Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Ingawaje watu wengi husifu sana Katiba ya Kenya, lakini mimi nina mawazo tofauti! Ninaamini hii Katiba itawarudisha Wakenya nyuma sana, ukiiangalia vizuri utaona ya kwamba ni Katiba nzuri lakini sio kwa nchi masikini na inayoendelea kama Kenya!
Kenya bado ina changamoto nyingi sana kama zilivyo nchi nyingi za Kiafrika. Kwa mfano nchi nyingi za Kiafrika wala huwezi hata kuziita Taifa (Nation), bado ni makundi mbalimbali ya watu yanayooishi kwenye nchi moja na kila kundi lina maslahi yake binafsi na wala sio ya nchi nzima!
Sasa ili uweze kujenga Taifa jambo ambalo ni muhimu katika ustawi wa nchi yoyote ile Duniani, unahitaji kuwa na rais au kiongozi aliye na madaraka makubwa, madaraka ambayo yatamuwezesha kuchukua maamuzi magumu lakini ya lazima na yasiyopingwa mahali popote kwa manufaa ya nchi yote, lakini hili sasa hivi Kenya haliwezekani tena.
Kwa mfano tangu Uchaguzi uliopita uliomuingiza Uhuru Kenyatta madarakani, ni kama bado nchi iko kwenye uchaguzi, Uhuru Kenyatta wala hapewi muda wa kupanga na kutekeleza sera zake, kila siku maandamano, hakuna uamuzi atakaochukua ambao hautapingwa kwa maandamano.
Kwa mfano sasa hivi nasikia kuna wabunge wanataka kumshitaki rais wa nchi, sasa atafanya kazi saa ngapi? Ni hivi majuzi tu ametoka kumalizia kesi ya ICC, hajakaa sawa sijui Sukari watu wanapinga, mara sijui waalimu na yote haya ni kwa sababu Katiba mpya inaruhusu!
Hivyo kwangu mimi hii Katiba ya Kenya itawasumbua sana huko mbeleni, kwani ni kosa kubwa sana kwa nchi changa kuvunja vunja madaraka ya rais/ kiongozi na ndio maana hata Wazungu walilijua hili, wakati wa Ukoloni Magavana walikuwa na madaraka makubwa sana na ndiyo waliojenga hizi nchi zetu!!