Katiba Mpya ni kete kwenye ilani ya CHADEMA 2025

Katiba Mpya ni kete kwenye ilani ya CHADEMA 2025

Kwa kweli ni ngoma nzito. Lakini sio sababu ya kutopiga na kupaza sauti mpaka wakubali. Tukiwa wamoja inawezekana. Ile hatua iliyofika ni 50% Twaweza kwenda tena 75%
Nasema kuwa mchakato wenyewe ni wa hovyo hivyo sheria ya uundwaji wa katiba mpya lazima kwanza ibadilishwe kwanza la sivyo tutapata kichekesho cha katiba si katiba inayokidhi kiu ya wananchi bwashee
 
KATIBA MPYA NI KETE KWENYE ILANI YA CHADEMA 2025.

Leo 09:15hrs 07/07/2021

Je CCM itakuja na agenda hii kwenye ilani ya kutafutia kura? Je tumeutafakari uzuri na ubaya wa katibs tuliyonayo!? Je tumeshatafakari uzuri na ubaya wa katiba Mpya tunayoitaka!?

Katiba tuliyonayo haikutuvusha wakati wa msiba bali hekima za Watanzania,Busara za Watanzania,na Uvumilivu wa Watanzania,tusiwekeze kwenye hekima,Busara na Uvumilivu tuwekeze kwenye katiba Mpya itayotoa ridhaa ya Watanzania wote baada msiba maana kesho na kesho kutwa watakuja watu wasio na hekima, Busara wala Uvumilivu.

Katiba ya sasa haifikii ukuu wa taasisi ya Urais,Ukuu wa katiba unaishia pale Rais anaposhika madaraka,Sasa hili ni tatizo kubwa kwa maana itahitaji utashi wa Rais kuendesha nchi,tuwekeze kwenye katiba Mpya kwenye madhara ya uvunjaji wa katiba, Rais aweze kuwaji bishwa na taasisi nyingine.

Je ipitishwe katiba pendekezwa ya Warioba au tuanzie alipoishia Jaji Warioba au tuanzie kwenye sheria inayoruhusu kuandika katiba mpya,ni kweli katiba Mpya haipo kwenye ilani ya CCM lakini utashi wa Mh Rais unaweza kuileta katiba Mpya,mambo muhimu yote yatafanywa tukiwa na katiba inayotia mkazo maendeleo ya nchi,

Nimalizie kwa kusema Ilani ni nyenzo ya kutafutia kura Uchaguzi ujao.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
kete gani wakati hawashiriki uchaguzi
 
Nasema kuwa mchakato wenyewe ni wa hovyo hivyo sheria ya uundwaji wa katiba mpya lazima kwanza ibadilishwe kwanza la sivyo tutapata kichekesho cha katiba si katiba inayokidhi kiu ya wananchi bwashee
Yote yanawezekana kama tuna nia na taifa letu. Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Tukipaza sauti inawezekana
 
Back
Top Bottom