Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,733
Wanabodi
Baada ya kusikiliza kwa makini maoni ya wanasiasa wa vyama vyote na pande zote mbili za Muungano, nashawishika kuamini kuwa kinachogomba si idadi ya serikali katika Muungano huu. Toka mapema katika hadidu za rejea kwa tume ya Warioba, ilipaswa wananchi waulizwe kama wanautaka Muungano ama hawautaki. Maoni ya wengi kama yangesema wanautaka, ndipo lingekuja swali la Muungano wa namna gani: serikali moja, mbili, tatu, au tano? Na kama wangejibu hawautaki, basi hapo tungeitaka tume ituandalie road map ya kuachana kwa amani. Kipindi cha miaka kama miwli kingetosha kugawana mbao, kuamua uraia mtu anaoutaka, na hapo katiba ya Tanganyika ingeandaliwa.
Sasa tuko kwenye vurugu tupu kwa sababu ya kuogopana kuulizana maswali magumu. Na ukiangalia kwa makini matokeo ya maoni ya wananchi yaliyokubaliwa na tume ya Warioba, utagundua logic ya ninachokisema kwamba;
-Wazanzibari wanaotaka Muungano wa mkataba, hawataki Muungano ila wanajificha ndani ya neno mkataba.
-Watanganyika wanaotaka serikali tatu, hawataki Muungano ila wanazunguka na kujificha ndani ya serikali tatu.
-Watanzania (pande zote mbili) wanaotaka serikali mbili, hawataki Muungano na wanajua haziwezekani kwa sasa ila
wanajificha ndani ya dola kulazimisha serikali mbili ili Muungano uvunjike.
Mwisho wa siku, tunahitaji kiongozi jasiri anayeshimu matakwa ya wananchi akubali wananchi waulizwe kama wanautaka Muungano au hawautaki. Hili ndilo swali la msingi, mengine ni kupotezeana muda.