Katibu Mkuu CCM weka alama Tanga

Katibu Mkuu CCM weka alama Tanga

Tumbu

Senior Member
Joined
May 27, 2021
Posts
109
Reaction score
96
Mh. Daniel Chongolo Katibu Mkuu wa chama tawala,ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ukiwa ziarani Tanga ninajua sipo nje ya ajenda zako lakini ninakupa dondoo kidogo kwamba kero zilizopo Tanga ni.
Migogoro ya ardhi iliyosababishwa na Shigela,Mayeji na kikosi kazi chao cha kupora ardhi kwa maskini na kuuzia matajiri. Pamepigwa hela nyingi sana. Migogoro hiyo ya ardhi ilisababisha vifo na mkuu wa wilaya ndugu Mwilapo aliambiwa lakini hajafanya kitu. Ingawaje aliunda kamati ya kuchunguza sababu za mgogoro na madhara yake lakini hakufua dafu mbele ya Shigela na Mayeji na kikosi kazi chao.
Lukuvi alikuja wakamzonga,wakamfungia kwenye chumba wakamdanganya na kilichotokea Lukuvi ziara yake haikua na afya kwa wakaazi wa Tanga.

Mh. Chongolo hao angalia wasije wakakuzonga. Tena wana nguvu za ziada hata hawataki viongozi waje. Wakiweka vitu vyao mahali Tanga huingii.
 
Back
Top Bottom