KATIBA: Wazee wa CCM wampongeza JK

KATIBA: Wazee wa CCM wampongeza JK

Hao wazee sidhani hata kama wanajua nini maana ya katiba

Mkuu huu wimbo wa katiba unaimbwa tu, ukweli ni kwamba ni sehemu ndogo sana ya watanzania wanaoijua katiba. Tanzania hatuko kama Kenya, kenya hata lay men na women wanajua maana ya katiba na wajua vipengele vyake na wanajua inawaathiri vipi. Hapa kwetu Tanzania hata baadhi ya wabunge haaifahamu katiba zaidi ya kuiona.

Ni afadhari tuwaache wenye uelewa wa katiba wafanye kazi hii kwa niaba yetu, tukianza kuwasikiliza wazee wa CCM ambao hata katiba ya chama hawaijui vizuri, ni makosa makubwa.
 
Njaa tu inawasumbua Wazee hawa wa CCM, hekima zao wameweka pembeni kabisa na kutumiwa na mafisadi kila wanapoona umuhimu wa kuwatumia Wazee hawa.


Hao ni wazee wachache wa CCM wanaotumiwa na viongozi wa CCM kwa maslahi yao viongozi.

Kazi yao ni kupongeza tu, na always kupongeza, lolote linalosemwa na viongozi wa CCM.

Hawana lolote. Hata kama Kikwete angesema hataruhusu Katiba mpya, wazee hao wa CCM bado wangempongeza kwa 'kauli yake yenye busara'.

Shame on them!

Wazee wa ukweli wanateswa na Serikali kwa kunyimwa mafao yao na Jumuia ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.
 
Kwa kuangalia sura za hao wanaoitwa wazee na kofia zao, haihitaji hata form four kubaini kuwa hawajui watendalo. Ni wazee wa umri lakini watoto wa akili. Hiyo ndiyo sisiem.
 
ccmwazeekatiba.jpg



Hawa ni kama wazee wa CUF! Nadhani nimesomeka nasema tena hawa ni CUF sidhani kama ni CCM
 
wanavuruga maendeleo wakusanywe wote waka2pwe kwenye bwawa la mamba kama idamin alivo wa2paga viwete.
 
Hawa wazee wanatumika sana hata wenyewe sijui kama wanajua, lakini hii yote ni umasikini. Ukiwa masikini utajikomba tuu ili angalau upate kitu. Hivi wanajua kiasi gani wanaibiwa? Mbona hawasikiki kwenye dowans na mengine? Aah sometimes mimi hata sitaki kuwasikia.
 
Hawa wazee wanatumika sana hata wenyewe sijui kama wanajua, lakini hii yote ni umasikini. Ukiwa masikini utajikomba tuu ili angalau upate kitu. Hivi wanajua kiasi gani wanaibiwa? Mbona hawasikiki kwenye dowans na mengine? Aah sometimes mimi hata sitaki kuwasikia.

Nadhani ni umasikini wa kufikiri mkuu ungekazia na hilo, maana hata kwa kujikomba kwa watawala bado haiwaondolei umaskini wao.
 
Back
Top Bottom