Kwa upande wa zanzibar saivi tumebakia kujiandaa na kuilinda katiba ya zanzibar tu hatuwezi kushindana na wanaotumia nguvu sisi ni kidogo sana,elimu ya makongamano ni kukumbushana tu kwa zanzibar kwa sababu siasa inaeleweka vizuri sana hapa na mbinu za viongozi wa tz(tanganyika) zinaeleweka vyakutosha hapa.
sote tumejionea jinsi ya bunge lilivyokwenda ni aibu tupu,na kura zilivyopigwa,kwa hio yale yalikuwa maamuzi yao na sio maamuzi ya kisheria kama ilivyotarajiwa kuwa.
sasa nijibu baadhi ya maswali ya mtoa mada
1. je Walipata walichokuwa wanataka?
katika mchakato wa katiba kwa zanzibar tulitaka mkataba wengi wetu na katika mtazamo mzima wa saisa za tanzania zanzibar tunataka kuwa na hadhi na heshima kama nchi mshirika wa muungano na pia uwezo wa kufanya maamuzi yanayohusu muungano yaani kuwa na say katika muungano kwa kiwango cha sawa kwa sawa na mshirika mwenzetu tanganyika bila ya kuangalia ukubwa au wingi wa watu hizi ni nchi na sio muungano wa makundi ya watu.
jawabu hapa ni bado ubeberu wa tanzania unaendelea,na hakuna kilichopatikana kwa zanzibar ila ni tricks na dharau tu.
2. Warioba anawafanyia kazi ambayo walitakiwa waifanye?
mimi bin nafsi yangu kama mzanzibari namshukuru sana nd.warioba na watanganyika wote ambao wana mtazamo wa haki na sheria,na anavyofanya mzee warioba ni wajibu wa kila mmoja kuelimisha na kuamsha watu ili kukaa katika mstari wa haki na sheria,wale ambao wanamuona warioba anawafanyia kazi wazanzibari wafikiri upya ya kuwa nchi hii inaelekea kwenye uongozi wa kidictator na itaathiri kila mtu,serikali ikianza kupinda sheria hadharani bila ya kujali ni sawa na kula nyama ya mtu na ni hatari sana,mwisho wake ni udictator tu na haya yanaanza na rushwa ambayo imepindikia. na itaathiri kila mmoja wetu regardless of political affiliation
jawabu ni nd.warioba anatimiza wajibu wake
3. Ni delay tactic?
jawabu ya hili hakuna delay tactic,wazanzibari tumeshtushwa sana na matukio ya bunge la katiba,kwa sababu mambo yaliyofanywa pale zamani yalikua yakifanywa kwa siri na ndani ndani lakini kuona sasa kima kakosa miti anarukia kila mtu inashtua kwa kweli
tunaangalia mustakbali wa katiba ya zanzibar tu ndio ngao kwa sasa
4. Baada ya kutimuliwa Mwanasheria Mkuu wao waliogopa?
zanzibar hakuna khofu ya aina hii kabla ya kufkuzwa mwanasheria alifukuzwa mansour na kabla ya mansour wako walitishwa na kufkuwa pia wengi tu na wengi wamepoteza maisha zanzibar yote hayo na mengine hayatoondoa uzanzibar maisha,ni kupoteza wakati na mapesa tu,
wakati tanzania in 2014 bado inajikita kuandaa mbinu za kisiasa kuendelea kuidhibiti zanzibar na/ili kuwafanya raia wake kama mazombi wasiweze kufkiri kenya na rwanda zinaondoka kimaendeleo,juzi nimeona plan 2040 ya rwanda its impresive,hapa bado tunaruhusu siasa za kikoloni.
jawabu hapa ni kuwa kwa zanzibar haitatokea siku ya kuacha kutetea haki iwapo haki na sheria hazitatawala.
asanteni na wale wanaofikiri tafauti msinielewe vibaya i wish things could have been different in different circumstances but its seems as thou politics is our biggest challenge so far,its lack of imagination that keeps us back in old colonial days and here we will stay unless we find the right way