Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

HKigwangalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2008
Posts
722
Reaction score
971
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.
 
Mimi nataka mshahara wa rais na viongozi wengine ambao mishahara yao inatoka kwa pesa za walipa kodi iwekwe wazi ili Mtanzania yeyote yule akitaka kujua ajue wapi pa kwenda kuzipata hizo taarifa.

Walipa kodi wana haki ya kujua pesa zao zinatumikaje.
 
Ni jambo zuri Mh kigwangwala kupeana ushauri nikupongeze kwa hili.
 
Last edited by a moderator:
Wabunge mpunguziwe mshahara, na posho msipewe kabisa maana mnapewa pesa nyingi halaf msitembelee mashangingi mpewe gari za kawaida tu
Maana tunawachagua mkatuwakilishe mkasemee matatizo yetu lakini kwaajili ya posho na mishahara mikubwa mnasinzia tu

Halaf CCM imetawala muda mrefu ipumzike na yenyewe kama kweli kuna democracy nchini mwetu vyama vingine vitawale
 
Tatizo wengi wetu humu ndani JF hatukuamini kwa kuwa umekuwa MNAFIKI na MSALITI sana.
Hata maoni ya madaktari wakati wa migomo yao 2012 ulitumwa na Bunge kwenda kuyakusanya lakini ulichokwenda Kukiwalisha bungeni ni mashudu yako matupu na sio uhalisia.

Dr.Kigwangwalla wewe bado sana, unajaribu kufanya mambo kama Mwigulu Nchemba ili kudraw attention za watu tu lakini huna dhamira yoyote njema.

Kwa kuanzia tu, embu tupe msimamo wako ni upi kwenye bunge la Katiba na nini utafanya katika haya:
1/Mfumo wa serikali (Utafuata sera ya CCM serikali mbili au Msimamo wa Warioba na watanzania wengi(61%) serikali tatu au vinginevyo).

2/Posho ya shilingi 700000/= kwa siku kwa kila mjumbe wa bunge la katiba kwa siku 70.
 
mtakuwa mnalipwa sh. ngapi kwa siku?
hivi ni kweli tunaihitaji katiba kwa gharama kubwa namna hii, msimamo wa chama chako ni serikali mbili, ndio msimamo utakaoingia nao bungeni au wewe hushurutishwi na chama chako?

N.B tunaogopa kutupa almasi mdomoni pa nguruwe.
 
Washauri wajumbe wezako wa Ccm kuwa serikali mbili hazifai waunge mkono mapendekezo ya jaji Warioba serikali tatu kwa mstakabali wa taifa ili na kama jana wamemsikia atakuwa amewafungua zaidi na zaidi.
 
Mimi nipo kwenye masuala ya muungano.

Nijuavyo mimi Wazanzibar wanataka mamlaka kamili yaani sovereignty. Kwa maana ya mkataba wa Montevideo ni kwamba pamoja na mambo mengine sovereignty inaifanya nchi iweze kuwa na mahusiano na nchi nyingine ama na vyombo vya kimataifa.

Niaminivyo, Wazanzibar wanataka wawe huru ili hata wawezi kujiunga na OIC. Lakini kwa muundo huu uliopendekezwa na Tume ni kwamba Wazanzibar hawawezi kupata hiyo fursa, sovereignty state itakuwa ni Jamhuri ya Muungano na si Tanganyika wala Zanzibar.

Wazanzibar wakija kujua kwamba hawawezi kujiunga na FIFA ama OIC kwa kuwa si sovereign state basi wataanza tena chokochoko na mambo kibao ya kero za muungano; uhai wa muungano utakuwa shakani tena.

Maoni yangu ni kwamba kama tunataka Muungano basi tuwe na muungani wa kweli kwa maana ya serikali moja na si mbili wala tatu. Mbili hakuna muungano ni kero tuuuu; na hizo tatu ndio vurugu kabisa.

Nawasilisha
 
Kwa nini mnakubali kulipwa laki saba kwa siku?hamuoni kuwa hamuwatendei haki wananchi wengine...
Nlitegemea ulivyoingia bungeni ungepinga malipo makubwa namna hiyo wakati watu wengine wenye professional zao hata hiyo laki saba hawazifikishi kwa mwezi..
Nikisema nyie wanasiasa ni wanafiki litakuwa ni kosa?
Nkirudi kwny katiba mpya wengi wetu tunapenda serikali tatu.
 
Mimi nataka Kila Mfanyakazi alipe Kodi kupitia kwenye Account yake na si kukatwa Makampuni alafu haipelekwi TRA, au haijulikani inakoenda. Kama NSSF na PPF mtu ukiacha kazi ndiyo unaanza kuhangaikia mafao na pengine unakuta yalikuwa hayapelekwi.
 
Sina imani sana na nyie wabunge wa CCM.

Anyway,back to the topic,kinga ya raisi iondolewe,madaraka ya raisi yapunguzwe mfano kuteua majaji,kuteua msajili wa vyama vya siasa,DPP,mkurugenzi wa TAKUKURU n.k

Raisi asiwe na mamlaka ya kulivunja bunge na waziri mkuu akijiuzulu au kufukuzwa baraza zima la mawaziri lisivunjwe .
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.
kuhusu muungano,nitafurahi kama utasimamia uwepo wa serikali moja kama kweli tunadhamini undugu wetu wazanzibar na watanganyika kama hilo la serikali moja linashindikana hapo lazima ieleweke kwamba kuna upande mmoja hautaki muungano hivyo kuwa na serikali tatu hakutakuwa na maana yoyote bora kila nchi iwe kivyake tubaki majirani wema kama tulivyo na nchi nyingine
 
nakisikia kwa siku mtalipwa 700,000/- hivi kweli wewe binafsi unaona hii ni fair hasa ukilingalisha hali ya maisha wa watu wa Tanganyika?

TANU ya mwalimu ilikata MIRIJA na kuweka usawa kwa wote, ila CCM yenu sasa badala ya mirija sasa imeweka MABOMBA kabisa ili inyonye vizuri - posho ya laki saba kwa siku - jamani hebu mumuogope na mwenyezi mungu wakati mwingine!!

Hilo kalikemee kama unaweza!! na uikatae hiyo POSHO.
 
Mfike mahali mkubali ukweli kuwa bunge mnafanya shughuli za Tanganyika na si za Tanzania,na kuwa Zanzibar
ni nchi kamili yenye dola,so acheni unafiki mkubaliane na hali halisi kuwa tunahitaji serikali tatu'
 
Kubwa hapa ni serekal ya Tanganyika irudi ,pili Rais apunguziwe madaraka ,tatu kuwe na uwaz wa nn rais analipwa hapo magogon,nne tumehuru ya uchaguz pamoja na kutoa minyororo iliyofungwa kwenye mahaka zetu,tano malipo ya mishahara yaendane na kiwango cha elimu na wala si taaluma mfano mwl wa degree alipwe sawa na afisa organ mwenye degree.
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.
Wakatabahu,HK.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...enye-kikao-hali-yachafuka-18.html#post8678930

Heri ya wewe uliyesema utasikiliza, wenzako wamekimbia jamvi kwa kuogopa hata kusikiliza.
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.

Kigwangala,
Nacho kiona katika suala la Muungano, ni kuweka wazi mambo ya asili ya huo Muungano yaliyo asisiwa na waliotakana kuungana, kishayajadiliwe namna yalivyoendelezwa na baada ya hapo sasa ndo yatizamwe yale yaloongezwa na sasa yakazusha kitu kiitwacho"KERO ZA MUUGANO", na kwa kuanzia hapo ndo tutakuwa tumepata namna ya kuiendea hio iitwayo"MUUNDO WA MUUNGANO",

Nakuusieni nanyi Wabunge msikae pale ki-siasa wala ki-vyama ili kutokujidhulumu"NAFSI", tambueni mtalipwa na alokuumbeni juu ya uadilifu wenyu, maana hamkijiumba bali mmeumbwa.

Sasa msitake kuzifurahisha nafsi zenyu ilhaali hamjui safari zenyu kwa muumba ni lini na muda gani na wapi..!!

Kama mtendavyo na ndivyo mtalipwa.

Ahsanta .
 
Back
Top Bottom