Katiba Mpya: Mimi ni CHADEMA lakini kwa hili nasema NO, tena Big No

Kwa hiyo wewe unataka kusema kila alitakalo Lissu ndilo lafaa kuwa kwenye Katiba?
 
Mkuu nami nakuunga Mkono 100%
Vyama vya siasa wanaangalia tuu maslahi yao.
Na Hapa Tuweke wazi Chadema maana ndio tunaowajadili!
Serikali 2,3
Zinamanufaa gani Kwa Mwananchi wa Kawaida!
Ina Maana Mambo Mengine kama Tume huru,Mawaziri kutokuwa wabunge,kuomba baadhi ya nafasi ziwe za Ku apply na Sio Kuteuliwa,Na Masuala Mengine waliyapuuza na Kuona Lenye Umuhimu kwao Ni La Muungano tuu,Hivyo likishindikana bora Kususa Hayo Mengine sio Kipaumbele Kwao!
Namuunga Mkono RAISI SAMIA SULUHU HASSAN haina Haja ya Kuanzisha sijui bunge la Katiba,Ni Either tuendelee pale tulipoishia,Wao wanaangalia Maslahi yao sio ya Wananchi,Wakiulizwa wananchi wataje Vipaumbele vyao 5 tuu,Hutosikia Suala la Muungano hapo!likiwepo litakuwa la mwisho.
Labda Ndio linawapa Kiki!
 

Uzuri pia wa katiba hiyo hiyo na eneo hilo la ubunge, kulikuwa na kifungu cha kumuwajibisha mbunge bila kusubiri miaka mitano kuisha iwapo ataonekana hafikii matakwa ya jimbo lake.
 
Reactions: BAK
Chadema hakuna ruzuku, wanatafuta mwanya wa kupiga hela kupitia bunge la katiba. Raisi Samia achana nao hawa wachumia tumbo wa kisiasa.

Hawana ruzuku ama wamegomea ruzuku haramu?
 
Naitaka katiba mpya . lakini hapa mkuu unahoja kubwa. Lile liumoja lao ukawa lilisababisha mkwamo wa katiba. Cuf walikuwa lazima wasikilizwe na ukawa wenzao kuhusu mamlaka ya Zanzibar. Ndio maana hoja ya serikaki tatu isiyo na msingi wowote ikavuruga mchakato
 
Nimekuona hamnazo uliposema swala la Serikali 2/3 lilikuwa halina maana.
Hivi unajua muundo wote wa kiutawala utategemeana ni aina gani ya Serikali inayohitajika?
Kwa ushauri rudia kusoma rasimu ya Katiba ya Warioba,kisha chukua ile nakala ya Katiba pendekezwa ndio uje na hitimisho.
 
Sasa hoja ya Serikali Tatu kama ilikuwa haina msingi kwa maelezo yako inakuwaje tena iharibu mchakato wa kupata katiba nzima?.
Usilolijua ni kuwa ufafanuzi pale kwenye utangulizi kwamba Tanzania ni Nchi either ni Jamhuri ya Muungano inayohusisha Nchi ngapi? Ndio Jambo LA msingi kuliko mengine yote.
 
Reactions: BAK
😂😂😂😂😂mkuu acha uongo, hata mtoto mdogo anajua KATIBA mpya ni muhimu. Mkuu hebu jaribu kuvuta picha na utulize akili yako, utagundua KATIBA ni muhimu.
 
Reactions: BAK
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 

Mkuu yawezekana wewe ndio mtoto.sisi wengine tunajua tangu yanaundwa mabaraza ya kata.then soma vizuri andiko langu
 
Huwezi kuwa chadema wewe mpumbavu na dhuluma ya uchaguzi wa Mwaka Jana ukiongea mambo ya ki mat*ko hapa wakati watu wameumia! Sitaki kukutukana!

Kaa huko CCM na akili za kipumbabu!
 
Reactions: BAK
wewe bora ungebaki msomaji milele, maana una uwezo mdogo sana wa kuchambua mambo.BAKI KUA MSOMAJI TU MKUU UTAJIFUNZA MENGI.
 
Wewe huna sifa ya kuwa mwana Chadema sema wewe ni magamba sugu wala hatutojali
 
Kwan nn faida na harasa ya serikali 3 na zipi faida na harasa za serikali 2? Wenda kila upande ulikuwa unajaribu kujitengenezea mazingira ya upataji kiurahis ndio maana hawakuona vitu vingne zaid ya hilo.
Je, huoni kuwa ni Zanzibar ni nchi , ina katiba, ina bunge lake, ina rais wake, ina wimbl waje wa taifa? xHii Zanzibar iliungana na nani mpaka tukapata Tanzania? Hiyo nchi iko wapi?
Kama Zanzibar ni nchi mbona haichangii cho chote kwenye muungano?
Wabunge wa Zanzibar hushiriki kwenye vikao vya bunge la Tanganyika ni serikaliinayolipa kila kitu chao, posho, mpaka pesa za majimbo wkt skule kuna serikali inayojitegemea.

Sasa hivi tuna rais anatawala Tanganyika kwa kuwa Zanzibar haichangii kwenye muungano.

Wengine wanasema Waziri mkuu anatawala Tabganyika sio kweli.bAnayetawala ni yule anayemteua ndiye mtawala. Rais aliyepo Mzanzibari anasimamia serikali ya Tanaganyika lakini sio ya Zanzibar. Kwa kuwa Zanzibar ina rais wake na serikali yake. Anayetawala Tanganyika mbona siye aliyechaguliwa na Watanganyika kama Zanzibar wanavyoteua wao. Kwanini tunyimwe haki hii yetu ya kikatiba ndio maana tunataka serikali yaTanganyika kwenye muungano usoeleweka
 
Wewe siyo Chadema bali Kadema!
 
Hawana ruzuku ama wamegomea ruzuku haramu?
Mwaka 2010 chadema walisema uchaguzi haukuwa huru na wa haki, lakini kwa vile Mbowe na genge lake walishinda katika uchaguzi ule na kuwa na uhakika wa kuingiza ruzuku ndan ya chama kwa kila kichwa kimoja, basi waliingia bungeni na wakawa wanashiriki vikao vya bunge. Mwaka 2015 pia chadema wakaja na kilio kile kile cha kususia matokea ya uchaguzi kwa madai kwamba uchaguzi ule haukuwa huru na wa haki, lakini kwa vile Mbowe na genge lake walishinda ubunge tena katika majimbo yao na kupata uhakika wa ruzuku kupitia vichwa vyao basi walikubali kuingia bungeni na kushiriki vikao vya bunge kama kawa. Mwaka 2020 baada ya mwenyekiti na genge lake kuangukia pua ndo wanakuja na porojo ya kususia bunge kwa madai yale yale ambayo wao yaliwaingiza bungeni kwa zaidi ya miaka 10. Mbowe na genge lake wanafikiria kuwa kila mtanzania ni poyoyo kam ilivyo misukule yake. Mwambie akumbuke haya maneno ya kingereza "You can fool some people sometimes, but you can't fool all the people all the time" - Bob Marley. Mwambieni atafute vyanzo vingine vya kupata pesa za kuwalipa kina Mmawia, hizi propaganda zake za kutaka kupiga hela kupitia mchakato wa katiba wenye akili tushaugundua na hautamsaidia.
 
mzee huna lolote Zaidi ya kusumbuliwa na bangi ebu tuletee kipengele kinachohusu tume huru ya uchaguzi kwenye rasimu ya warioba na ulete kipengele kwenye rasimu ya CCM halafu ndio utuletee bangi zako sawa kijana kwa ushauri tu wa bure acha kuvuta bangi bora ubugie cocaine itakusaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…