hata hilo unalotaka halina tabu,ni kuweka wazi tu, ni mambo gani mnayotaka yashughulikiwe ndani ya dini husika,kwa mfano waislamu wao mambo yao ni matatu, mambo ya ndoa,miradhi,na kutoa maamuzi kama kuna tofauti kuhusu tafsiri za kuruani, sasa hapo matatizo yako wapi?Ikitokea wakubali kuwa iwepo mahakama ya Kadhi humu nchini, basi kifungu hicho kifafanue bayana kuwa kila dhehebu la dini litakalotaka kuwa na mahakama yake kulingana na msahafu wa dini hiyo, linaruhusiwa na Serikali itatambua mahakama hiyo na kuihudumia. Wasipofanya hivyo, watakuwa wagawa wananchi. Niafadhali kuweka msimamo kuwa Serikali haitajihusisha na masuala ya dini yoyote wala bunge lisiburuzwe kujadili mambo ya dini moja na kutaka kuyapa hadhi ya kitaifa!