Katiba Zote Huandikwa, Kwanini Si Ya Uingereza...?

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,246
Ndugu zangu,

Majuzi hapa nilimsikia Profesa Maghembe wa Bunge Maalum la Katiba akimkosoa Mbunge mwenzake aliyetamka kwa makosa, kuwa Uingereza nao waliandika Katiba yao. Profesa Maghembe alikiri kuwa hakufahamu zaidi hayo ya Katiba ya Uingereza kwa vile yeye ni mwanasayansi.

Naam, ngoja mie nifafanue kidogo, hata kama si expert wa Sayansi ya siasa. Kila jambo lina sababu yake. Waingereza walikuwa na sababu zao za kwanini hawakuandika Katiba yao.

Na duniani hapa si Uingereza tu ambayo haina Katiba ya kuandikwa. Kuna nchi nyingine mbili; Israel na New Zealand. Na zote hizo, nazo zina sababu zake.

Kutokuwepo kwa Katiba za kuandikwa Uingereza na NewZealand kunachangiwa na nchi hizo kuwa na misingi imara ya muafaka wa kitaifa kwenye mambo ya msingi. Kwamba, hayo yanafanya uandishi wa Katiba, hata wakati huo, usionekane kuwa ni wa muhimu sana. Muafaka wa Kitaifa nao ni Katiba.

Israel wao walijaribu kuandika Katiba wakashindwa, wakaamua kuacha. Kwanini?

Waisrael hawakukubaliana kwenye mambo kadhaa ya kimsingi ikiwamo mahusiano ya dini na dola. Israel ina madhehebu kadhaa. Unaandikaje Katiba yenye kulinda haki za madhehebu yote hayo? Bora kuacha!

Na je wajua, Kuwa duniani hapa kuna nchi moja imeshindwa hata kufikia muafaka juu ya wimbo wake wa taifa.

Ni Hispania. Imegawanyika katika ya Catalansca na Baskien. Ndio chimbuko la Barcelona na Real Madrid. Maeneo hayo mawili katika nchi moja yana lugha mbili tofauti.

Sasa basi, swali likaja, wimbo wao wa taifa uimbwe kwa lugha gani?

Wakafikia muafaka kuwa uwe ni wimbo wa ala tu, bila sauti. Ndio maana, mpaka hii leo, ukiona Hispania inacheza mechi na wimbo wake wa taifa unapigwa, wachezaji wake huwa wamefunga midomo. Hawana cha kuimba!

Good morning!

Maggid Mjengwa
Iringa.
http://mjengwablog.com
 

Nchi hizo hazina katiba kwa sababu maalum.Sababu kubwa ni kuwa katika mambo ya sheria kuna waumini wa aina mbili.

Kundi la kwanza linaamini kuwa sheria zilizotungwa zinatosha kuendesha nchi na kuleta utengemano katika nchi wakati kuna kundi la pili linaamini kuwa pamoja na kutunga sheria mbalimbali lazima kuwe na sheria mama au baba inayoitwa katiba.

Kundi la wasio na katiba linaamini sheria zote ni sawa na kila mtu yuko sawa mbele ya kila sheria.wapenda kuwa na katiba wanaamini kuna sheria kuu kuliko zingine ambayo ni katiba hiyo ndio mama hizo zingine watoto na vitukuu vya sheria mama!!!!??

Kundi la kwanza la nchi zisizokuwa na katiba linaamini kuwa kama kuna sheria ya uhuru wa kutoa mawazo ipo tayari kwenye sheria mfano vya habari kuna haja gani tena uandike kwenye katiba kuwa kuna uhuru wa kutoa mawazo? Wanaamini sheria hiyo inatosha kulinda huo uhuru wa kutoa mawazo uwe wa kidini,kiuandishi n.k haihitaji tena watu wale posho watunge kipengele kingine eti cha sheria mama katiba tena! Ile sheria inatosha mtu akivunja adhabu zimo mule

Nchi ulizotaja zisizo na hicho kinachoitwa katiba sheria zinafanya kazi vizuri na zime-cover maeneo yote yawe madaraka ya raisi,mawaziri viongozi,masuala binafisi,mambo ya biashara n.k.Wanaamini zikishatungwa kazi ni kila mtu bila kujali cheo au hadhi kuzitii na kuzisimamia.Wao wanaishi kwa sheria sisi tunaishi kwa katiba na sheria.Wao hawataki duplication sababu mengi yanayotajwa kwenye katiba utashanga unaenda kuyakuta yamo katika sheria ambazo tayari zipo.Chukulia mfano katika katiba unasema mtu ana haki ya kuajiriwa bila kubaguliwa sheria ya ajira unakuta inataja hivyo tayari ni duplication tu ambazo nchi hizo zisizo na katiba ziliona ujinga mtupu kuwa kwa nini ukalishe watu wakopy na ku-paste yaliyoko kwenye sheria zingine yahamishiwe kwenye katiba?.

Sheria ndio msingi wa uendeshaji wa hizo nchi zisizo na hicho kinachoitwa katiba na sheria zote zinatambuliwa kama sheria mama usipozitii unalo.
 
Maelezo mazuri yenye kuvutia, namuunga mkono Maghembe, mimi ni mwana sayansi siyajui haya, mnao yafaham mtuelekeze.
 
maggid
Katiba Zote Huandikwa, Kwanini Si Ya Uingereza...?



Wacha kudanganya watu. Katiba ya New Zealand imeandikwa.
I quote:
"New Zealand is often incorrectly described as not having a "written constitution". New Zealand has a constitution, but it is not all in one document, and it includes crucial pieces of legislation, several legal documents, common law derived from court decisions as well as established constitutional practices known as conventions. Increasingly, New Zealand's constitution reflects the Treaty of Waitangi as a founding document of government in New Zealand."
source:
https://gg.govt.nz/role/constofnz.htm

Sasa wewe nani ka kwambia kuwa New Zealand haina katiba ya kuandika?
 
Maelezo mazuri yenye kuvutia, namuunga mkono Maghembe, mimi ni mwana sayansi siyajui haya, mnao yafaham mtuelekeze.

Sayansi ipi kwa hakusoma siasa/uraia/development studies (DS)-political economy of capitalism/socialism au The origin of the state by Lenin?? enzi zake za primary/sekondary?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…