Katibu Mkuu CHADEMA Kanda ya Kaskazini ajiuzulu nafasi hiyo na kujivua uanachama

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan amejiondoa rasmi katika nafasi yake pamoja na kujivua uanachama wa chama hicho, akieleza kuwa uamuzi huo umetokana na sababu binafsi.

Katika barua yake ya kujiuzulu ya tarehe 01 Aprili 2026, aliyokuwa ameielekeza kwa Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, kiongozi huyo ameeleza kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kutafakari kwa kina, akisema hana tena nia ya kuendelea kushika wadhifa huo ndani ya chama.

Ameongeza kuwa pamoja na kujiuzulu, pia ameamua kujivua uanachama wake wa CHADEMA, hatua inayohitimisha rasmi ushiriki wake katika shughuli za kisiasa kupitia chama hicho.

Katika barua hiyo, ametoa shukrani kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho Kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake.

Aidha, ameomba chama hicho kumpa nafasi ya kuendelea na shughuli zake binafsi nje ya mfumo wa kisiasa, huku akisisitiza kuwa ataendelea kuheshimu misingi ya demokrasia na utawala bora.

Jambo TV imemtafuta Ndondi ambapo amedhibitisha kumuandikia katibu mkuu barua hiyo lakini hakuwa tayari kuzungumzia zaidi uamuzi huo

Hadi sasa, uongozi wa CHADEMA haujatoa tamko rasmi kuhusu uamuzi huo.

1775049781482.png

1775049810433.png
 
Source: Jambo TV
Gentleman,
mtu mwenye malengo ya kisiasa na maono ya kijamii na kiuchumi,
kamwe hawezi kuvumilia au kung'ang'ana kuishi ndani ya kachama kalikojaa viongozi ombaomba, waropokaji na waliopoteza uelekeo kabisa kisiasa.

hakuna chama hapo ndugu zangu.
well done kamanda kuachana na hao malofa waropokaji
 
WhatsApp Image 2026-04-01 at 15.38.45.jpeg
Mhe. Katibu Mkuu,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

YAH: KUJIUZULU NAFASI YA KATIBU WA KANDA - KASKAZINI​

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.
Kwa heshima kubwa ninapenda kujulisha kuwa ninajiuzulu nafasi yangu ya ukatibu wa Kanda ya Kaskazini kuanzia leo hii tarehe 01.04.2026. Kutokana na majukumu yangu mapya nimeamua kujivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo rasmi kuanzia sasa.

Nashukuru Kamati Kuu ya chama kwa imani yao kubwa juu yangu na kwako binafsi kwa kipindi ambacho tumefanya kazi pamoja. Pia niwashukuru viongozi na wanachama wote wa Chadema Kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano walionipatia. Nawatakia mapambano mema

Wako katika Demokrasia,
KUJIUZULU NAFASI YA KATIBU WA KANDA_page-0001.jpg
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini, Ndonde Totinan amejiondoa rasmi katika nafasi yake pamoja na kujivua uanachama wa chama hicho, akieleza kuwa uamuzi huo umetokana na sababu binafsi.

Katika barua yake ya kujiuzulu ya tarehe 01 Aprili 2026, aliyokuwa ameielekeza kwa Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, kiongozi huyo ameeleza kuwa amefikia hatua hiyo baada ya kutafakari kwa kina, akisema hana tena nia ya kuendelea kushika wadhifa huo ndani ya chama.

Ameongeza kuwa pamoja na kujiuzulu, pia ameamua kujivua uanachama wake wa CHADEMA, hatua inayohitimisha rasmi ushiriki wake katika shughuli za kisiasa kupitia chama hicho.

Katika barua hiyo, ametoa shukrani kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho Kanda ya Kaskazini kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake.

Aidha, ameomba chama hicho kumpa nafasi ya kuendelea na shughuli zake binafsi nje ya mfumo wa kisiasa, huku akisisitiza kuwa ataendelea kuheshimu misingi ya demokrasia na utawala bora.

Jambo TV imemtafuta Ndondi ambapo amedhibitisha kumuandikia katibu mkuu barua hiyo lakini hakuwa tayari kuzungumzia zaidi uamuzi huo

Hadi sasa, uongozi wa CHADEMA haujatoa tamko rasmi kuhusu uamuzi huo.

Source: Jambo TV
Tayari kafika bei. Pesa zilizochotwa kifisadi zimeanza kutumika.
 
Kujiuzuru uongozi ndani ya chama ni jambo moja; tofauti kabisa na kujiondoa hata ndani ya chama.

Huyu hakuwa mwamini chochote inachokisimamia CHADEMA.

Niunganishe fikra hapa:

Hivi kule CCM ni viongozi wangapi ndani ya chama hicho waliowahi kujiuzuru: au wanachama tu kujiondoa ndani ya chama hicho?

Kuna maelezo yanayojitosheleza kuonyesha utofauti huu?
CCM mambo ni shwari kabisa, ila huko kwingine kila mara ni viongozi na wanachama kuvurugana tu!
 
Wameanza vile vidrama vyao vya mwaka jana kuanzia March hadi May , wanalipiwa press na script ya kusoma kutoka CCM.

Yote hayo ni kuhamisha mjadala wa kesi ya Lissu, ripoti ya CAG na ionekane CHADEMA kuna mpasuko.

Ninawapa pole watangayika kwa sasa wamekataa hadaa , kama hawaamini wawaulize Chaumma kwanini walipotea mapema kwenye maigizo yao.
 
BAJETI YA MANUNUZI YA BINADAMU IMESHAANZA KUFANYA KAZI.

WATU HAWANA AKILI UNAPOTEZA PESA KUNUNUA WATU UNAFIKIRI WATAISHA? YAANI AKITOKA HUYO ANAKUJA MWINGINE USIKUTE NDO ATAKUWA WA MOTO ZAIDI.

MNAHARINU PESA ZA WALIPA KODI
 
Back
Top Bottom