DIZZO MTAWALA
JF-Expert Member
- Aug 22, 2015
- 240
- 767
Nchi yetu hii ilifikia hatua nzuri sana ya watu kuwa huru kutoa mawazo yao,bahati mbaya baada ya Jakaya Kikwete kutoka madarakani tulianza kutunga sheria kali dhidi ya wenye mawazo kinzani.
Wenye mawazo kinzaji waliitwa kila aina ya majina ya kebehi, wenye mawazo kinzani waliitwa mawakala wa mabeberu, vyombo vya habari vyenye mawazo kinzani vikafungiwa.
Wabunge wenye mawazo kinzani wakaapiwa kutorudi bungeni, 2020 tukashuhudia Uchaguzi wa ajabu uliojaa ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu, tukaambiwa wakosoaji wote hawatakiwi bungeni. Ulikuwa ni Uchaguzi wa kufukuza wenye mawazo kinzani bungeni na mabaraza ya madiwani.
Tukiamua kuzuia mpaka mijadala ya wazi ya bunge,,wengine tukashauri kuwa siyo njia sahihi hiyo,tukaaambiwa, acheni tujenge nchi.
Bunge likakubali kuingiza mpaka wasio na sifa za ubunge,wenye kuona mbali wakasema tusifike huko.
Na sasa waliokuwa vinara wa kupinga mawazo kinzani, wanalia uhuru wao wa kutoa mawazo kunywa.Nenda kasome kisa cha Tawio Adamafio
Credit DOTTO BULENDU