Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

Naunga Mkono Hoja za
Mjumbe isipokua hoja no. 5 Inahitaji Marekebisho.Hasa kufuta Wizara ya
Michezo na Utamaduni!

bora umenisaidia. jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza. Watu wengi hawafahamu umuhimu wa utamaduni ktk maendeleo ya nchi.
I dought hata ktk hao wajumbe wa bunge hili kama kuna mwakilishi wa utamaduni.. hii nchi itauzwa lolz.
 
Mh. Swala la serikali tatu. Najua wewe kwa msimamo wa chama chako, serikali tatu ndio chaguo.
Ila endapo mkizidiwa nguvu na wale 'wa tatu' basi kuwe na rais mmoja tu wa tanzania. Tanganyika na zanzibar kuwe na mawaziri wakuu kama viongozi wakuu. Mimi ishu ya kuwa na marais wa tatu, ni ukakasi ambao utakuja kuwa na mkanganyiko!
Hilo tu Mh!
 
Yap,kama zanzibar ina rais wake kwa nn tanzanyika isiwe na rais,kama s hvyo bas awepo rais mmoja kwa tanganyika na zanzibar
 

serikali inapotoa tenda kwa ujenzi wa barabara iseme ni tsh zinatumika serikali iwe wazi kwa kila kitu kwa nn mnafichaficha?
 

Kwaiyo unataka kumlazimisha sasa aseme unachotaka wewe??

Kakwambia utoe maoni wewe unaanza kumpa makondisheni ....dah .....
 
Kuitishwe kura ya maoni nchi nzima ya kuukubali au kuukataa muungano.Binafsi siutaki huu muungano.
 

Ina maana hujapokea main I ya wanajimbo lako? maana ccm hawataki maoni ya wananchi ww upo neutral au wapi maana vinginevyo hayo maoni yataishia hapahapa
 

Salaam Aleikhum Daktari'
Wazo zuri hilo. tafadhali hakikisheni Tanganyika inatoka nyuma ya pazia; watanzania tunaogopa nini kudai nchi yetu? Viongozi wetu mnawadekeza wazanzibari kwa nini! hivi kweli ni lazima tuwalambe miguu wazanzibari ili kuendelea kubaki ndani ya muungano; Hivi ni kweli nje ya Muungano huu cosmetic watanganyika hatuwezi kuishi?

Najua rasimu ya katiba ina mambo mengi muhimu ya kujadili; but when prioritised; no doubt the form of the union comes on top.
Nitafuatilia mijadala yako kwa karibu sana.
 

Tuwekee email address yako hapa na tuko tayari kukuleta maoni, ushauri na michango yetu kuhusu hoja mbali mbali za rasimu ya Katiba kwa Bunge maalum la Katiba. Tutashukuru kama maoni yetu utayafikisha huko. Mengi si vizuri na si rahisi kuyaandika humu, kwenye email ingekuwa ndiyo bora zaidi na ni nyepesi zaidi. Kwenye simu itakuwa usumbufu kwako
Hivyo tupe email address yako.
 

Hilo ndiyo mchango wangu kwa Tume. Tatizo Tume waliwekewa uzio wa mambo ambayo hawawezi kuyagusa kwa mujibu wa sheria ambayo iliweka hadidu za rejea...kuwa ni lazima Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwepo...sasa hili lingewezekana wapi? Huwezi kuwalazimisha Zanzibar wasiwe na Rais...wakati wao wanataka wawe na serikali yao, yenye mamlaka kamili ya kutekeleza mambo yao yasiyo ya muungano. Kwa lugha nyingine kulilazimisha hilo ingekuwa hatua kuelekea kuuvunja Muungano, jambo ambalo pia lilipewa kinga na sheria...

Regards,
HK.
 
Tumia Email hii kufikisha ujumbe kwangu: hkigwangalla@gmail.com
 
Shukrani
Yafuatayo n mapendekezo yangu

1. Serikali moja ya Muungano, ikishindikana ni tatu.Sio mbili za sasa.
2. Watanganyika waruhusiwe kumiliki Ardhi Zanzibar kama Wazinzibari wanavyoruhusiwa kumiliki Ardhi Bara. Kama wataendelea kukataa kama katiba yao inavyosema sasa, basi na wao wasiruhusiwe kumiliki Ardhi bara.
 
Mimi nataka mshahara wa rais na viongozi wengine ambao mishahara yao inatoka kwa pesa za walipa kodi iwekwe wazi ili Mtanzania yeyote yule akitaka kujua ajue wapi pa kwenda kuzipata hizo taarifa.

Walipa kodi wana haki ya kujua pesa zao zinatumikaje.
mkuu hebu tuwaulize tena
 
Mawaziri waajiriwe,lakini waingie bungeni kujibu maswali tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…