Katiba Mpya si kwa Utashi wa Zitto, Mukandara wala Samia

Katiba Mpya si kwa Utashi wa Zitto, Mukandara wala Samia

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Nchi si shamba la bibi. Katika nchi, yote ni kwa mujibu wa katiba.

Kwa mujibu wa katiba, sote tuna haki sawa ambapo uamuzi ni kwa kura. Kura moja kwa mtu.

Si Samia, Zitto, Mukandara, Dr. Hosea au awaye yote kwamba wanaweza kujimilikisha mustakabala wa msingi wa nchi hii.

Labda kama wanataka kuleta fujo.

Inafahamika kuwa wapo watu wenye maslahi yao binafsi kwenye mahitaji haya ya msingi sana kwetu.

Uzi huu wa mwaka jana ungali unaishi:

Tutambuane, nani ni nani katika kudai Katiba mpya

Tunakoelekea mbona tusije kuja kumlaumu dobi?

Kwani la kuvunda liliwahi kuwa na ubani?
 
Samia Suluhu Hassan Rais wa jqmuhuri ya Muungano anatqkq kqtiba mpya. Kama utqkumbuka alikuwa makamu mwenyekiti kwenye lile bunge la katiba wakati wa mzee Kikwete.

Wasiotaka katiba mpya ni CCM. Ambao wanajuq wazi kabisa, kwamba siku ikipatikana katiba mpya tu ndio mwisho wao kuendelea kuitawala hii nchi.

Adui mkubwa wa watanzania kwa sasa ni CCM.
 
Itakuwa makosa kumtenganisha Samia hapa.

Samia anataka urais 2025. Anajua Kwa katiba iliyopo ataupata, ila si kwa katiba nyingine.

Ndani ya CCM wapo wanaotaka katiba mpya wengi tu, lakini si Samia Suluhu Hassan.

Tume ya Mukandara na wenziwe ni tume ya Samia kufanikisha kurejea kwake madarakani 2025.

Zingatia sababu za kigugumizi chake kuwakemea polisi pia.
 
Back
Top Bottom