Katiba ni Wananchi si ya serikali- James Mbatia

Katiba ni Wananchi si ya serikali- James Mbatia

bmbalamwezi

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2015
Posts
788
Reaction score
195
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI Taifa, Bwana James Mbatia amewasaidia kuwaondolea ujinga waliokuwa wakisema kuwa Katiba Inayopendekezwa ni ya Chenge na Sitta. Bwana Mbatia amesema kuwa Katiba ni ya Wananchi na si ya serikali kwani Katiba Ndiyo inayoizaa serikali. Bwana Mbatia amesema hayo katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV. Hivyo wananchi inabidi muelimike mkijua kuwa Katiba Inayopendekezwa ni yenu. Mkijidai kususia mchakato wa kura ya maoni mlitaka kujisusia wenyewe. Na kwa uelewa huo. Ipigie kura ya Ndiyo Katiba Inayopendekezwa wakati ukifika.
 
Katiba ni ya wananchi na si ya serikali kwani Katiba ndiyo inayoizaa serikali. Hivyo ipigie kura ya ndiyo kama ulivyofafanuliwa na Mwenyekiti wa NCCR- MAGEUZI Taifa, Bwana James Mbatia. Uelewe kuwa Katiba si ya Chenge wala Sitta ni yako na mimi. Upo hapo ndugu. Kazi kwako.
 
Katiba siyo mali ya ccm ni mali yetu sisi wananchi ccm katiba waliyoiandika wenyewe tutapiga kura za Hapana
 
Katiba siyo mali ya ccm ni mali yetu sisi wananchi ccm katiba waliyoiandika wenyewe tutapiga kura za Hapana
wewe mbna unakuwa kama samaki pori? Mmeshaambiwa kuwa ni ya Wananchi sasa nani kakwambia kuwa ni ya ccm? Umekimbia mirembe wewe au? Uwe muelewa sasa! Na ukae ukijua kuwa UKAWA wameahidi kuipigia kura ya NDIYO siku ikifika so kaa chonjo kwa hilo.
 
wewe mbna unakuwa kama samaki pori? Mmeshaambiwa kuwa ni ya Wananchi sasa nani kakwambia kuwa ni ya ccm? Umekimbia mirembe wewe au? Uwe muelewa sasa! Na ukae ukijua kuwa UKAWA wameahidi kuipigia kura ya NDIYO siku ikifika so kaa chonjo kwa hilo.

Acha upotoshaji Ukawa walishatoa tamko la kutoshiriki .
 

Attachments

  • 1429119142203.jpg
    1429119142203.jpg
    31.7 KB · Views: 117
Katiba sio ya UKAWA umeliwa nyie ndo wale mnaofungwa magoli kwa uzembe mnategemea kubebwa na refa!kalia kushikiwa akili mpaka siku ya uchaguzi mkuu utasubiri UKAWA ikakupigie kura!!
 
[h=2][audio] "Haturudi kwenye Bunge Maalum la Katiba" - UKAWA [/h]
ukawa1.jpg

Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono mara baada ya kuongea na waandishi wa habari kutoa tamko la UKAWA kuhusu wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.

Kutoka kulia ni Profesa Safari Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambabe, Mwenyekiti wan CHADEMA Freeman Mbow, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Wilbrod Slaa, Mbunge Sakaya na Julius Mtatiro wakiwa nje ya Makao Makuu ya CUF
Ripoti ya Dina Chahali, via VOA - Umoja wa katiba ya wananchi- UKAWA na Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Tanzania bado wanavutana juu ya uendeshaji wa bunge hilo maalum la katiba jambo linalozusha shaka juu ya mustakbali wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania.

Wajumbe wanaounda UKAWA chini ya uenyekiti wa mwenyekiti wa taifa wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba wameendelea na msimamo wake wa kutokurejea katika bunge maalum la katiba linalotarajiwa kuanza tena vikao vyake Agosti tano mwaka huu, kwa siku 60 zilizoongezwa na Rais Kikwete ambapo ilitarajiwa wakikamilisha awamu hiyo itarudishwa kwa wananchi kwa ajili ya
kura za maoni.
Imeelezwa kwamba ili Katiba inayopendekezwa iweze kupata uhalali wa kupitishwa kwake, sheria inaweka sharti kwamba ni lazima ikubalike na pande zote za muungano kwa zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote kwa kila upande.

Wakitoa tamko juu ya msimamo wao jijini Dar es Salaam, Alhamis viongozi wa UKAWA akiwemo mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe na mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI James Mbatia, wamesema wako tayari kurudi bungeni pindi rasimu hiyo ya katiba iliyowasilishwa bungeni na tume ya mabadiliko ya katiba ambayo ni maoni ya wananchi, itakapojadiliwa na si vinginevyo.

UKAWA waliondoka bungeni April 16 baada ya kususia bunge maalum la katiba kwa madai kwamba bunge hilo halijadili rasimu yenye maoni ya wananchi ambayo iliwasilishwa bungeni hapo na Jaji Joseph Warioba pamoja na kulaumu kwamba bunge hilo linaendeshwa kibabe kwa kufuata matakwa ya chama tawala cha CCM kinachosisitiza kuwepo na serikali mbili ya muungano badala ya iliyopendekezwa katika rasimu ya pili ya muungano wa serikali tatu.

Hadi kikao cha kwanza cha bunge maalum la katiba huko mjini Dodoma kilipoahirishwa April 25 mwaka huu kupisha bunge la bajeti, wajumbe wa UKAWA walikuwa wamesusia vikao na kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi kwamba walichosusia ni mwenendo mbovu wa bunge hilo.
 
Katiba sio ya UKAWA umeliwa nyie ndo wale mnaofungwa magoli kwa uzembe mnategemea kubebwa na refa!kalia kushikiwa akili mpaka siku ya uchaguzi mkuu utasubiri UKAWA ikakupigie kura!!

Endeleeni kujipa moyo
 

Attachments

  • 1429119825224.jpg
    1429119825224.jpg
    50 KB · Views: 75
Katiba ni ya wananchi. Katiba Inayopendekezwa ni ya Chenge na Sitta. Bado haijawa Katiba
 
wewe mbna unakuwa kama samaki pori? Mmeshaambiwa kuwa ni ya Wananchi sasa nani kakwambia kuwa ni ya ccm? Umekimbia mirembe wewe au? Uwe muelewa sasa! Na ukae ukijua kuwa UKAWA wameahidi kuipigia kura ya NDIYO siku ikifika so kaa chonjo kwa hilo.

Kura lini?
 

Attachments

  • 1429119919618.jpg
    1429119919618.jpg
    97.4 KB · Views: 66
[h=1]Warioba: Kazi ya Bunge la Katiba siyo kubadili Rasimu[/h]
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge Maalumu la Katiba kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.

Akihutubia mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), wa tafakuri na maridhiano kuelekea Katiba Mpya jana, Jaji Warioba alisema:
"Madaraka ya Bunge Maalumu yamekuwa yanabadilika kwa kutegemea aina ya mchakato unaotumika. Afrika Kusini, Namibia na Cambodia, Bunge Maalumu lenyewe ndilo lilipewa jukumu la kuandika Rasimu ya Katiba. Katika mazingira haya, Bunge Maalumu lilikuwa na madaraka ya kubadilisha mambo mengi katika Rasimu ya Katiba… lilikuwa na madaraka ya kuachana na Rasimu ya Katiba na kuandika Rasimu Mbadala.
"Madaraka ya Bunge Maalumu yanakuwa na mipaka endapo Rasimu ya Katiba imeandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba au chombo cha aina hiyo.

Bunge Maalumu linaweza kuwa huru kurekebisha baadhi ya masharti yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba lakini si suala la kawaida Bunge Maalumu kubadili hoja ya msingi. Jinsi ushirikishaji wa wananchi unavyokuwa wa wazi na mpana ndivyo madaraka ya Bunge Maalumu yanavyopungua."
"Mantiki ni kuzuia Bunge Maalumu kunyang'anya madaraka ya wananchi, yaani "act of popular sovereignty". Wataalamu wa masuala ya Katiba wanaeleza kuwa madaraka ya Bunge Maalumu katika mazingira haya ni kuboresha Rasimu ya Katiba.
"Kwa mujibu wa Kifungu cha 25(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, Bunge Maalumu limepewa madaraka ya kujadili na kupitisha masharti ya Katiba, kutunga Sheria ya Masharti ya Mpito na Masharti yatokanayo na kabla ya kuanza kazi hiyo, Bunge Maalumu litapitisha Kanuni za Bunge Maalumu ambazo zitaongoza utekelezaji wa mamlaka ya Bunge Maalumu."
Bunge Maalumu la Katiba litaanza kukutana Jumanne ijayo kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30, mwaka jana.
Moja ya masuala yanayotazamiwa kusababisha mvutano mkubwa kwenye vikao vyake ni lile la muundo Muungano na hasa suala la Serikali Tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataka kusukuma ajenda ya kuendelea kwa muundo wa Serikali Mbili Bunge la Katiba wakati vyama vya upinzani vinataka mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Serikali tatu yaheshimiwe.
Jaji Warioba alisema Bunge Maalumu linapaswa lifanye kazi ya kuboresha masharti ya kikatiba yaliyomo ndani ya Rasimu ya Katiba pasipo kuweka masharti mapya ambayo kwa taathira yake yanabadilisha au kufifisha yaliyomo kwenye rasimu hiyo.
Kuhusu mchakato wa kupata Katiba Mpya Tanzania, Jaji Warioba alisema kila mtu anafahamu kuwa ulifuata utaratibu wa kuandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo maana hata Bunge Maalumu la Katiba litakapokutana Dodoma litatakiwa kufuata utaratibu huo.
Jaji Warioba alisema utungaji wa Katiba unatakiwa kuwa shirikishi kwa maana ya kuwahusisha wananchi katika hatua zote za mchakato kwa maelezo kuwa kwa kadri mchakato wa kuandika Katiba unavyowashirikisha kwa mapana, ndivyo utakavyoongeza uwezekano wa kukubalika, kuheshimika na utekelezaji wa Katiba utakavyokuwa rahisi.
"Wananchi wanaposhiriki katika utungaji wa Katiba na pale matakwa yao yanapozingatiwa ndani ya Katiba, wananchi hao huimiliki Katiba hiyo na kuiona kuwa ni yao. Wananchi huona hivyo kwa sababu licha ya kushiriki lakini pia Katiba hiyo huakisi utashi wao na ndoto zao na hivyo kukubali kuongozwa na masharti yaliyomo ndani ya Katiba," alisema.
Apinga kura kupitisha maoni
Akizungumzia upigaji wa kura katika kufanikisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya, Jaji Warioba alionya akisema hatua hiyo itasababisha kuzaa Katiba itakayopingwa na wananchi wengi.
"Bunge la Katiba lina jukumu la kusimamia mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba ya wananchi wote. Kama tunataka kuunganisha Taifa, tukubaliane kwa maridhiano, mkikubaliana kwa kupiga kura siku hiyohiyo Katiba itaanza kupingwa," alisema Jaji Warioba.
Dk Bilal asema kura itaamua
Akifungua mkutano huo, Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal alisema suala la mchakato wa Katiba ni zito na hutokea mara chache katika maisha hivyo kumtaka kila aliyepata wasaa wa kushiriki katika Bunge Maalumu la Katiba, kutumia fursa kwa busara.
Dk Bilal alisema ni vizuri wanasiasa na wadau wote kujiandaa kupokea matokeo ya kura kama itakavyopigwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.
Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuonyesha mfano kwa kuhubiri amani ili mchakato wa Katiba umalizike kwa amani huku kila mmoja akiweka masilahi ya taifa kwanza na yale ya kisiasa baadaye.
"Katiba ni yetu wote, hatuna haja ya kutoana ngeu… tukiweka Tanzania kwanza tutafanikiwa, lakini tukiweka masilahi yetu ya siasa mbele hatuwezi kufanikiwa… kila mmoja wetu atumie fursa hii kwa busara," alisema.
Mbatia atoa angalizo
Mwenyekiti wa TCD, James Mbatia alisema Katiba siyo mali ya viongozi na wanasiasa, bali ni ya wananchi wote na kuwakumbusha wote waliopewa jukumu la kuiandaa kuelewa kuwa wananchi wanataka Katiba inayoakisi ndoto na matarajio yao na itakayopunguza na au kuondoa hofu waliyonayo ya kuzidi kuwa maskini na fukara.
"Katiba haipatikani kwa wingi wa kura, bali kwa kugusa mioyo ya kila anayeshiriki kuona kwamba amekuwa sehemu ya maridhiano yaliyopatikana. Ni vizuri tukubaliane leo na kesho kuweka misingi ya pamoja ya kuhakikisha tunapata Katiba Mpya kwa njia ya kujadiliana na kuridhiana," alisema Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.
Source : Mwananchi
Imeandikwa Na : Joyce Mmasi
 
[h=1]SIKILIZA MANENO MACHACHE YA JAMES MBATIA BUNGE LA KATIBA[/h]
 
Last edited by a moderator:
[audio] "Haturudi kwenye Bunge Maalum la Katiba" - UKAWA
ukawa1.jpg
Viongozi wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakishikana mikono mara baada ya kuongea na waandishi wa habari kutoa tamko la UKAWA kuhusu wito wa Viongozi wa Dini wa kurudi Bungeni.Kutoka kulia ni Profesa Safari Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Mosena Nyambabe, Mwenyekiti wan CHADEMA Freeman Mbow, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Wilbrod Slaa, Mbunge Sakaya na Julius Mtatiro wakiwa nje ya Makao Makuu ya CUF Ripoti ya Dina Chahali, via VOA - Umoja wa katiba ya wananchi- UKAWA na Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Tanzania bado wanavutana juu ya uendeshaji wa bunge hilo maalum la katiba jambo linalozusha shaka juu ya mustakbali wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania.Wajumbe wanaounda UKAWA chini ya uenyekiti wa mwenyekiti wa taifa wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba wameendelea na msimamo wake wa kutokurejea katika bunge maalum la katiba linalotarajiwa kuanza tena vikao vyake Agosti tano mwaka huu, kwa siku 60 zilizoongezwa na Rais Kikwete ambapo ilitarajiwa wakikamilisha awamu hiyo itarudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni.Imeelezwa kwamba ili Katiba inayopendekezwa iweze kupata uhalali wa kupitishwa kwake, sheria inaweka sharti kwamba ni lazima ikubalike na pande zote za muungano kwa zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote kwa kila upande. Wakitoa tamko juu ya msimamo wao jijini Dar es Salaam, Alhamis viongozi wa UKAWA akiwemo mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe na mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI James Mbatia, wamesema wako tayari kurudi bungeni pindi rasimu hiyo ya katiba iliyowasilishwa bungeni na tume ya mabadiliko ya katiba ambayo ni maoni ya wananchi, itakapojadiliwa na si vinginevyo.UKAWA waliondoka bungeni April 16 baada ya kususia bunge maalum la katiba kwa madai kwamba bunge hilo halijadili rasimu yenye maoni ya wananchi ambayo iliwasilishwa bungeni hapo na Jaji Joseph Warioba pamoja na kulaumu kwamba bunge hilo linaendeshwa kibabe kwa kufuata matakwa ya chama tawala cha CCM kinachosisitiza kuwepo na serikali mbili ya muungano badala ya iliyopendekezwa katika rasimu ya pili ya muungano wa serikali tatu.Hadi kikao cha kwanza cha bunge maalum la katiba huko mjini Dodoma kilipoahirishwa April 25 mwaka huu kupisha bunge la bajeti, wajumbe wa UKAWA walikuwa wamesusia vikao na kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi kwamba walichosusia ni mwenendo mbovu wa bunge hilo.
HUNA JIPYA TYTA aka Tetty UNATULETEA STORY YA APRIL MWAKA JANA KULINDA MASLAHI YAKO HAPA HA HA HA HA MH:MBATIA ANAJIELEWA NA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WA UKAWA WANAODRIVE LILE KUNDI, TOKA APRILI 2014 MPAKA LEO APRILI 2015 NI MWAKA SASA UKAWA WAMETUBU MAKOSA YAO YA KULIKIMBIA BUNGE NA WANAJUTIA UAMUZI WAO KWA KUWA HAUKUZAA MATUNDA NA TULIWASHANGAA, KWA JAMBO HILO MBATIA AMELIONA HILO NA ANASISITIZA HAKUNA MWENYE HATI MILIKI YA KATIBA IWE NI UKAWA, CDM,CCM,CUF,TLP,NCCR-MAGEUZI, NLD n.k UZALENDO KWANZA , NA MAMA TANZANIA KWANZA KAMA KAULI MBIU YAKE, KATIBA NI YA WANANCHI, GOOD JOB MBATIA.
 
sikiliza maneno machache ya james mbatia bunge la katiba




aprili 2014 mpaka aprili 2015 ni mwaka sasa hiyo ni paste tense,tunazungumzia ya itv aliyozungumza mhe:mbatia usitafute huruma mh.anajitambua, na utaokoteza viclip mpaka ufe.
 
Last edited by a moderator:
aprili 2014 mpaka aprili 2015 ni mwaka sasa hiyo ni paste tense,tunazungumzia ya itv aliyozungumza mhe:mbatia usitafute huruma mh.anajitambua, na utaokoteza viclip mpaka ufe.
kura zinapigwa lini?
 
aprili 2014 mpaka aprili 2015 ni mwaka sasa hiyo ni paste tense,tunazungumzia ya itv aliyozungumza mhe:mbatia usitafute huruma mh.anajitambua, na utaokoteza viclip mpaka ufe.
Mwambie atafute clip ya Jumatatu ya kipindi cha Dakika 45 asikie vizuri Bwana Mbatia akilonga kuwa katiba ni ya wanachi na si ya serikali.
 
James Mbatia ana akili ndo mana Rais wa chama kilichokulea wewe unayepinga Katiba Inayopendekezwa alimteua Mbatia kuwa Mbunge. Rais alifahamu kuwa Mbatia ni kifaa na si mnafiki yeye huenda kwa hoja!
 
Back
Top Bottom