Katiba Mpya ndiyo mkombozi wa Watanzania

gwamaka aswile

Senior Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
186
Reaction score
106
Licha ya baadhi ya watu hususan kutoka kambi ya upinzani kudai kwamba Katiba Inayopendekezwa imelenga kukinufaisha Chama Cha Mapinduzi, napingana nao pia naomba Watanzania waisome kwa umakini watabaini ukweli na kuachana na propoganda zinazotolewa na watu hao. Wakiisoma naamini hawatasita kuipigia kura ya ndiyo muda utakapofika kwa ndiyo mkombozi wao.
 
Viroba vya mchana na mahindi ya kuchoma noma sana

Umesamehewa mkuu maana huyo aliyekutuma ni mdogo kama wewe ndo maana amekupa apple utafune ili akili yako itoe vumbi mchana!pole sana, kama huijui Katiba inayopendekezwa pata copy yako usome uache kudundadunda!
 
Viroba vya mchana na mahindi ya kuchoma noma sana

Sipendi tabia yako ya kupenda unywaji wako wa hivyo vitu. Sipendi mfululizo. Hii ni tabia yako umeamua kutujulisha tu! Anyway, Unywaji wa viroba ni hatari kwa afya yako, badilika.
 
Licha ya baadhi ya watu hususan kutoka kambi ya upinzani kudai kwamba Katiba Inayopendekezwa imelenga kukinufaisha Chama Cha Mapinduzi, napingana nao pia naomba Watanzania waisome kwa umakini watabaini ukweli na kuachana na propoganda zinazotolewa na watu hao. Wakiisoma naamini hawatasita kuipigia kura ya ndiyo muda utakapofika kwa ndiyo mkombozi wao.

Hivi wewe umetumwa na nani!? Ni kweli kuwa tunahitaji Katiba Mpya itutoe hapa tulipokwama lakini siyo Katiba Pendekezwa! Hiyo Katiba yenu Pendekezwa na CCM imefuta haki za binadamu zisiingie kwenye katiba kwa madai kuwa zitatungiwa sheria, hivi ni mtawala gani ambaye anapenda kutoa haki za binadamu na kubanwa na sheria!
 
Mkuu hata usipate taabu hizo hasira zako zihifadhi utaziweka kwenye kura yako aisee othewise utakua kichaa katiba Inayopendekezwa itapita aisee!
 
Hivi wewe umetumwa na nani!? Ni kweli kuwa tunahitaji Katiba Mpya itutoe hapa tulipokwama lakini siyo Katiba Pendekezwa! Hiyo Katiba yenu Pendekezwa na CCM imefuta haki za binadamu zisiingie kwenye katiba kwa madai kuwa zitatungiwa sheria, hivi ni mtawala gani ambaye anapenda kutoa haki za binadamu na kubanwa na sheria!
Wewe ndo umetumwa mwehu weweee unaongea tu, weka ushahidi ni wapi katiba hiyo imefuta haki za binadamu. Acha kudanganya watu humu ndani utaolewa
 
Licha ya baadhi ya watu hususan kutoka kambi ya upinzani kudai kwamba Katiba Inayopendekezwa imelenga kukinufaisha Chama Cha Mapinduzi, napingana nao pia naomba Watanzania waisome kwa umakini watabaini ukweli na kuachana na propoganda zinazotolewa na watu hao. Wakiisoma naamini hawatasita kuipigia kura ya ndiyo muda utakapofika kwa ndiyo mkombozi wao.

Watanzania afadhali wachomwe moto Mungu aumbe upya!
 
licha ya baadhi ya watu hususan kutoka kambi ya upinzani kudai kwamba katiba inayopendekezwa imelenga kukinufaisha chama cha mapinduzi, napingana nao pia naomba watanzania waisome kwa umakini watabaini ukweli na kuachana na propoganda zinazotolewa na watu hao. Wakiisoma naamini hawatasita kuipigia kura ya ndiyo muda utakapofika kwa ndiyo mkombozi wao.
fulsa sawa gender issue 50/50
walemavu
albnisms
nk
mie nafikri hivi ni vidogo hata nchi zilizo endelea sidhani wamefanya hivi
maadili,ya viongozi.mikataba c siri kwani ni vyetu
 
Unataka kujua faida utakayopata au kujua mkataba?
 
Licha ya baadhi ya watu hususan kutoka kambi ya upinzani kudai kwamba Katiba Inayopendekezwa imelenga kukinufaisha Chama Cha Mapinduzi, napingana nao pia naomba Watanzania waisome kwa umakini watabaini ukweli na kuachana na propoganda zinazotolewa na watu hao. Wakiisoma naamini hawatasita kuipigia kura ya ndiyo muda utakapofika kwa ndiyo mkombozi wao.

Weka na rejea mbili tatu
 
Sheria mama yani katiba katika taifa lolote ndio msingi wa maendeleo,tuwapuuze wale wote wanaopotosha jamii kuhusu katiba inayopendekezwa
 
Watanzania tuchukue muda wetu kuisoma katiba inayopendekezwa ili tusipotoshwe,kwa kuwa ni haki yetu kuisoma na hatimaye kufanya maamuzi
 
Uhondo wa ngoma ni kuingia na kucheza. Uzuri wa Katiba Inayopendekezwa huwezi kuujua kwa kuambiwa na watu tu. Chukua fursa ya kuisoma sasa ili uielewe vizuri. Acha kuambiwa na watu, muda ni sasa jielimishe kwa kusoma na siyo kuambiwa au kusomewa. Wapo wapotoshaji akisoma, anatafsiri kulingana na matakwa yake au ya mtu fulani matokeo yake anaudanganya Umma. Chonde chonde soma na ujionee mwenyewe yaliyomo kwenye Katiba Inayopendekezwa.
 
Katiba inayopendekezwa ndio msingi wa maendeleo endelevu katika taifa letu,tuiunge mkono kwa kuisoma nA kuielewa ili hatimaye tufanye uamuzi sahihi
 
Back
Top Bottom