Nonda,
..hofu ya Ukomunisti doesnt make much sense to me.
..lakini si Nyerere alikuja kuwa Mjamaa/Mkomunisti na tukawa na uhusiano wa karibu sana na Wachina?
..tena Nyerere akawatimua West Germany waliokuwa wakitushinikiza tuache mahusiano na East Germany. tulifungua ubalozi na East Germany kwasababu wao walikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa kutambua serikali ya Mapinduzi.
..halafu si Karume aliyenukuliwa akisema "Ujamaa mwisho Chumbe...."?!!
..tuchukulie kwamba ni kweli Nyerere alimtisha Karume kwamba usalama wake uko mashakani.
..sasa kama suala hilo lilikuwa la uongo basi Karume angeweza kuweka mguu chini na kukataa vitisho hivyo.
..lakini tunaona pia kwamba Tanganyika ilipeleka kikosi cha Polisi kusaidia Zanzibar, kwa msingi huo inawezekana kabisa kwamba hali ilikuwa tete huko visiwani.
..pia hivi kwa akili za kawaida tunaweza kubisha kwamba kikosi kilichompindua Sultani mwarabu kilikuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi ya mamluki kama Bob Denard aliyepindua Comoro, au wale walikodishwa na Holden Roberto wa Angola?
Nonda said:
Baada ya juhudi zote ambazo Karume na Serikali yake ya Kuitaka Zanzibar kama nchi, kuomba msaada huku na huko kufanikisha kumpindua « sultani » ili wajitawale katika nchi yao, wakubali kirahisi kuitowa Nchi yao kwa Nyerere na iwe mkoa au wilaya ?
..hapa umenena!!
..wanasiasa wa Zenj wanapenda muungano pale unapowafaidisha kimadaraka na kiuchumi.
..kuna waandishi wanadai Mzee Jumbe alianza kupinga Muungano baada ya kuona Nyerere amemtupa mkono ktk harakati za kutafuta mrithi wa nafasi ya Raisi wa Muungano.
..Maalim Seif naye baada ya kupata madaraka sasa msimamo wake kupinga muungano umefifia.
NB:
..kuna kipindi CUF walikuwa wakiita CCM "Catholic Church Movement." Maalim alikuwa haishi kuitukuza himaya ya Sultani iliyoshamiri kwa biashara ya utumwa. yaani ilikuwa kana kwamba analilia zama zile za Wabara kukamatwa utumwa zirudi tena.