Kwa hii kauli ya Samia maana yake maneno aliyoandika Chongolo jana kuhusu kujiuzulu kwake ni ya kweli, amesingiziwa uongo, hivyo akaamua kujiuzulu ili kulinda hadhi yake na ya chama chake.
Tatizo linakuja, kama issue ya Gekul Samia aliweza kuchukua hatua, jambo linaloonesha alishauriwa na vyombo vyake vya usalama, iweje kwa hili la Chongolo Samia atuambie anafuatilia?
Kwanini asingefuatilia ili kujiridhisha halafu watakapokutana kwenye hiki kikao chao awe na jibu kamili? au Samia anataka kutuaminisha hili la Chongolo linekuja ghafla sana kuzidi lile la Gekul?
Hapa Samia ameamua kufunika kombe mwanaharamu apite, baada ya muda wamteue KM mpya maisha yaendelee, kwa maana nyingine kapigwa bao na Chongolo.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app