Katiba ya zanzibar ndio sababu no 1 ya serikali tatu.

Katiba ya zanzibar ndio sababu no 1 ya serikali tatu.

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Nawashangaa wanaopiga kelele kuhusu mapendekezo ya SERIKALI TATU!
Bila hata kuangalia sababu zingine ,ni wazi Katiba ya Zanzibar inayotambua Zanzibar kama nchi ndio msingi mkubwa wa mapendekezo ya Muungano wwa kuwa na Serikali tatu!
wATANZANIA TAUCHE UNAFIKI WANAOPIGA KELELE SASA WALITAKIWA WALIONE HILO MAPEMA!
 
Ni hoja ambayo haina msingi wote tunajua kuwa mabadiliko ya katiba ya zanzibar yalivunja katiba ya muungano waliofanya hivyo walitakiwa washitakiwe sio kuunda katiba nyingine hii inamaanisha hata katiba ya sasa tunayoitaka haitaheshimiwa
 
mimi naona una hoja, yaani huo ndio ukweli, mfano Ibara ya 1 tu inasema Zanzibar ni nchi miongoni mwa nchi 2 za JMT, hiyo nchi nyingine ni ipi?
 
Du Kamanda uwashtaki wenye nchi waliojiamulia namna ya kuendesha mabo yao ...Watanganyika amkeni kusimamaia nchi yetu!
 
kwhyo unamaanisha kuwa walitakiwa kupiga kelele wakati katiba ya Zanzibar inatungwa?
 
Zanzibar haijavunja katiba ila bunge ndio lilokuwa la mwanzo kuvunja katiba kwa mambo ambayo sio ya mungano na kuyafanya kuwa ya mungano
 
Amavubi nchi ingine ni hiyo Tanganyika kwenye katiba haipo ila nyinyi mnaotoa timu yenu ya taifa hamuoni kua ipo
 
Ni hoja ambayo haina msingi wote tunajua kuwa mabadiliko ya katiba ya zanzibar yalivunja katiba ya muungano waliofanya hivyo walitakiwa washitakiwe sio kuunda katiba nyingine hii inamaanisha hata katiba ya sasa tunayoitaka haitaheshimiwa

Kwani hiyo Katiba ya Muungano inatoka kwa Mungu. Imetengenezwa na Watu 14 waliojifungia na kupata maelezo kutoka kwa Mungu mtu Nyerere. Kwani hiyo inayoitwa Katiba ya Muungano Si imevunja Hati ya Muungano mbona hakushtakiwa Nyerere?
 
Kuna vitu unachanganya kuna kutunga katiba na kuna kuheshimu katiba kama katiba haieshimiwi hata zitengenezwe katiba ngapi hazitakuwa na maana yoyote waliovunja katiba ya muungano kwa kutengeneza katiba ya zanzibar bila kufata taratibu walitakiwa waadhibiwe leo hii tumekuwa tukishabikia siasa za marekani wakati tunajua moja ya sababu iliyoifanya marekani kufika hapo ni kuheshimu katiba yao lakini sisi tunashabikia katiba mpya bila kuiwekea kinga
 
Kwani mawazo ya kuwa na serikali tatu yalianza lini na katiba ya Zanzibar ilikuja lini?
 
mimi naona una hoja, yaani huo ndio ukweli, mfano Ibara ya 1 tu inasema Zanzibar ni nchi miongoni mwa nchi 2 za JMT, hiyo nchi nyingine ni ipi?

JMT ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwani huo muungano ulikuwa wa mikoa au nchi?
 
Amavubi nchi ingine ni hiyo Tanganyika kwenye katiba haipo ila nyinyi mnaotoa timu yenu ya taifa hamuoni kua ipo

Kweli wewe mtu umefikiria na kutulia uzito kila kinachofanywa na pande zote. Kitendo cha kuwa na timu ya taifa la Tanzania bara maana yake kumbe Tanganyika ipo
 
Ndio maana tunasema Kuwa Tanganyika ipo lakini imejifunika mwavuli wa JMT
Mfano: timu ya T/Bara ipo inatumia jezi ambazo zina logo ya TFF chama cha mpira wa miguu Tanzania isitoshe kocha wa Taifa stars ndie Huyo pia anaetumiwa na Kilimanjaro stars timu ya taifa T/bara kocha ambaye anamfundisha CANAVARO wa Zanzibar heroes napia AMRI KYEMBA wa Kilimanjaro stars timu ya taifa moja ambalo ni JMT unadhani kihaki na usawa CANAVARO atakua radhi kocha huyo kumchukua AMRI KYEMBA na kumfundisha pembeni pekee yake wakati ni kocha wao wote ??
SWALI
(1) -KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA ANAITWAJE ?
(2) - KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA T/BARA ANAITWAJE ?
(3) - KOCHA WA TIMU YA TAIFA ZANZIBAR ANAITWAJE?
JIBU WEKA MOYONI MWAKO NAJUA UTAPATA FAIDA SANA NA HUTAMLAUMU WARIOBA NA TUME YAKE
MATUMIZI :
Ni wazi kua wakati timu hiyo inatumia kila kitu cha JMT (TFF) kuanzia jezi hadi kocha ni wazi kua hata pesa za kuendeshea timu hiyo ni za pamoja ila anazitumia Tanganyika kupitia kivuli cha JMT
MWISHO
Napenda kusema kua leo hii mchakato huu tulionao nadhani khitilafu kubwa kwenye michezo zitapata ufumbuzi
Nimejikita sana kuongelea michezo kwa sababu ni mpenzi wa sekta hiyo asanteni
 
Kwani mawazo ya kuwa na serikali tatu yalianza lini na katiba ya Zanzibar ilikuja lini?
yalianza wakatinchi zinaungana ,na yameendelea hivyo lakini yamekuwa yakizimwa kwa mkono wa chuma! Lakini kumbuka ni vigumu kuyazuia mawazo positive!
 
kimefika kipindi cha watu kujua haki zao mambo haya yanahitaji kufikiria juu ya hii serekali tatu maana hapa kuna kazi nzito
 
Back
Top Bottom