Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,234
- 1,815
Ni kiwango kipi cha Uhuru kinakubalika na watawala kisiwe Uchochezi?
Kama Taifa tumetoa Uhuru (Demokrasia) pana sana kwenye sekta ya uchumi hasa Ubinafsishaji wa bei ya kutupwa ya mali na mashirika ya umma. Lakini tumebana sana na kwa kiwango cha kutisha Uhuru na Demokrasia ya mawazo kisiasa.
Uhuru wa kujieleza ni biashara ya mawazo/fikra yenye soko kamili kama ilivyo bidhaa nyingine yoyote sokoni. Kamwe si jukumu la serikali wala la yeyote yule kuamua ni wazo lipi au ni fikra ipi au ni habari ipi iwe halali, bali ni soko la mawazo ndio huamua. Soko la mawazo/fikra litaamua ni wazo au fikra au habari ipi ni sahihi hivyo habari ya uongo itashindwa bila amri au shuruti ya Serikali.
Udhibiti wa habari au mawazo/fikra huru ni kinyume cha Ibara ya 18 ya Katiba yetu ya mwaka 1977, na kwa kuzingatia Ibara hii ya Katiba kile ambacho watawala wanakiita Uchochezi ndio Uhuru wenyewe wa kujieleza ambao unalindwa na ibara hii.
Ni nani mwenye haki ya kuamua uhalali wa maoni na aina ya uhuru wa mawazo/fikra ya mtu katika kutekeleza haki hiyo ya kikatiba?
Ni kiwango gani cha Uhuru kinakubalika na watawala ili kisiwe uchochezi?
Uhuru/demokrasia lazima izingatie vigezo vya kimataifa
Nanyaro EJ