Katiba pendekezwa itaifanya ZNZ kutumia rasimali zake ikiwa ni pamoja na kuchimba gesi na mafuta

Katiba pendekezwa itaifanya ZNZ kutumia rasimali zake ikiwa ni pamoja na kuchimba gesi na mafuta

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Napenda kuwasihi ndugu zangu wazanzibar ambapo binafsi nina undugu nao wa damu kabisa kwa upande wa mama yangu mzazi kuisoma vizuri kabisa, Katiba Inayopendekezwa, kifungu kwa kifungu ili kuepuka matukio ya upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na wapinzani ambao wanataka kuficha ukweli kuhusu ubora wa katiba hiyo.

Karibia mambo yote yaliyokuwa kikwazo na kero kwa Wazanzibari kuhusiana na Muungano yamepatiwa ufumbuzi na kuwekwa sawa baada ya kutolewa ufafanuzi wa kina katika Katiba Inayopendekezwa.

Suala la ardhi ni miongoni mwa mambo yaliyofanyiwa ufafanuzi wa kina katika Katiba Inayopendekezwa lakini ukawa na wamekuwa wakipotosha suala hilo kwa makusudi kwa kudai kuwa "Ardhi ya Zanzibar imeuzwa Bara."
Katika sura ya Tatu, Ibara ya Katiba 23 hadi 26 katika Katiba Inayopendekezwa imeweka ufafanuzi mzuri wa matumizi ya ardhi kwa upande wa Bara na kwa upande wa Zanzibar na kutaja ardhi ndiyo rasilimali kubwa ya kukuza uchumi na maendeleo ya ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa Katiba Pendekezwa, matumizi ya Ardhi kwa upande wa Tanzania Bara sheria zake zitatungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati sheria za Ardhi na matumizi yake kwa upande wa Zanzibar zitatungwa na Baraza la Wawakilishi.

Katiba Inayopendekezwa imeondoa suala la Ardhi katika orodha ya mambo ya Muungano ambayo yapo 16 na kwamba hatua hiyo itaifanya Zanzibar kutumia rasilimali zake ikiwa ni pamoja na kuchimba rasilimali ya mafuta na gesi.
Katiba Inayopendekezwa imetoa fursa kubwa kwa Wazanzibari ambao sasa watakuwa na fursa ya kikatiba kutumia ardhi iliopo Tanzania kwa shughuli zao zote ikiwemo biashara na kilimo. Aidha wananchi wa Tanzania Bara waliopo Zanzibar nao wanayo fursa na haki ya kikatiba kutumia Ardhi iliopo Zanzibar kwa shughuli zao mbali mbali ikiwemo ujenzi wa nyumba za kudumu.

Ukawa na cuf kwa pamoja wamekuwa wakivusha kuwa ardhi ya Zanzibar imeuzwa Tanzania Bara, wanapaswa kuwapuuza kwa sababu katiba hii imetoa fursa kubwa kwa Wazanzibari kutumia ardhi iliopo Bara kwa matumizi yao mbalimbali bila ya bughudha ninaondoa kero zilizopo, kjiografia ukubwa wa ardhi iliopo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo eneo la Bara lina ukubwa wa kilomita za mraba wastani zaidi laki tisa, wakati Ardhi iliopo Zanzibar ni kilomita za mraba 2,600 tu.

Kiuhalisia ardhi ya Zanzibar hata kwa matumizi ya Wazanzibari wenyewe ndiyo maana sehemu kubwa ya wananchi wa Zanzibar waliopo Tanzania Bara wanamiliki maeneo makubwa ya ardhi Tanzania bara bila matatizo wala ubaguzi wowote.

Wapinzani na UKAWA kwa makusudi wamekuwa wakifanya upotoshaji wa makusudi kinyume na misingi ya kiungwana baada ya kuona wanashindwa kujenga hoja za msingi za kuikosoa Katiba Inayopendekezwa wamebakia kutengeneza fitina za kuwachonganisha watu wa Bara na Zanzibar.

inashangaza kuona Cuf wanapinga Katiba Inayopendekezwa wakati ina mambo ambayo wao wenyewe waliyapendekeza wakati walipokuwa katika vikao vya Baraza la Wawakilishi, walipitisha azimio la kutaka masuala ya ardhi, mafuta na gesi kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano, jambo ambalo limepitishwa na Katiba Inayopendekezwa lakini bila aibu wanaipinga Katiba hiyo.

Bunge la Katiba lilikubaliana na hoja hiyo na masuala ya gesi na mafuta yamepatiwa ufumbuzi na kuondolewa kwenye Muungano sasa wapinzania wanachopinga ni nini? Kitendo cha Ukawa kuisusia Katiba Inayopendekezwa na kuwashawishi wafuasi wao kutoipigia kura kinaonesha jinsi watu hao walivyokuwa hawana imani na uchungu wa wananchi wa Zanzibar ambao wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana.

Kwa sababu ikiwa Katiba Inayopendekezwa itapigiwa kura ya ndio kwa wingi itatoa fursa na nafasi kwa Zanzibar kuanza kuchimba mafuta na gesi kwa ajili ya kujenga mazingira mazuri ya kiuchumi na ustawi wa jamii kwa wananchi wake. Anafahamisha kuwa juhudi zimeanza kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibair ikiwemo kuwasomesha vijana mbali mbali katika fani ya mafuta na gesi.
 
mwarobaini wa muungano ni katiba pendekezwa tu, hakuna zaidi ya hapo
 
Nchi hii hata ufanye jema gani wewe utaonekana hufai tu ili balaa kweli.
 
tatizo tuna wasaka tonge wanaotaka muungano ufe wagawane vyeo

Anae ona hapa tz apamfai mimi nagharamia paspot na visa akaishi kongo tumechoka kila kitu kupunga tu kwenye ela hawapingi si ujinga huu sasa.
 
Waambie wahuni wenzako ccm kuhusu katiba inayopendekezwa.....Watz wanataka katiba waliyoiwasilisha kupitia mzee wao wa heshima jaji joseph sinde warioba.
OCTOBER 2015 NDO MTAJUA KUWA WANANCHI NDO WENYE NCHI NA SIO ccm
 
Waambie wahuni wenzako ccm kuhusu katiba inayopendekezwa.....Watz wanataka katiba waliyoiwasilisha kupitia mzee wao wa heshima jaji joseph sinde warioba.
OCTOBER 2015 NDO MTAJUA KUWA WANANCHI NDO WENYE NCHI NA SIO ccm

Kazi yako ni jina lako. Kwenye avatar yako ulivyovaa tuu, bila shaka lolote wewe ni muhuni tuuu! Hiyo inajidhirisha kwa maneno yako ambayo mara zote huwa unayatumia ni ya kihuni kihuni tuuu! Matendo yako ndiyo yanatoa jibunkuwa wewe ni muhuni. Acha tabia hizo kua wewe. Makufuli kiunoni ya nini?
 
Kazi yako ni jina lako. Kwenye avatar yako ulivyovaa tuu, bila shaka lolote wewe ni muhuni tuuu! Hiyo inajidhirisha kwa maneno yako ambayo mara zote huwa unayatumia ni ya kihuni kihuni tuuu! Matendo yako ndiyo yanatoa jibunkuwa wewe ni muhuni. Acha tabia hizo kua wewe. Makufuli kiunoni ya nini?

bora hata ningekuwa najibizana na ng'ombe.......nyau wewe!
 
Waambie wahuni wenzako ccm kuhusu katiba inayopendekezwa.....Watz wanataka katiba waliyoiwasilisha kupitia mzee wao wa heshima jaji joseph sinde warioba.
OCTOBER 2015 NDO MTAJUA KUWA WANANCHI NDO WENYE NCHI NA SIO ccm

Huko kote Oktoba 2015 mbona mbali nilijua unasema sasa hivi wananchi ndo wenye nchi ha ha ha ha u dont no what ua talking about!
 
Back
Top Bottom