Katiba Mpya: Rais Samia Suluhu achague kutenda haki kwa kuwatumikia Watanzania masikini au kuwatumikia CCM

Katiba Mpya: Rais Samia Suluhu achague kutenda haki kwa kuwatumikia Watanzania masikini au kuwatumikia CCM

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
2,946
Reaction score
2,932
Waraka huu wa kukushauri tu, ninavyowafahamu waislam ni watu wanaohubiri haki japokuwa swala ndiyo yenye nguvu kubwa ktk Uislam.

Yalipo kwenye utangulizi wa waraka wangu , moja linabeba pepo na jingine jehanam.

Kuwatumikia CCM wachache kwa maslahi yao ni sawa na mwislamu aliyesoma elimu dunia ambayo mwisho wa siku kifo kikimkuta anaenda kunako moto wa milele.

Kwasababu CCM haijawahi watendea haki watanzania hata walio CCM wenzao toka upatikane uhuru.

Wachache wanaonufaika na CCM kuwepo madarakani ndiyo wanaopinga mchakato wa Katiba Mpya maana maslahi yao yataondolewa.

Rais unajua kuwa kurudisha mchakato wa Katiba ni kuwakosea CCM, lakini kwa upande wa pili unajua kwa kutofanya hivyo unawaumiza wananchi waliowengi.

ATHARI

Swala zako hazitaswihi
Funga zako hazitaswihi
Utakuwa Mwislam wa dini na siyo haki

NAKUSHAURI RUDISHA MCHAKATO WA KATIBA BILA KUJALI LAWAMA ZA MACCM,LINDA IMANI YAKO.
HARI KULAUMIWA NA WANAADAM KULIKO KULAUMIWA NA MUNGU
 
Katiba Mpya itamwokoa hata yeye dhdi ya maharamia ndani ya chama na serikali.
 
Bahati mbaya ameshachagua kuwatumikia CCM. Ushahidi uko wazi kabisa.
 
Kwa mungu hakuna katiba, kwa mungu hakuna tume huru, kwa mungu hakuna siasa, kwa mungu ni matendo yako ndio utafika panapo staili kama pepo au moto. Kwa hiyo tusidanganyane na siasa zako za maji taka au siasa uchwara za Bongo.
 
Back
Top Bottom