Katiba na maamuzi ya mahakama za kimataifa

Joined
Oct 12, 2012
Posts
52
Reaction score
10
Habari wanajf!! Mimi nataka kufahamu kwamba kwakuwa katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa tanzania ni sheria mama na ni zao la wananchi wa tanzania, na kwamba sheria za kimataifa ili zitambulikd nchini lazima zifate taratibu zilizowekwa na katiba hii!! Lakini je maamuzi ya mahakama za kimataifa yana nafasi gani juu ya katiba hii!!? Mfano maamuzi ya mahakama ya haki za binadamu afrika kwa upande wa mtikila na law society of tanganyika!!
I beg to submit!!
 
Sasa mkuu funguka zaidi hiyo mtikila na law society ni kesi ama nin? Maana swali kama vile halijawa clear kwa upande wangu funguka kwa kina kama ni kesi mbili tofauti au inakuaje..!! Samtyms unaweza usieleweke kwa kushindwa kuwasilisha swali vizuri
 
Kesi ya mtikila na tanganyika law society zilifanana katika kupinga mabadiliko ya kumi na moja ya katiba na kuomba kuhalalishwa kwa swala la mgombea huru katika katib yetu!! rufaa iliyowasilishwa katika mahakama ya haki za binadamu afrika, maamuzi yakawa kwa upande wa hao warufani!! Sasa ninachouliza ni je maamuzi ya hiyo mahakama yananafasi ipi juu ya katiba ya nchi inayoweka misingi ya utoaji haki kwa kuunda chombo cha kutoa haki ambacho ni mahakama zetu tukufu!? Na je maamuzi ya mahakama za nje yanatambulika na katiba yetu!! Je tuyaimplement hayo maamuzi na kuweka katiba yetu kuwa subject to the orders of amendments from the african court of human rights!! Kama nitakuwa sijaeleweka plz naombeni nijuzwe tuweze kujadili tujue hatma ya katiba zetu na maamuzi ya kimataifa!!
 
Kimsingi maamuzi ya mahakama za kimataifa ni sehemu ya vyanzo vya sheria katika dola (states) mbalimbali, ila ili ziweze kuwa na nguvu (binding ness) ni lazima zikubalike na sheria mama na nchi husika ( ratification of laws) kwa mantiki hii hukumu nyingi na sheria za kimataifa zinaangukia katika kundi la sheria laini ( soft laws). hivyo nguvu yake katika utekelezwaji inategemea utayari wa nchi husika, ndio maana sheria nyingi hasa za kimazingira (environmental laws) zinaelekeza mambo mengi lakini mara nyingine nchi husika zinagomea utekelezaji wake mfano marekani ilivyogomea kusaini na utekelezaji wa mkataba wa Kyoto kuhusu kupunguza uzalishaji wa gesi zinazoharibu ozone layer, aidha ni hivyo hivyo ambapo mahakama ya kimataifa ICJ ilipotoa tamko la kumkamata Albashir lakini hakuna nchi inayolazimishwa kumkamata ndio maana hadi leo anadunda afrika. Kwa msingi huo hata maamuzi unayoyazungumzia kuhusu kesi ya mtikila bado yako ndani ya discretion ya nchi kuamua kuifata au la maana still ni soft law
 
decision ya mahakama hiyo iko binding on us,kwa kuwa tulijiunga wenywe na hiyo Mahakama,na hata kama,mtu au taasisi haiwezi kupeleka madai kwenye hiyo Mahakama hadi i-exhaust all means of justice katika nchi yako na ikashindikana ndio utapata kibali cha kupeleka madai yako huko,ila once the decision is made,it is binding,foreign awards.ndio maana kama unavyoona Mtikila alivyolalamika abt mgombea binafsi,sasa na hii katiba mpya lazima kuwe na changes.As long as tumeratify mikataba katika establishment ya hiyo Mahakama,tumekubaliana na Articles zake pia..hii ni kwa maoni yangu tu
 
@ viva89
Nashukuru kwa mchango wako ndugu, lakini kwa namna ya utekelezaji wa mikataba na sheria zingine za kimataifa utambue kuwa tupo katika mtazamo wa kidualism… hadi sheria au mkataba hucka upitishwe kwa maridhio ya bunge! Na hii taratibu imewekwa na katiba.
 
Sheria nyingi, au maamuzi mengi ya mahakama za kimataifa hayatekelezwi na mataifa husika kwa sababu ya "Enforcement".
Enfocement za maamuzi ya mahakama hizi hutegemea nchi wanachama.

Na njia ya enforcements za hizi mahakama ni allienation au kususiwa na nchi wanachama wa mahakama hiyo, kiuchumi n.k jambo ambalo nchi nyingi zinazohusiana kiuchumi symbiotically huwa hazitekelezi kwa madai ya kutoingilia sovereignty.

Most of these courts enforcement yake imebase purely on "Outcasting" .....
Mfano mzuri ni kama excommunication in classical canon law au hata Outlawry in medieval Icelandic law.

Kwa ufupi, maamuzi yake hayana effects za maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…