Ndugu zangu,
Majuzi hapa nilimsikia Profesa Maghembe wa Bunge Maalum la Katiba akimkosoa Mbunge mwenzake aliyetamka kwa makosa, kuwa Uingereza nao waliandika Katiba yao. Profesa Maghembe alikiri kuwa hakufahamu zaidi hayo ya Katiba ya Uingereza kwa vile yeye ni mwanasayansi.
Naam, ngoja mie nifafanue kidogo, hata kama si expert wa Sayansi ya siasa. Kila jambo lina sababu yake. Waingereza walikuwa na sababu zao za kwanini hawakuandika Katiba yao.
Na duniani hapa si Uingereza tu ambayo haina Katiba ya kuandikwa. Kuna nchi nyingine mbili; Israel na New Zealand. Na zote hizo, nazo zina sababu zake.
Kutokuwepo kwa Katiba za kuandikwa Uingereza na NewZealand kunachangiwa na nchi hizo kuwa na misingi imara ya muafaka wa kitaifa kwenye mambo ya msingi. Kwamba, hayo yanafanya uandishi wa Katiba, hata wakati huo, usionekane kuwa ni wa muhimu sana. Muafaka wa Kitaifa nao ni Katiba.
Israel wao walijaribu kuandika Katiba wakashindwa, wakaamua kuacha. Kwanini?
Waisrael hawakukubaliana kwenye mambo kadhaa ya kimsingi ikiwamo mahusiano ya dini na dola. Israel ina madhehebu kadhaa. Unaandikaje Katiba yenye kulinda haki za madhehebu yote hayo? Bora kuacha!
Na je wajua, Kuwa duniani hapa kuna nchi moja imeshindwa hata kufikia muafaka juu ya wimbo wake wa taifa.
Ni Hispania. Imegawanyika katika ya Catalansca na Baskien. Ndio chimbuko la Barcelona na Real Madrid. Maeneo hayo mawili katika nchi moja yana lugha mbili tofauti.
Sasa basi, swali likaja, wimbo wao wa taifa uimbwe kwa lugha gani?
Wakafikia muafaka kuwa uwe ni wimbo wa ala tu, bila sauti. Ndio maana, mpaka hii leo, ukiona Hispania inacheza mechi na wimbo wake wa taifa unapigwa, wachezaji wake huwa wamefunga midomo. Hawana cha kuimba!
Good morning!
Maggid Mjengwa
Iringa.
http://mjengwablog.com