Pre GE2025 Katibu mkuu BAVICHA: CCM inatufanya tuendelee kuwa masikini hali yakuwa wao wana maisha mazuri

Pre GE2025 Katibu mkuu BAVICHA: CCM inatufanya tuendelee kuwa masikini hali yakuwa wao wana maisha mazuri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana CHADEMA Dua Lyamzito amesema uwepo wa Chama cha Mapinduzi madarakani unaendelea kuwafanya wantanzania kuwa maskini hali yakuwa wao(CCM) wanakua na maisha mazuri.

Akizungumza akiwa Kibanga, Muleba mkoani Kagera Dua amesema “kwetu Karambi nikienda miaka mitano nikirudi napakuta vilevile unadhani hii ni kwa sababu ya Mungu, Mungu ndiye anaamua mtu mmoja anaweza akala chakula akatupa na mwingine akakosa vile vile? kuna watu wanaitwa CCM wako ofisini wamesababisha sisi tule au tufe njaa”

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Dua ameongeza kuwa ni maamuzi ya wananchi kuendelea kuiamini CCM na waendelee kuishi maisha magumu ya kushindwa hata kupata mlo au kuitoa madarakani ili waweze kumudu maisha yao na hata kukidhi mahitaji yao ya msingi kama chakula.

 
Unashangaa kupakuta vilevile kwani wewe umefanya nini kupaendeleza? Mie nakaa Mwanza, lakini nyumbani Kiziba nimejenga na mdogo wangu nimemwekea ka biashara. Wewe hujafanya chochote halafu unalalamika eti hapajabadilika! PUMBAVU!!
 
Kuchagua ccm ni kuchagua umasikini katana ccm na genge lake katana kizimkazi na chawa wake
 
Back
Top Bottom