Katiba ya Tanganyika itakuwa tayari lini?

Katiba ya Tanganyika itakuwa tayari lini?

Bin Faza

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
502
Reaction score
191
Wana JF

inaonekana wazi kwamba sasa Tz inaanza kupezuki kisiasa. Ripoti hii inatupa sisi Wazanizbar burudani masikioni na moyoni mwetu tukijuwa sasa uhuru wetu umekaribia.

Nanukuu makala haya

Na Nasra Abdallah

BARAZA la Katiba la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) linatarajia kutoa mapendekezo yake leo ya uundwaji wa Katiba mpya, huku likitaka kusitishwa kwa mchakato huo hadi hapo katiba ya Tanganyika itakapopatikana.

Hilo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa jana jijini Dar es Salaam, wakati wa kupitia kipengele kimoja baada ya kingine ndani ya rasimu ya Katiba mpya kulikofanywa na wajumbe wa baraza hilo wapatao 70 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Felix Nielema, mwanaharakati kutoka Wilaya ya Ngara, alisema rasimu hiyo inazungumzia muungano, hivyo kufanya iwe batili, kwani inawalazimisha Watanzania kuingia kwenye muungano bila ya kuwa na katiba yao.

“Jamani katika hili tunatakiwa tuwe makini sana, kwani hawa jamaa tayari wanatulazimisha kuingia kwenye mambo ambayo hatujashirikishwa. Hivyo rasimu hii isimamishwe kwanza, tupate kwanza katiba ya Tanganyika ili tukija kujadili suala la muungano tujue yapi yaingizwe katika muungano na yapi yaachwe,” alisema Nielema.

Wakili Frugence Masawe, alikosoa sura ya 10 ndani ya rasimu hiyo inayoelezea mambo ya mahakama ya muungano wakati ukweli ni kwamba suala la mahakama si la muungano.

Naye Mwangalizi wa Haki za Binadamu kutoka Ukerewe, Benjamin Mtebe, alisema katika kipengele cha uendeshaji wa Bunge, kinaeleza kwamba endapo hoja ya bajeti ya wizara fulani itapingwa na wabunge na kurudishwa kwa ajili ya marekebisho, ikipingwa tena kwa mara ya pili serikali ina uhalali wa kuipitisha hivyo hivyo.

Kutokana utaratibu huu, wajumbe waliokuwawakijadili kipengele hicho walipendekeza kuwa ni vema bajeti ikarekebishwa hata mara sita mpaka wabunge watakapoiridhia, kwani wao ndio wawakilishi wa wananchi.

Awali Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, HaroldSungusia, alisema baraza hilo limepewa kibalihalali na Tume ya Kurekebisha Katiba kuichambua rasimu ya Katiba mpya.
 
Hayo ndio maneno,lazima tuwe katiba yetu,ndiyo tuzungumzie swala la muungano na katiba yake.ila tumeburuzwa sana watanganyika.kumbe muungano ungevunjika tusingekuwa na katiba.hii ni hatareee!
 
Deiman

Hayo ndio maneno,lazima tuwe katiba yetu,ndiyo tuzungumzie swala la muungano na katiba yake.ila tumeburuzwa sana watanganyika.kumbe muungano ungevunjika tusingekuwa na katiba.hii ni hatareee!

tatizo ni kwamba nyinyi Watanganyika, mumesanifiwa na MTU MMOJA TU muliefikiri munamuamini kumbe alikuwa anakudanganyeni anakufanyeni watoto wadogo na akafanya atakavo na nyinyi nyoooote muliosoma na wasiosoma mukawa munampigia makofi na kuwacha kazi zenu kusikiliza hutoba zake zisizokwisha

kakunyimeni nchi yenu na kaliuwa jina la nchi lenu akaanza kukuiteni Tanzania bara jina lisilo na maana yoyote ya utaifa, badala ya Tanganyika jina linabeba utaifa wenu

leo hata nyinyi watanganyika munaona aibu kujiita watanganyika, hakuna geziti au TV au Radio inayosema nyinyi ni watanganyika, labda Tanganyika packers

Hii ni haki yenu munayopaswa kuisimamia na kuhakikisha jina lenu linarejea kama lilivokuwa..............
 
Back
Top Bottom