Pre GE2025 Katibu Mkuu ACT Wazalendo, Ado Shaibu: Rais Samia ajitathimini

Pre GE2025 Katibu Mkuu ACT Wazalendo, Ado Shaibu: Rais Samia ajitathimini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Maazimio ya Halmashauri Kuu

Halmashauri Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo imekutana kwenye kikao chake cha kawaida jana tarehe 23 Februari 2025 katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo katika Jengo la Maalim Seif (Makao Makuu ya Chama).

Kikao hicho kilipokea na kujadili Taarifa ya Uvurugaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, Hali ya Kisiasa Nchini na Mwelekeo wa Chama katika Kukabiliana na Mazingira mabovu ya Chaguzi nchini.

Baada ya mjadala wa kina, Halmashauri Kuu iliazimia kama ifuatavyo;

1. Kwamba kipaumbele cha Chama kwa sasa ni kupigania maboresho ya mfumo wa uchaguzi nchini utakaohakikisha HAKI na kuheshimiwa maamuzi na matakwa ya wananchi. Halmashauri Kuu imeelekeza kwamba suala la kushiriki ama kutoshiriki Uchaguzi kabla ya kufanyika marekebisho yanayotakiwa litaamuliwa na Kamati ya Uongozi ya Taifa katika wakati muafaka.

2. Halmashauri Kuu ya ACT Wazalendo imejiridhisha kuwa maridhiano yaliyoahidiwa na Rais Samia Suluhu Hassan yamesambaratika na falsafa yake ya 4R imeota mbawa.
Ikumbukwe kwamba Chama cha ACT Wazalendo, vyama vingine vya upinzani na wadau wengine wa demokrasia nchini walimuunga mkono Rais Samia kutokana na ahadi yake ya kuboresha mazingira ya kisiasa nchini ikiwemo kuhakikisha kwamba chaguzi zinakuwa huru, za haki na za kuaminika. Halmashauri Kuu imejiridhisha kuwa hakukuwa na utashi wa kisiasa kutekeleza ahadi hii.

Hivyo basi, Halmashauri Kuu inamtaka Rais Samia kujitathmini juu ya tofauti iliopo baina ya ahadi anazotoa kwa maneno na kukosekana kwa vitendo katika kutekeleza ahadi hizo. Mh. Rais ajiulize swali muhimu: Yanapojengwa mazingira ya ahadi za Rais kutoaminika, wananchi wamuamini nani?

3. Halmashauri Kuu imeelekeza kuwa Chama kifanye uchambuzi na kuandaa ripoti ya kina juu ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu nchini vilivyofanywa na vinavyoendelea kufanywa na Serikali za Chama cha Mapinduzi (Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar) yakiwemo matukio ya mauaji na utekaji na madhila ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

4. Kwa upande wa Zanzibar, ACT Wazalendo kinayo ripoti ya kina juu ya mauaji ya raia 21 na matukio mengine ya ukatili wa kutisha yaliyofanyika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020. Pia, chama kimekusanya vitendo vyote vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Zanzibar tangu mwaka 2020-2025.

Halmashauri Kuu imeelekeza Ripoti hizo zichapishwe na kupelekwa kwa wadau wa demokrasia nchini pamoja na jumuiya ya kimataifa ikiwemo taasisi za fedha za kimataifa na pia kushirikiana na taasisi hizo kufikisha kesi katika Mahakama za Kimataifa.

5. Halmashauri Kuu imeelekeza kuwa Chama cha ACT Wazalendo kiendeleze ushirikiano na vyama vingine makini vya upinzani na wadau wengine muhimu wa demokrasia ikiwemo Asasi za Kiraia na viongozi wa dini katika kujenga vuguvugu la kitaifa la kupigania maboresho ya mfumo wa uchaguzi nchini.

6. Halmashauri Kuu imeelekeza Chama kiandae operesheni kubwa ya kulinda demokrasia nchini Tanzania itakayojulikana kama OPERESHENI LINDA DEMOKRASIA. Lengo la operesheni hiyo ni kuhamasisha umma wa Watanzania kupigania haki zao na kutokubali kuwa wanyonge.

7. Halmashauri Kuu imeelekeza Chama kijikite katika kupigania maboresho ya mfumo wa uchaguzi nchini ikiwemo kufanyika kwa mabadiliko madogo ya katiba (minimum constitutional reforms), kuundwa kwa Tume Huru za Uchaguzi (NEC na ZEC kwa upande wa Zanzibar) na kupinga kwa nguvu zote kura ya mapema kwa upande wa Zanzibar.

HITIMISHO:

Wanachama na viongozi kwenye ngazi zote wanaelekezwa kujiandaa kwa ajili ya mapambano ya kuilinda na kuitetea demokrasia nchini Tanzania ili kura ya kila mwananchi iweze kuwa na thamani. Muda wa kubembeleza mageuzi umekwisha sasa ni muda wa mapambano!

Ado Shaibu
Katibu Mkuu ACT Wazalendo
Feb 24, 2025
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

1740396131860.png

1740396148018.png
 
1. Falsafa ya 4R haijasambaratika bali inatekelezwa kwa vitendo

ACT Wazalendo wanadai kuwa maridhiano yamesambaratika, lakini ushahidi wa matendo ya Serikali unathibitisha vinginevyo:

Maridhiano (Reconciliation): Serikali ya Rais Samia imeshiriki katika majadiliano na vyama vya siasa kupitia Kikosi Kazi cha Demokrasia kilicholeta mapendekezo mbalimbali ya maboresho ya kisiasa.

Ujenzi wa Upya (Rebuilding): Vyombo vya habari vya upinzani kama Mwanahalisi na Mawio vilifunguliwa, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa imeruhusiwa, na Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi.

Ustahimilivu (Resilience): Serikali inajenga mazingira ya kisiasa yenye uvumilivu wa hoja tofauti badala ya mivutano isiyo na tija.

Mageuzi (Reforms): Marekebisho ya sheria za uchaguzi yanaendelea kujadiliwa bungeni, ikionyesha utayari wa Serikali kuleta mabadiliko yenye tija badala ya siasa za malalamiko.

Kwa hiyo, hoja kwamba 4R imefeli ni propaganda isiyo na msingi.

2. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa haukuwa wa vurugu, bali changamoto chache hazimaanishi mfumo mbovu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekuwa na changamoto ndogo kama inavyotokea katika kila mfumo wa demokrasia, lakini Serikali imekuwa tayari kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa sheria.

ACT Wazalendo wanataka kutengeneza taswira ya uchaguzi mbovu kwa sababu walishindwa vibaya. Badala ya kukubali matokeo na kufanya tathmini ya mapungufu yao, wanatafuta visingizio.

Uchaguzi huu ulisimamiwa kwa uwazi, na hakuna ushahidi wa kitaalamu unaothibitisha kuwa ulivurugwa kwa kiwango kinachotajwa na ACT Wazalendo.

3. Hakuna uhaba wa utashi wa kisiasa – Serikali inafanya mabadiliko kwa njia ya mchakato rasmi

Mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hayawezi kufanywa kwa haraka na kwa shinikizo la chama kimoja pekee. Serikali inafuata mchakato wa kisheria unaoshirikisha Bunge, Tume ya Uchaguzi, na wadau wengine.

ACT Wazalendo wanadai kuwa hakuna utashi wa kisiasa, lakini ukweli ni kwamba Serikali imefungua majadiliano na vyama vya siasa, imewezesha uchaguzi wa marudio uliofanyika kwa utulivu, na inazingatia mapendekezo ya maboresho.

4. Serikali haijashindwa kulinda haki za binadamu – ACT Wazalendo wanatumia propaganda za uongo

ACT Wazalendo wanadai kuwa kuna mauaji na utekaji wa watu, lakini hawatoi ushahidi wowote wa uhakika unaokubalika kisheria.

Serikali ya Awamu ya Sita imeimarisha haki za binadamu kwa kuruhusu vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru, kuondoa vikwazo kwa asasi za kiraia, na kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu Zanzibar, ni ajenda ya ACT Wazalendo kupotosha ukweli kwa kuwa walishindwa uchaguzi wa 2020 na sasa wanajaribu kueneza hofu kwa jamii.

5. Operesheni Linda Demokrasia ni propaganda ya kichochezi, si hoja ya kweli ya kuimarisha mfumo wa uchaguzi

ACT Wazalendo wanazungumzia "mapambano" dhidi ya Serikali iliyo madarakani kihalali, jambo linaloashiria siasa za vurugu badala ya kushiriki mchakato wa kidemokrasia.

Wanataka kutumia propaganda ya "kupigania haki" wakati ukweli ni kwamba mfumo wa uchaguzi unarekebishwa kwa njia rasmi, na wana nafasi ya kutoa maoni yao ndani ya mfumo huo.

Hitimisho: Serikali ya Rais Samia imeleta mageuzi makubwa, ACT Wazalendo wanapotosha ukweli

Tangu Rais Samia aingie madarakani, amefungua uwanja wa siasa kwa maridhiano, uhuru wa vyombo vya habari, na mchakato wa mabadiliko ya sheria.

Hoja za ACT Wazalendo zina misukumo ya kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa hali ya kisiasa nchini.

Serikali inaendelea kusimamia haki, demokrasia, na maendeleo ya taifa kwa utaratibu wa kisheria, si kwa shinikizo la propaganda za vyama vya siasa.
 
Hongereni ACT.
Kama haya ni maamuzi yenu kweli, nawapongeza na naomba myasimamie kweli na msiyakiuke.

Taifa hili linatuhitaji sote kuwa wakweli sasa na kuliweka sawa kwa faida ya vizazi vinavyokuja. Tusiposimama kwenye nafasi zetu sasa, vizazi vyetu vitalaaniwa.
 
Mkumbusheni. Raisi wa machawa, ukiona unaimbiwa mapambio sana ni either wewe ni dictator au haupo sawa
 
Wewe jamaa ni zwazwa sana.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao nyie CCM mlipaswa at least kuwaonesha Watanzania kuwa mmefanya reforms za kweli ndo mliubaka vibaya sana kwa kuondoa maelfu na maelfu ya wagombea wa upinzani.

Msidhani Watanzania ni wajinga. Narudia tena msidhani Watanzania ni wajinga. TANZANIA ni nchi yetu sote. Kubalini mabadiliko kwa amani maana yakipatikana kwa fujo mtakuja kuwajibishwa vibaya sana nyie na vizazi vyenu
1. Falsafa ya 4R haijasambaratika bali inatekelezwa kwa vitendo

ACT Wazalendo wanadai kuwa maridhiano yamesambaratika, lakini ushahidi wa matendo ya Serikali unathibitisha vinginevyo:

Maridhiano (Reconciliation): Serikali ya Rais Samia imeshiriki katika majadiliano na vyama vya siasa kupitia Kikosi Kazi cha Demokrasia kilicholeta mapendekezo mbalimbali ya maboresho ya kisiasa.

Ujenzi wa Upya (Rebuilding): Vyombo vya habari vya upinzani kama Mwanahalisi na Mawio vilifunguliwa, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa imeruhusiwa, na Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Uchaguzi.

Ustahimilivu (Resilience): Serikali inajenga mazingira ya kisiasa yenye uvumilivu wa hoja tofauti badala ya mivutano isiyo na tija.

Mageuzi (Reforms): Marekebisho ya sheria za uchaguzi yanaendelea kujadiliwa bungeni, ikionyesha utayari wa Serikali kuleta mabadiliko yenye tija badala ya siasa za malalamiko.

Kwa hiyo, hoja kwamba 4R imefeli ni propaganda isiyo na msingi.

2. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa haukuwa wa vurugu, bali changamoto chache hazimaanishi mfumo mbovu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umekuwa na changamoto ndogo kama inavyotokea katika kila mfumo wa demokrasia, lakini Serikali imekuwa tayari kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa sheria.

ACT Wazalendo wanataka kutengeneza taswira ya uchaguzi mbovu kwa sababu walishindwa vibaya. Badala ya kukubali matokeo na kufanya tathmini ya mapungufu yao, wanatafuta visingizio.

Uchaguzi huu ulisimamiwa kwa uwazi, na hakuna ushahidi wa kitaalamu unaothibitisha kuwa ulivurugwa kwa kiwango kinachotajwa na ACT Wazalendo.

3. Hakuna uhaba wa utashi wa kisiasa – Serikali inafanya mabadiliko kwa njia ya mchakato rasmi

Mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hayawezi kufanywa kwa haraka na kwa shinikizo la chama kimoja pekee. Serikali inafuata mchakato wa kisheria unaoshirikisha Bunge, Tume ya Uchaguzi, na wadau wengine.

ACT Wazalendo wanadai kuwa hakuna utashi wa kisiasa, lakini ukweli ni kwamba Serikali imefungua majadiliano na vyama vya siasa, imewezesha uchaguzi wa marudio uliofanyika kwa utulivu, na inazingatia mapendekezo ya maboresho.

4. Serikali haijashindwa kulinda haki za binadamu – ACT Wazalendo wanatumia propaganda za uongo

ACT Wazalendo wanadai kuwa kuna mauaji na utekaji wa watu, lakini hawatoi ushahidi wowote wa uhakika unaokubalika kisheria.

Serikali ya Awamu ya Sita imeimarisha haki za binadamu kwa kuruhusu vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru, kuondoa vikwazo kwa asasi za kiraia, na kushughulikia malalamiko kwa mujibu wa sheria.

Kuhusu Zanzibar, ni ajenda ya ACT Wazalendo kupotosha ukweli kwa kuwa walishindwa uchaguzi wa 2020 na sasa wanajaribu kueneza hofu kwa jamii.

5. Operesheni Linda Demokrasia ni propaganda ya kichochezi, si hoja ya kweli ya kuimarisha mfumo wa uchaguzi

ACT Wazalendo wanazungumzia "mapambano" dhidi ya Serikali iliyo madarakani kihalali, jambo linaloashiria siasa za vurugu badala ya kushiriki mchakato wa kidemokrasia.

Wanataka kutumia propaganda ya "kupigania haki" wakati ukweli ni kwamba mfumo wa uchaguzi unarekebishwa kwa njia rasmi, na wana nafasi ya kutoa maoni yao ndani ya mfumo huo.

Hitimisho: Serikali ya Rais Samia imeleta mageuzi makubwa, ACT Wazalendo wanapotosha ukweli

Tangu Rais Samia aingie madarakani, amefungua uwanja wa siasa kwa maridhiano, uhuru wa vyombo vya habari, na mchakato wa mabadiliko ya sheria.

Hoja za ACT Wazalendo zina misukumo ya kisiasa zaidi kuliko uhalisia wa hali ya kisiasa nchini.

Serikali inaendelea kusimamia haki, demokrasia, na maendeleo ya taifa kwa utaratibu wa kisheria, si kwa shinikizo la propaganda za vyama vya siasa.
 
ACT ya Kweli.. Hayoo au ndo vile..!!!???
 
Back
Top Bottom