Katiba ya Tanzania yazidi kusiginwa , 8 waliojiuzulu udiwani Cuf Tanga na kujiunga na CCM wahudhuria kikao cha bajeti na kulipwa posho

ccm itavuna inachopanda
 
Watanzania tunasahau, serikali haziendeshwi kwa maneno wala mikutano ya kwenye majukwaa.

Kama hakuna barua ya kujiuzulu wala kufukuzwa, basi ni madiwani halali.
 
Write your reply...Hahahahaaa, inasikitisha sana kwa wapenda haki. Hata hivo sitarajii kusikia cuf wakilalamikia hili sbb mwasisi wa haya yote ni boss wao wa chama, kama alijiudhuru na baadaye kulala ofisini unategemea nini.
 
Mbona hujibu swali la msingi?

Kuna ushahidi kuwa wamejiuzulu au kufukuzwa? Hii ni legal issue, tusipende kuweka hisia.
Wamepokelewa na Katibu mkuu wa ccm mbele ya huyo huyo Mkurugenzi wa jiji , hatuandiki hizi taarifa kwa kutunga , hii si mara ya kwanza ccm kufanya hivi , haya yamekwishakutokea pia huko Tunduma
 
Ok lakini kama madiwani wangekuwa wametoka ccm na kujiunga na upinzani bila kumpa taarifa rasmi huyo mkurugenzi ni lazima wangezuiwa kushiriki vikao...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chama kitawafukuzaje watu ambao siyo wanachama wao tena na katika kikao wamekaa upande wa chama tawala?
 
Wamepokelewa na Katibu mkuu wa ccm mbele ya huyo huyo Mkurugenzi wa jiji , hatuandiki hizi taarifa kwa kutunga , hii si mara ya kwanza ccm kufanya hivi , haya yamekwishakutokea pia huko Tunduma
Hata kama angewapokea Rais mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi, hivi wewe leo mkurugenzi wa kampuni yako atangaze mbele ya watu kuwa umefukuzwa kazi bila kukupa barua, utakuwa umefukuzwa kazi kweli kisa "ametangaza" hadharani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…