Ndugu watazania na watanganyika suala la katiba mpya ni la lazima na wala sio ombi, kwani tayari Zanzibar wameshafanya mabadiliko. na hayo yameifanya kuikiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inasema Tanzania ni nchi moja yenye pande mbili, hivyo kuifanya zanzibar ni nchi ni kukiuka katiba ya Tanzinia, Hivyo mabadiliko ni lazima yafanyike kwa kuanzia na hilo pamoja na mengine mengi. Mara nyingi najiuliza ilikofia Tanganyika, kwani mbona siku ya uhuru wake tunasherehekea kwa picha ya Uhuru wa Tanzania wakati hakuna siku Tanzania ilipopata uhuru wake! Bendera inapandishwa ya Tanzania, Mgeni rasmi ni rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania! Ni lini nchi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipata uhuru wake na kutoka kwa nani?