Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,315
- 5,058
Kwasasa wana jeuri sana, ila katiba mpya itapatikana ndani ya miaka minne.Kufeli kwake sio tija yeye yuko hapo kukamilisha mchezo wa kufosi hati ya dharura ya kukodisha kampuni au mitambo ya uzalishaji ili capacity charges zilipwe na sura yake isio na haya hata kidogo 😅...
Hakuna Katiba itakayoruhusu kuondoa Mawaziri kwa nguvu ya umma hakuna. Maelezo yako yanachembe chembe za udikteta, Katiba pia haitataka viongozi madikteta.Kama taifa letu litapata Katiba mpya basi tatizo la umeme hapa nchini Tanzania litakwisha kabisa. Maana kama tutakuwa na mawaziri mizigo na wazembe wenye harufu za ufisadi basi itakuwa ni suala kuwaondoa kwa nguvu ya umma tu.
Rasimu ya Warioba ilipendekeza Mawaziri wasiwe wanateuliwa kati ya wabunge, bali wawe na mikataba na wakishindwa basi wananchi wanawaondolewa kwa kutotekeleza mikataba ya ajira zao.
Makamba amefeli ndani ya siku 60 lakini CCM inamchekea tu.
Tulisahau mgao wa umeme kabisa.