Katibu Baraza la Kata jela miaka mitatu kwa rushwa

Katibu Baraza la Kata jela miaka mitatu kwa rushwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mahakama ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imemhukumu Katibu wa Baraza la Kata ya Binza wilayani humo, Daud Willison Elias kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh 500,000 baada ya kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya Sh 50,000.

Hukumu hiyo ilitolewa Jana na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Enos Misana baada ya mshitakiwa kukiri kosa lake.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU), Carson Nkya aliieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda kosahilo Juni 6, mwaka huu na kufunguliwa kesi ya jinai Na38/2021.

Alidai mshitakiwa akiwa Katibu wa Baraza la Kata hiyo aliomba kiasi hicho cha fedha kwa Mussa Jigeleka ili aweze kumwandikia hukumu yenye upendeleo katika shauri la madai lililokuwa linamkabili kwenye baraza hilo.

Mwendesha mashitaka huyo alizidi kuieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa awali aliomba kiasi cha Sh 70,000 lakini baada walikubaliana kuwa atoe kiasi cha Sh 50,000 tu.

Nkya alizidi kueleza kuwa baada ya Takukuru kupata taarifa hizo walitengeneza mtego na kumkamata mjumbe wa baraza la Kata hiyo, Emanuel Paul Gibe ambaye alitumwa kupokea fedha hizo na kukamatwa Juni 16 mwaka huu.

Nkya alidai kuwa kosa alilofanya mshitakiwa ni kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2017.

Chanzo: Millard Ayo
 
Kwahiyo ameshindwa kulipa hiyo laki 5?...Manguli ya kula rushwa yanapeta tu kitaa.
 
safi.
bado rushwa ni kero ktk vyombo vinavyo toa Haki, baadhi yao bado wanaomba rushwa, wanekuwa kero mno!
TAKUKURU pigeni KAMBI kwenye maeneo hayo naamini kila siku mtawanasa wala rushwa wasumbufu, kamwe msikae maofisini mkasubiria mletewe tu taarifa, wekeni kambi kwenye maeneo hayo, lkn kwa kujificha bila kujulikana.
 
Jela ni kwa ajili ya watu masikini huwezi sikia majizi makubwa kama kina chenge,dau,mzindaakaya, bashite,kakoso wakiingia huko ni watumishi wanaodokoa Ili alipe kodi,au ada.Na sio ma papa
 
Back
Top Bottom