozi hao.

Kwa hakika katiba mpya inanukia sasa kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa hakika na aje na wenzake Kwa maana saa ya ukombozi ni sasa.
 
Huyu jamaa aliwakamata wasiojulikana wote wa yahaya jameh akawasweka ndani sijui mama anangoja nini. Mbona wote wanajulikana kwa msaada wa wananchi dakika sifuri tu wote wanalipa matendo yao.

Kumbuka huyu na yule ni mtu mmoja. Hata sasa safari haitakuwa rahisi.

Mkakati thabiti wa mabadiliko kamili kufikia 2030 na kuwa na angalau bunge kamili la wananchi by 2025 uwepo bila kujali matanuru yao kama yangalipo.
 
Hahhaaaa naona huyu mtoa mada ametoa mifano ya waliomwaga damu kwenye harakati za ukombozi wa afirika
Zingatia:

"Harakati hizi zinahitaji uongozi mahiri wenye kuweka maslahi ya taifa mbele dhidi ya maslahi yote binafsi."

Tuweke rekodi sawa. Mifano hapa ni ya watu hao.
 
Back
Top Bottom