Wanabodi
Katibu kata wa CHADEMA kata ya Enduleni Ngorongoro ameshikiliwa kituo kikuu cha polisi Arusha, baada ya mtego aliowekewa kumnasa, Katibu huyu Denis Paulo alijifanya kuwa ni Katibu mkuu wa wizara ya utalii, kisha kumpigia Mhifadhi utalii wa NCAA Bi Veronica na kumtaka atoe Mil I6, ili kumsaidia kwenye tume iliyoundwa na waziri kuchunguza ubadhirifu mkubwa kwenye mamlaka hiyo.
Baada ya mahojiano na polisi Katibu huyo amekana kujua chochote, nilikutana na Nanyaro ambaye ni mmoja wa viongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha, na akakiri kumwekea dhamana polisi, ni kweli huyu ni katibu wa chama kata ya enduleni, nimemdhamini kwa masharti kuwa aripoti kituoni kesho asubuhi, mazingira ya kukamatwa kwake yanatia mashaka sana,
Ukumbuke kuwa Katibu huyu alifanikisha kuhamisha zaidi ya wanachama 2800 wa CCM wakahamia CHADEMA, mapema mwaka huu, kesho nitakuwa kwenye nafasi nzuri ya kulizungumzia baada vingozi wenzangu, alisema Nanyaro