nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
JUMAMOSI, JANUARI 12, 2013 09:04 GABRIEL MUSHI NA ARODIA PETER, DAR ES SALAAM
*Mahakama ya Kadhi, OIC, Vatican zaibua mjadala
*Washia wao wataka umri wa kupiga kura miaka 16
TUME ya Mabadiliko ya Katiba jana iliendelea na mikutano yake na wawakilishi wa makundi maalum katika jamii wakati ilipoendelea kukusanya maoni kutoka kwa viongozi wa kidini.
Mara baada ya mikutano hiyo iliyoendeshwa kwa nyakati na maeneo tofauti, viongozi wa kidini walikutana na kuzungumza na waandishi wa habari kueleza yale yaliyojiri katika vikao vyao hivyo.
Katika mazungumzo yao, kulionekana kuwapo kwa mvutano na ukinzani mkali wa hoja kati ya viongozi wa Kikristo na Kiislamu kuliko ilivyokuwa kwa watu wa imani tofauti.
Kubwa lililojitokeza na kuonekana kugusa hisia za viongozi wakuu wa dini hizo mbili halikuwa jingine zaidi ya kuendelea kuvutana kuhusu kuwapo ama kutokuwapo kwa Mahakama ya Kadhi hoja ambayo imeendelea kulitafuna taifa hili tangu mwaka 2005.
Mbali ya viongozi wa Kikristo kuendelea kusisitiza msimamo wao wa kupinga juhudi zozote za serikali kujihusisha katika uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, kinyume ilivyosisitizwa na wenzao wa Kiislamu, hoja nyingine iliyoibua mjadala miongoni mwa wawakilishi wa dini hizo mbili ni ile ya Tanzania kuwa au kutokuwa mwanachama wa Nchi za Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).
Wakiwasilisha maoni yao, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), walisema Mahakama ya Kadhi haina maslahi kwa Watanzania wote bali ni kwa kikundi kinachotaka kuhodhi haki za watu wengine.
Makamu Rais wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi alisema itakuwa kosa kama Katiba mpya itaruhusu kuwapo kwa mahakama hiyo, kwani itachochea uhasama.
"Mahakama ya Kadhi, kama chombo cha Kiislamu kina misingi, mamlaka na maamuzi yake, tutanataka isiwe ya kulazimishwa kuingizwa katika mifumo ya kiserikali
"Si vizuri, Serikali kuwa na dini. Tukiruhusu Mahakama ya Kadhi maana yake ni kwamba Serikali imejiingiza kwenye dini… dini imekuwepo kabla ya Serikali hivyo ziwe na taratibu zake na kamwe zisirasimishwe," alisema Niwemugizi.
Kuhusu OIC, Askofu Niwemugizi alisema kumekuwa na usiri mkubwa mno na itakuwa hatari kama itaruhusiwa kwa sababu ina lengo la kuua ukristo.
"Kuhusu OIC, bahati haya kwa kipindi kirefu sasa, mambo hayawekwi wazi, moja ya sheria za OIC ni kueneza uislamu na kufuta ukristo, kwa nchi wanachama mambo ambayo hayana maslahi kwa makundi mengine,
"Katika suala la Ubalozi wa Vatican nchini, si la Tanzania tu ni la kimataifa hivyo ni suala la mahusiano tu kwa kuwa kuna baadhi ya nchi za Kiislamu zenye uhusiano wa moja kwa moja na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu,
"Haya yalikuwa ni makubaliano ya mwaka 1929,kati ya Vatican na Italia ambako ndipo yalipo makao makuu ya baba Mtakatifu.
"Kiongozi wa Vatican, ni kiongozi wa Kanisa Katoliki dunia nzima ana mchango mkubwa wa kijamii, hivyo si vibaya akawa na mwakilishi kila nchi.
"Kuufuta Ubalozi wa Vatican nchini ni sawa na kusema ufute ubalozi wa Iran, kwani nayo ni nchi ya Kiislamu na tunaendelea kuwa na uhusiano mazuri kama taifa pia kama ilivyo kwa Vatican," Askofu Niwemugizi.
CCT
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk. Peter Kitula alisema si haki kuingi mambo ya dini kwenye Katiba ambayo inagusa wananchi wote.
"Na si Mahakama ya Kadhi tu, hata iwe ya mahakama ya kanisa hatuhitaji iingizwe kwenye mfumo wa kiserikali, tunataka Serikali iendelee kutekeleza mambo yake nje ya dini.
"Kama ilivyo katika ibara ya tatu, kipengele kidogo cha nne katika Katiba ya sasa, tunadhani hili libaki kwa kuwa litaendeleza umoja wa Watanzania,
Kuhusu suala la Muungano, CCT inapendekeza Serikali moja au ikishindikana ziwe Serikali tatu.
"Yaani pasiwepo na Serikali ya Zanzibar iliyo na bendera na wimbo wake, kama hii haiwezekani, namna nyingine ni kuwa na serikali tatu ambazo moja ya Zanzibar, Tanganyika na Muungano.
"Serikali hizi, zitaongozwa na mawaziri wakuu na zitakuwa na mambo yake kama nchi zinazojitegemea,Serikali ya Muungano itakuwa na wizara maalum ambazo zitashughulikia masuala ya muungano," alisema.
Katika hatua nyingine, makundi maalum yamependekeza kuwepo kwa Tume huru ya Uchaguzi, ambayo haitateuliwa na Rais kama ilivyo sasa, badala yake ipendekezwe na makundi mbalimbali ya kijamii.
MASHEIKH
Kwa upande wake, Amiri wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha alisema wamependekeza suala la Mahakama ya Kadhi lazima litambuliwe kama chombo kitakachosimamia sheria za jamii ya Waislamu wote.
Alisema hicho ndiyo chombo pekee, ambacho kinaweza kuwaunganisha Waislamu pindi wanapotaka kupata suluhu ya matatizo yao.
"Tunataka Mahakama ya Kadhi, iingie kwenye Katiba mpya ili mambo yetu tuweze kuyaendesha wenyewe, imani na uhuru wetu viwezi wazi,
"Katika hili, tunataka pia Katiba mpya itenge siku ya Ijumaa iwe maalum kwa asili ya kumpuzika kuazia saa 6:00 mchana ili kutoa fursa kwa wafanyakazi na wanafunzi wa Kiislamu kwenda kwenye ibada kama tunavyolekezwa na vitabu vya mwenyezi Mungu.
"Hii ni huduma ya kijamii, kwa sababu miongoni mwa matatizo yanayotupata ni kugombea mali... lakini mgawanyo huu umeelezwa vizuri katika taratibu za Kiislamu, unaepusha ugomvi au vita ya kugombea mali, baada ya mmiliki kuondoka.
"Hili si suala la mchezo kwa sababu isiwe kama mzaha huu, uliofanyika kipindi kilichopita... tunataka chombo kinachokubalika kisheria ambacho kitakuwa na mamlaka.
"Ni sawa na mgonjwa wa saratani anapopelekwa Muhimbili anahamishiwa hospitali ya Ocean Road… Waislamu hawataki sheikh mmoja ana midevu mingi, wanataka wanasheria wenye kujua sheria ya Kiislamu juu ya masuala ya mirathi ndoa na talaka, watengenezewe kama ilivyotengenezwa hosptali ya kutibu saratani.
WASABATO NA MISAADA
Nalo Kanisa la Waadventista wa Sabato, wametaka Katiba mpya itambue vikundi vidogo vidogo vya kidini ili visimezwe na makanisa makubwa.
"Tunataka fursa sawa katika uhuru wa kuabudu bila kukandamizwa, tunaamini tunafanya kazi siku sita, kama jumamosi tunakwenda kuabudu basi tufanye kazi jumapili na watoto wetu wasilazimishwe kufanya mitihani siku za jumamosi ili kuwatendea haki watu wote. "Suala la udini,lisipewe nafasi katika Katiba mpya, kwa maana kuwa masuala ya dini yasiingizwe katika mambo ya kiserikali ... mwenye uwezo wa kuongoza Serikali aangaliwe uwezo wake wala si dini au kabila lake," alisema Askofu Mkuu wa Jimbo la Mashariki mwa Tanzania, Mchungaji Mark Malekana.
WAASIA
Nao Muungano wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithina-Asheri Jamaat ya Afrika, umeitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhakikisha inaingiza kipengele kitakachorushu msichana mwenye umri wa miaka 16 kuolewa.
Akiwasilisha maoni hayo, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mohamed Dhilan alisema miaka 16 ni umri ambao unafaa kwa mwanamke kuolewa na kupiga kura kwa sababu viungo vyake vitakuwa vimekomaa.
"Tunashauri katiba mpya ipige marufuku kugombea zaidi ya awamu mbili kwa sababu viongozi wengi wakikaa huko bungeni wanazoea hadi wanaota mizizi.