KATIBA MPYA YA TANZANIA 2026 MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIWA ,ILA MUUNGANO MTALIONGEZEA HAPO ILI TUKOMBOLEKE

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,223
Reaction score
31,465
Misingi ya Katiba yenye mgawanyo madhubuti wa madaraka

1. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wasiteuliwe moja kwa moja na Rais. Wawe na utaratibu wa wazi wa kikatiba/kisheria wa uteuzi au uchaguzi unaowapa uhuru wa kiutendaji. Pia wasiruhusiwe kuwa wajumbe wa Kamati za Siasa za CCM katika mikoa au wilaya wanazoziongoza, ili kutenganisha Serikali na chama.

2. Mawaziri na Waziri Mkuu wasiteuliwe kwa utaratibu unaohitaji idhini ya Bunge kupitia kura ya wabunge. Hii itaongeza uwajibikaji wa mawaziri kwa Bunge badala ya kumuwajibikia Rais pekee.

3. IGP na CDF wasiwe nafasi zinazoteuliwa na Rais pekee. Nafasi hizo zitangazwe wazi, watu wenye sifa waombe, na kuwe na chombo huru cha kitaaluma kitakachofanya usaili na kutoa mapendekezo. Uteuzi wa mwisho uwe na mchakato wa kuthibitishwa na Bunge.

4. Majaji na viongozi wa taasisi muhimu za kikatiba wasiteuliwe na Rais pekee. Kiwepo chombo huru cha uteuzi chenye uwakilishi wa taaluma husika, Mahakama, Bunge na wadau wengine wanaofaa, kwa vigezo vya sifa, uzoefu, uadilifu na uwezo.

5. Tume ya Uchaguzi iwe huru kikatiba, ikiwa na utaratibu wa uteuzi unaozuia chama au Serikali moja kuwa na uwezo wa kuamua nani awe wajumbe wake.

7. Vyombo vya ulinzi na usalama viwe vya Taifa, si vya chama au Serikali ya siku hiyo. Katiba iweke wazi wajibu wao wa kutenda kwa mujibu wa sheria na kutokuwa na ushiriki wa kisiasa wa kichama.
Mamlaka ya Rais ya uteuzi yapunguzwe katika maeneo ambayo uteuzi huo unaweza kuathiri uhuru wa taasisi zinazopaswa kumdhibiti au kumuwajibisha Rais.

8. Bunge lipewe mamlaka makubwa zaidi ya kuisimamia Serikali, ikiwemo uwezo wa kuchunguza na kuidhinisha baadhi ya teuzi muhimu za kitaifa.

9. Mahakama iwe na uhuru kamili wa kiutendaji na kifedha, pamoja na mfumo wa uteuzi unaolinda uhuru wa majaji.

10. Rasilimali za Serikali zitenganishwe kikatiba na shughuli za chama tawala, ili ofisi ya Serikali isitumike kama chombo cha chama.
 
Uzi wako nimeusoma wote na nimepata jibu kwamba Pendekezo la katiba iliyo kwenye tovuti ya www.katibampya.com imetoa majibu ya maswali yako yote.

Kwanza kabisa Rasimu hiyo ya katiba imeanza na kutatua muundo wa dola kwa kuqeka mibimili minne ya kitaifa, yaani.
1. Baraza l usimamizi wa taifa
2. Serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania
3. Bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
4. Mahakama ya jamhuri ya muungano wa tanzania

Kwa mujibu wa Rasimu hiyo Baraza la usimamizi wa taifa, Ndio mamlaka ya kimuungano, Mamlaka ya usimamizi wa misingi ya kitaifa, Tathmini na muongozo. Baraza limetamkwa katika sura ya nne ya katiba hiyo kuanzia ibara ya 98 mbaka 116 kisha kufuatia mihimili mingineyo sambamba kama ilivyotamkwa hapo juu.

Pia kwwnye maswala ya uteuzi kuna KAMATI KUBWA NA NDOGO YA UTEUZI ILIYOWEKWA KWENYE ibara ya 236 na 237 , Kamati hizo zimeweka uwiano wa mamlaka kwa kiwango cha juu kwa list ya wote uliowaweka hapo na kuweka masharti mbali mbali kwa kila mteuliwa.

Unaweza kufika kwenye tovuti hiyo kuisoma rasimu hiyo, kuisambaza kwa wengine kwa kuwapa jina la tovuti, n.k
 
Misingi ya Katiba yenye mgawanyo madhubuti wa madaraka

1. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wasiteuliwe moja kwa moja na Rais. Wawe na utaratibu wa wazi wa kikatiba/kisheria wa uteuzi au uchaguzi unaowapa uhuru wa kiutendaji. Pia wasiruhusiwe kuwa wajumbe wa Kamati za Siasa za CCM katika mikoa au wilaya wanazoziongoza, ili kutenganisha Serikali na chama.

2. Mawaziri na Waziri Mkuu wasiteuliwe kwa utaratibu unaohitaji idhini ya Bunge kupitia kura ya wabunge. Hii itaongeza uwajibikaji wa mawaziri kwa Bunge badala ya kumuwajibikia Rais pekee.

3. IGP na CDF wasiwe nafasi zinazoteuliwa na Rais pekee. Nafasi hizo zitangazwe wazi, watu wenye sifa waombe, na kuwe na chombo huru cha kitaaluma kitakachofanya usaili na kutoa mapendekezo. Uteuzi wa mwisho uwe na mchakato wa kuthibitishwa na Bunge.

4. Majaji na viongozi wa taasisi muhimu za kikatiba wasiteuliwe na Rais pekee. Kiwepo chombo huru cha uteuzi chenye uwakilishi wa taaluma husika, Mahakama, Bunge na wadau wengine wanaofaa, kwa vigezo vya sifa, uzoefu, uadilifu na uwezo.

5. Tume ya Uchaguzi iwe huru kikatiba, ikiwa na utaratibu wa uteuzi unaozuia chama au Serikali moja kuwa na uwezo wa kuamua nani awe wajumbe wake.

7. Vyombo vya ulinzi na usalama viwe vya Taifa, si vya chama au Serikali ya siku hiyo. Katiba iweke wazi wajibu wao wa kutenda kwa mujibu wa sheria na kutokuwa na ushiriki wa kisiasa wa kichama.
Mamlaka ya Rais ya uteuzi yapunguzwe katika maeneo ambayo uteuzi huo unaweza kuathiri uhuru wa taasisi zinazopaswa kumdhibiti au kumuwajibisha Rais.

8. Bunge lipewe mamlaka makubwa zaidi ya kuisimamia Serikali, ikiwemo uwezo wa kuchunguza na kuidhinisha baadhi ya teuzi muhimu za kitaifa.

9. Mahakama iwe na uhuru kamili wa kiutendaji na kifedha, pamoja na mfumo wa uteuzi unaolinda uhuru wa majaji.

10. Rasilimali za Serikali zitenganishwe kikatiba na shughuli za chama tawala, ili ofisi ya Serikali isitumike kama chombo cha chama.
ok.🐒
 
Back
Top Bottom