Katiba Mpya: Warioba aiumbua CCM

Katiba Mpya: Warioba aiumbua CCM

sababu kazi waliyopewa hawajamaliza .... wachakachuaji wanataka kuifupisha kwa sababu hawaungi mkono wachakachuaji wanachotaka wafanye!
 
- Lets say ninataka ubunge eti unatolewa kwa kuandika jamiiforums? ha! ha! ha! nani amepewa ubunge na jamiiforums? ha! ha!

Le Mutuz

Mbona uliomba hapa JF,tukuombee upate ubunge EAC?au umeshasahau maana ni kawaida wana ccm mkisha pata kura mnajisahau kabisa.Sishangai hata mzee john malecela alikua PM,makamu wa kwanza wa rais lakini hakuleta maendeleo mvumi,mtera,na alipokosa ubunge akang'oa visima vyake
 
kuna siku ulialikwa startv, uliongea kama mtu mwenye akili (ilikua mara ya kwanza nakusikia live), ilikua ni wakati ule unasema umejitoa jf (kitu ulichoshindwa kufanya hadi leo)

nilikua nashangaa kwa nini raia hawakuelewi, ninavozidi kusoma post zako ndio ninavyozidi kujua ni kwa kiasi gani wewe ni mwepesi upstairs

Pole sana mkuu huyu le mutuz haeleweki hivyo usimwekee dhamana
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz

Wewe mwenye mwili mkubwa km Miss BANTU,huna lolote! We subiri tu yakija mashindano ya waliojazijazia zile nyama alizowajaza Mwenyenzi Mungu Subhana Wahtalah!! ndio ujitokeze kugombea lakini Siasa huiwezi.

Hata km chanzo cha habari ni Tanzania Daima lakini habari ni ya ukweli. Ina maana wewe hukusoma au kuona habari hii kwenye chombo kingine chochote cha habari!!?
Ndio maana watu wanakudharau sana wewe Miss BANTU! Umesoma lakini hujaelimika.
 
Mkuu,jahazi lazama .. Kutapatapa ndio sehemu ya maisha yao..
Mwanahalisi wamefanikiwa kulizima.. JF na TZ Daima hawawezi katu kudhibiti..wamejitahidi saana kuanzisha VIJARIDA dhidi ya TZ Daima.. lakini hatudanganyiki kwani Ta ya Kijani inatupa Ruksa kusonga Mbele...

Mkuu hata samaki akiwa baharini anakuwa na jeuli ya ajaabu lakini akijinasa kwenye nyavu anakuwa mpole mazima yani magamba mwaka huu ni zaidi ya samaki aliye nasana kwenye nyavu lazima wawe wapole na watanzania tupate katiba tunayo itaka.
 
source ni tanzania chadema. msiba mwingine kwa taifa. wapi ccm imeumbuka.umbea mzigo sana
 
Warioba aiumbua CCM
• Asema muswada uliopitishwa bungeni unalenga kuifuta tume yake

na Irene Mark
Tanzania Daima

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba, amesema Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013 uliopitishwa na Bunge hivi karibuni unalenga kuifuta tume hiyo kabla ya kumaliza muda wake.

Muswada huo ambao ulipitishwa na wabunge wa CCM pamoja na Augustine Mrema wa TLP (Vunjo), ulisusiwa na wabunge wa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kutokana na kuchakachuliwa baadhi ya vipengele huku Zanzibar ikiwa haijashirikishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema miongoni mwa vipengele vilivyofanyiwa marekebisho kwenye sheria hiyo ni kile kinachotaka tume yake ivunjwe baada ya kuanza kwa Bunge la Katiba.
Hoja za Warioba ndizo hizo zinazopigiwa kelele na vyama hivyo vitatu pamoja na makundi ya asasi za kiraia huku viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwabeza na kudai muswada huo ulipitia taratibu zote.

Alisema marekebisho hayo yanakwenda kinyume cha sheria mama iliyounda tume hiyo ambayo inaweka wazi kwamba majukumu ya tume yatafika ukomo baada ya kupigwa kura ya maoni.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, uamuzi wa wabunge hao utaleta mkanganyiko endapo watashindwa kuelewana kwenye baadhi ya vipengele, kwani hapatakuwa na mtu wa kuwafafanulia, kwa kuwa tayari tume itakuwa imevunjwa.

"Sheria iliyounda tume hii inasema wazi kwamba ukomo wa tume ni baada ya wajumbe wa tume hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu kura ya maoni na mchakato wa kupiga kura hiyo utakapokamilika.
"Wao hawaoni sababu ya sisi kuendelea kuwapo hapa, nawaomba watafakari kipengele hicho," alisema Warioba aliyepata kuwa waziri mkuu wa Tanzania.


Kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano wa 12 wa Bunge mjini Dodoma, wabunge wa upinzani walitoka nje wakisusia kupitishwa kwa mabadiliko ya sheria hiyo, wakidai kufutwa kwa baadhi ya vipengele vilivyobadilishwa dakika za mwisho bila kuwahusisha.
Kususa huko wakati kikao kinaendelea kuliambatana na vurugu baada ya Naibu Spika, Job Ndugai, kuwataka askari wa Bunge kumtoa nje Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, jambo lililowafanya wabunge wa vyama hivyo vitatu kutoka wote.

Pamoja na madai hayo, wabunge hao walilalamikia utendaji wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Katiba na Sheria chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana, kwa kubadili vipengele hivyo kabla ya kuupitisha bungeni.
Baada ya wabunge wa upinzani kususa, wabunge wachache wa CCM waliokuwapo ukumbini hapo na Mrema, walipitisha mabadiliko hayo na kuyapeleka kwa rais ili asaini na kuifanya kuwa sheria.

Nje ya Bunge
Moto uliowashwa nje ya Bunge na viongozi wa upinzani pamoja na makundi ya asasi za kiraia umebadili upepo kwani kelele za kumtaka Rais Jakaya Kikwete kutousaini muswada huo zimezidi kuongezeka.
Ni katika hatua hiyo, mawaziri kadhaa, William Lukuvi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Stephen Wasira na Mathias Chikawe wa Katiba na Sheria, wamekuwa wakiendelea kuwabeza wapinzani.

Hivi karibuni Waziri Chikawe alifikia hatua ya kumtisha Rais Kikwete akisema kuwa endapo hatausaini muswada huo kuwa sheria atakuwa ametangaza mgogoro na Bunge.
Pia Wasira naye amenukuriwa akisema kuwa wanaopinga muswada huo usisainiwe lazima wampe rais sababu za kutofanya hivyo, kwa vile hana, na kwamba milango ya Ikulu kwa wapinzani hao kujadiliana na mkuu wa nchi imefungwa
.


Matamshi hayo ndiyo yamewaleta pamoja viongozi wa vyama hivyo na makundi mengine wakizunguka kwa wananchi kuwaeleza karoso zilizomo kwenye muswada huo ambao CCM inataka kutumia turufu hiyo kuhodhi mchakato wa Katiba mpya.

Angalizo la Warioba
Mwenyekiti huyo aliwataka wanasiasa kuacha malumbano katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya, huku akikanusha uvumi kwamba baadhi ya wajumbe wa tume hiyo wametishia kujiuzulu.
Badala yake aliwataka waketi pamoja na kukubaliana kuhusu vipengele wanavyotofautiana kwenye rasimu hiyo, kisha kuwaeleza wananchi manufaa ya kuwa na Katiba ya wote.

"Huu si wakati wa Tanzania kutengana, wanasiasa wanapaswa kutumia fursa walizonazo kukaa pamoja na kushirikiana ili tupate Katiba bora, hatuwezi kupata Katiba kwa maandamano, mikutano na mivutano baina ya vyama vya siasa," alisema.
Kwa mujibu wa jaji huyo, kilichopo kwenye rasimu hiyo ni maoni ya wananchi, hivyo hakuna haja ya kubadili, bali kuboresha ili kila Mtanzania anufaike na uwepo wa Katiba hiyo.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa mabaraza walidiriki kuwakashifu wajumbe wa tume yake, hasa kutokana na wanasiasa kutoa matamshi ya kuwalenga wajumbe hao wa tume.
"Hilo limetusikitisha, matamshi hayo yalitolewa kwa lengo la kuwadhalilisha wajumbe wa tume na kuishushia thamani kazi kubwa wanayoifanya ndani ya tume," alisema.
Jaji Warioba alisema pamoja na changamoto hizo, tume ilifanikiwa kukamilisha mchakato huo ambapo kwa kupitia mikutano 179 ambayo ilihudhuriwa na wajumbe 19,337 wa mabaraza ya Katiba walipata maoni.
Mbali na hatua hiyo, Jaji Warioba alisema tume imepokea maoni kutoka kwa makundi, asasi na taasisi mbalimbali 600 kuhusiana na rasimu ya Katiba mpya.

Alisema baada ya kukusanya maoni hayo, tume inatarajia kuanza mchakato wa kuchambua ili kuandaa ripoti itakayokuwa na maboresho na kuikabidhi kwa rais kwa ajili ya kuendelea kwa mchakato mwingine.
"Tumewahoji wawakilishi wa wananchi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania Bara na Visiwani, zaidi ya vikundi 176 vyenye uwakilishi wa watu tofauti tulikusanya maoni yao.
"Naamini Watanzania wanataka Katiba inayoheshimu utu wa mtu, umoja na kuvumiliana," alisisitiza Jaji Warioba.



kwenye blue, gazeti la udaku mwanzo mwisho
 
Babu Warioba tunakuombea afya wewe na tume yako tukufu mtuvushe ktk huu mto wenye mamba wakali. Kwa vyovyote vile rasimu iliyotoka inaridhisha kwa asilimia kubwa ila kwa CCM inawabana sana kwani wanajua fika sera zao haziendani na matakwa ya rasimu wakati wa utekelezaji!
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz

Kaka nakushauri tu kuwa huku JF tunapita watu wengi sana ambao wako ndani ya system na tuko waheshimiwa wengi sana humu wa CCM, hatuwezi tu kujitangaza majina yetu kutokana na hali ya kisasa na makundi ndani ya chama chetu, Ila kiukweli wewe unazidi kutuharibia sana chama chetu, kama huna la kuchangia sometime just keep quite brother, itasaidia, unaharibu taswira ya chama mbele ya wasomi na wanaojua mambo!!! Hata kama mzee warioba analia anapaswa kuiskilizwa, hata kama hana point ni vizuri akasikilizwa, ninajua wapo wengi hasa akina kibajaji, mwigulu, mama yako mdogo mwenyewe ambao dhamira yao ni kuona tunaendesha Nchi kwa visa, mikasa, ubabe na umimi zaidi!! lakini nawahakikishia mtashindwa tu potelea mbali hata kama katiba itakuja kuandikwa baada ya uchaguzi 2015, Katiba si yetu tu bali ya watoto na wajukuu wetu, wewe umeshaishi zaidi ya nusu ya umri wako, think of Tz not CCM u guys!!
CCM tuache uzandiki, ubinafsi, ubabe na kujifanya hatusikii wakati tunasikia na kuelewa. WATU KAMA WEWE HAWAFAI KABISA KWENYE CHAMA UNLESS MMEKUBALI KUBADILI MAONO NA MITAZAMO YENU, TANZANIA KWANZA CCM BAADAE!!! YOU NEED TO GROWN UP U YOUNG MAN OF GOD!!! May God Mould ur mind for ur own and Gods people interests!!!!!
 
- Source ni Tanzania Daima, halafu Warioba anazidi kujichafua kwa sababu kazi ya tume imeisha tayari sasa analia lia nini?

Le Mutuz
Hebu rudia tena kusoma ulicho andika, kwenye Bold, inaonesha unamashaka na source lakini kwenye underline unaonekana kuiamini habari, sikuelewi? Anyway, kwani Warioba alisemaje? Tupe source nyingine unayoijua!
 
CCM kilichobakia kwao ni kuishi kiujanjaujanja tu! Hawana lolote ndo maana huwezi watofautisha na wakola! Katiba ya wananchi wanafanya kama mali yao. kama Tume iliapa na kupewa muda wa kumaliza kazi yao ambayo ni baada ya kula ya maoni sasa nini kilichopelekea CCM kuwapunguzia muda wao na kuwa kabla ya kupeleka bunge la katiba! CCM ni kama pepo linalotakiwa kukemewa kwa nguvu zote.
 
Katiba Mpya majanga
• Nape afichua hofu ya CCM sasa

na Waandishi wetu
Tanzania Daima

MCHAKATO wa uundwaji wa Katiba mpya uliotarajiwa kuleta umoja, amani na utulivu sasa umegeuka shubiri, baada ya kukithiri kwa mpasuko baina ya njia zinazotumika kuelekea upatikanaji wake.
Mnyukano wa kisiasa ulioanza kuonekana hivi sasa unalifanya taifa lipite kwenye hali tete ambayo wachambuzi wa masuala ya siasa wanalidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa busara na hekima isipotumika kuna hatari taifa likashuhudia vurugu kubwa.

Wakati hofu hiyo ikianza kujitokeza, viongozi wa vyama vya CHADEMA,NCCR-Mageuzi na CUF, jana walikwenda katika Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kumueleza sababu za kupinga muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba na kumtaka Rais Kikwete asisaini muswada huo.

Tanzania Daima Jumapili imedokezwa kuwa mchakato huo umekiweka njia panda Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa Rais Jakaya Kikwete anayekabiliwa na shinikizo kubwa ndani na nje ya chama chake.
Uamuzi wowote atakaouchukua Rais Kikwete unadaiwa utakuwa na athari kwa chama chake ambacho hivi sasa wabunge wake wanasubiri iwapo hatausaini na kuurejesha bungeni ili ufanyiwe marekebisho yanayodaiwa na wapinzani.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili, tangu kupitishwa kwa muswada huo bila ridhaa ya wabunge wa upinzani umebaini kuwa kwa sasa CCM ni lazima iamue kuchukiwa na wananchi kama muswada huo utasainiwa na Rais Kikwete bila mabadiliko au kuondoka madarakani endapo rais akiurejesha muswada huo bungeni ufanyiwe marekebisho na wabunge wakigoma kufanya hivyo.

Kigogo mmoja wa CCM, amelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa hivi sasa chama chao kipo tayari kuchukiwa na wananchi kwa suala la muswada huo kuliko kuondoka madarakani kabla ya muda, ikiwa rais atalazimika kulivunja Bunge.
Inadaiwa kuwa kutokana na kasi ya upingaji wa muswada huo, Rais Kikwete atakuwa kwenye wakati mgumu ambapo kama atausaini ataweza kutoa maagizo ya kurekebishwa kwa vipengele vinavyolalamikiwa kama alivyofanya siku za nyuma.

Hofu kubwa imetanda kwa CCM baada ya tamko la hivi karibuni lililotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba akiwatuhumu wabunge wa CCM ingawa hakuwataja aliposema: “Sheria iliyounda tume hii inasema wazi kwamba ukomo wa tume ni baada ya wajumbe wa tume hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu kura ya maoni na mchakato wa kupiga kura hiyo utakapokamilika, lakini wao hawaoni sababu ya sisi kuendelea kuwapo hapa, nawaomba watafakari kipengele hicho”.

Kauli ya Warioba inafuatia muswada uliopitishwa hivi karibuni na wabunge wa chama hicho bila kuwapo wapinzani, kuwepo na kipengele kinachoivunja tume ya mabadiliko ya Katiba wakati rasimu itakapokuwa inajadiliwa na Bunge maalumu la Katiba, hivyo kusababisha rasimu ya Katiba kukosa watu watakaotetea mawazo ya wananchi yaliyoandikwa na kupitishwa na tume kabla ya kura ya maoni.

Wadau wa siasa wanasema endapo muswada huu utasainiwa na kuwa sheria bila kufanyiwa mabadiliko kuna uwezekano wa kikundi cha watu wachache kuweza kutumia mwanya huo kuingiza mambo ambayo hayajawekwa na tume ya mabadiliko ya Katiba kwa masilahi yao binafsi kwa kuwa tume itakuwa imevunjwa kwa kutumia udhaifu wa muswada unaoleta utata sasa kote nchini.

Hayo yote mawili yanazidi kukiweka Chama Cha Mapinduzi katika njia panda kwa kuwa kama rais atasaini muswada huo, CCM italazimika kuzunguka nchi nzima kutafuta ushawishi kwa Watanzania wengi wanaoonekana kuchukizwa na muswada huo uliopitishwa na wabunge wa chama hicho ukiwa na mapungufu ambayo hata Jaji Warioba tayari ameukosoa.

Pamoja na Jaji Warioba, viongozi wengine wa CCM waliotoa msimamo wao hadharani kusema kuwa wapinzani wapo sahihi katika hoja ya kutoivunja tume ili iweze kusimamia maoni ya wananchi wakati wa Bunge Maalumu la Katiba, ni Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, ambaye amenukuliwa akisema anaona hatari mbele ya Tanzania ijayo.

“Naona hatari mbele ya Tanzania ijayo, suala la Katiba si la kufikiria walio wengi bungeni wanaweza kupitisha kwa wingi wao, na kama rais atasaini pasipo mambo ya msingi kushughulikiwa, basi aviandae vyombo mbalimbali viwe tayari kukabiliana na matokeo yatakayojitokeza.”
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alikaririwa wiki iliyopita akisema kuwa ni vema pande zinazopingana zikasikilizwa hoja zao ili kuepuka kuwaburuza wananchi katika suala la mchakato wa Katiba.

Kufuatia misimamo hiyo ya Jaji Warioba, Samuel Sitta, Kangi Lugola na baadhi ya asasi za kiraia kuhusu suala la kasoro ya muswada huo wa mabadiliko ya Katiba, endapo Rais atasaini muswada huo Chama hicho kitalazimika kujisafisha mbele ya wananchi kwa kutumia nguvu kubwa kwa kupitisha muswada wenye kasoro unaotia doa zoezi la mchakato wa madiliko ya Katiba.

Nape aeleza hofu ya CCM
Tanzania Daima Jumapili lilimtafuta Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kujua msimamo wa chama katika suala hili, Nape alisema: “Hofu yangu ni kuwa rais asiposaini muswada huo, ataingia katika mgogoro kikatiba, itabidi arejeshe muswada bungeni aeleze kwanini hajasaini, na muswada ukishakaa miezi sita wabunge wakaurejesha tena kwake atalazimika kuvunja Bunge. Mimi ninaona afadhali rais asaini muswada huu ili kama kuna upungufu uwekwe mezani kama ilivyokuwa mwanzo, ila nakubali kabisa mzee Warioba ana hoja katika suala la kutovunjwa tume ya mabadiliko ya Katiba kabla ya kutetea rasimu mbele ya Bunge Maalumu la Katiba”.

Alisema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ni asilimia 74 ya wabunge wote, hivyo wakishikilia hoja ya kutobadilisha jambo lolote katika muswada huo baada ya kurejeshewa na rais, matokeo yake ni kuvunjwa kwa Bunge na nchi kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015.
Nape alisema CCM haiko tayari kuingia kwenye uchaguzi kabla ya 2015, hivyo akawataka wanaopinga na kuunga mkono hoja hizo watumie busara na hekima kufikia maridhiano yatakayolijenga taifa.

Kada mmoja wa CCM amelidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa muswada wa mabadiliko ya sheria wa mwanzo nao ulipitishwa ukiwa na kasoro lakini Chama cha Demokrasia na Maendeleo walienda kwa rais wakajadiliana wakakubaliwa viongozi wa CCM walilazimika kwenda Dodoma kuwaeleza wabunge msimamo wa Rais Kikwete na kuwashawishi waukubali.

“Tulipoona kuna hoja tulilazimika kwenda Dodoma kuwaomba wabunge wetu wakubali hoja za CHADEMA ili marekebisho yafanyike ingawa suala hilo lilifanyika kwa taabu sana, sasa zamu hii wabunge wa CCM wanaweza wasikubali hoja za wapinzani, na likiendelea vile rais atalazimika kuvunja Bunge, hili suala limetuweka pabaya sana CCM sijui hatima yetu,” alisema.

Lipumba, Mnyika wafunguka
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amemshauri Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu, Joseph Warioba, kuacha kuzungumzia uchakachuaji wa ukomo wa tume yake pekee bali kwenda mbele zaidi na kujadili upungufu uliopo katika muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko Katiba wa mwaka 2013.

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kikao cha pamoja na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mnyika, alisema kuwa Jaji Warioba alipaswa kwenda mbele zaidi na kutakiwa kujadili namna uchakachuaji wa vifungu mbalimbali vya sheria katika muswada huo ulivyofanyika.

Mnyika alisema kuwa wananchi na makundi mbalimbali yameporwa haki yao kwa kuwa uteuzi wa wajumbe 166 watakaochaguliwa na Rais Jakaya Kikwete ndio watakaoweza kuingia katika Bunge la Katiba.
“Wananchi wamechakachuliwa mamlaka ya Rais Kikwete ya kuteua wajumbe hao ilipaswa kufanywa na wananchi na si rais kama ambavyo muswada huo unavyosema, yote hiyo ni kupora haki za Watanzania,” alisema.

Pia mbunge huyo alisema kuwa kauli ya Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, haitawarudisha nyuma wala kuwafanya wasiendelea na mchakato wa kuwaeleza Watanzania juu ya uchakachuaji uliofanywa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kupitisha muswada huo.
“Tumemsikia Chikawe akisema kuwa Zanzibar pia haikushirikishwa, tuliamini kuwa kwa kauli hiyo angeweza kumshauri Rais Kikwete asisaini muswada huo lakini kwa vile amelewa madaraka hataki kufanya hivyo,” alisema.
Alisema kuwa upinzani wamedhamiria kwenda kwa wananchi kuwapa elimu juu ya muswada huo na kuwa uamuzi huo hautakoma.
Naye Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa wamekutana na Jaji Francis Mutungi na kumueleza juu ya ushirikiano wao na uchakachuaji uliofanywa na wabunge wa CCM juu ya muswada huo na sababu za kumuomba Rais Kikwete asisaini muswada huo.


Alisema kuwa walimjulisha Mutungi sababu ya kuwa na msimamo katika suala hilo na kutaka mwafaka ili kuweza kupata Katiba inayotokana na Watanzania.
Prof. Lipumba alisema kuwa hakuna sababu ya kuendelea na mchakato kwa kuwa kuna uwezekano wa Katiba hiyo kuwa ya chama kimoja.

Alisema ni vema kupata maridhiano katika suala hilo ili Katiba itakayopatikana itokane na Watanzania. “Kama Rais akisaini ina maana Katiba ya Watanzania itakuwa imekwama,” alisema.

Hata hivyo Prof. Lipumba aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 10, mwaka huu katika viwanja vya Jangwani ili kuwa na ushiriki wa kitaifa katika suala hilo.
“Tutafanya maandamano na mikutano ya amani na tutafuata taratibu zote za kisheria na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,” alisema
.


 
Kutoka maktaba yetu.
 
Back
Top Bottom