Katiba ya Tanzania haimtambui rais kama binadamu wa kawaida inamuona ni 'mungu'

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
2,471
Reaction score
3,768
Ndio maana sishangai rais kuipigia debe hii katiba maana inamfanya awe kiumbe wa daraja la juu kuliko viumbe vyote Tanzania.

Yaani hawezi kushtakiwa akiwa rais au hata baada ya kustaafu haitajalisha amefanya maovu kiasi gani.

Kwa maneno mengine rais wa Tanzania anaruhusiwa kuvunja katiba vyovyote apendavyo hana kinacho mguide sana sana anasukumwa na nia njema.

Na huu ndio ubatili wa katiba yenyewe maana tumeshuhudia kwenye mataifa ya wenzetu
Wakuu wa nchi hushtakiwa mahakamani na kukutwa na hatia na wanatumikia adhabu zao.
Kwa hiyo hawa Marais wa tanzania huwa tunawatoa sayari gani?
 
Naam! Akosei na atakiwi kusemwa ila sijajua ipo kwenye kifungu kipi kwenye katiba yetu kwamba rais ni mungu mtu.
 
Ndio maana wakati ule ukitaja jina la raisi lazima uanza na neno "Mtukufu"
 
Andika mungu sio Mungu. Moja ya urithi mbovu aliotuachia Hayati Nyerere ni hii katiba ya hovyo.
Sio swala la kumlaumu nyerere.
Kwa wakati wake ilikuwa sawa, kumbuka ilikuwa ni chama kimoja.
Katiba ilitakiwa kibadilika toka 1992.
 
Hakika shida ya nchi hii inaanzia hapo, maana mtu mmoja anakuwa ndiye nchi ndiye jeshi, polisi, mwajiri, bunge, mahakama yaani kila kitu cha mchi hii ni yeye na waliomzunguka.

Hivyo tunaposema katiba mpya machawa hayaelewi shida ya mtu mmoja kumiliki kila kitu ikiwa ni pamoja na uhai wa watu maana akisema tafuta fulani atoweke nconi mwamhu litatimia na hakuna cha kufanya.
PAMBANENI KUPATA KATIBA MPYA
 
Andika mungu sio Mungu. Moja ya urithi mbovu aliotuachia Hayati Nyerere ni hii katiba ya hovyo.
Naaam, katiba inayotegemea utashi wa mtu au mood zake. Siku akijisikia nchi nzima inaelekea huko juko
 
Utasikia wanufaika wanasema habari ya chakula mezani na si ni kitabu tu
 
Kwa Kisambaa anatambulika kama Imperial President! Yaani Rais mwenye mamlaka makubwa pasipo na sababu za msingi. Yaani Rais anayechukuliwa kama anaongoza ng'ombe, kondoo au misukule! badala ya binadamu.
 
 

Attachments

  • 1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 7
  • IMG-20260827-WA0012.jpg
    22.3 KB · Views: 8
Sio swala la kumlaumu nyerere.
Kwa wakati wake ilikuwa sawa, kumbuka ilikuwa ni chama kimoja.
Katiba ilitakiwa kibadilika toka 1992.
Yaa uko sahihi yaani tunachopaswa kufanya sasa ni kureiz awareness kwa kizazi kilichopo kuwaambia katiba tuliyonayo ni hatari sana kwa usalama wa taifa
 
mamlaka hutoka kwa Mungu mwenyewe sasa unashangaa vipi katiba kuliona hilo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…